JOTO LA MPAMBANO KATI YA TAIFA STARS NA THE ELEPHANTS LAANZA KUPANDA!!

Bodi ya Utalii TTB ikishirikiana na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF wameanza kampeni ya kuhamasisha umma wa watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia timu yao ya Taifa Taifa Stars wakati itakapopambana na timu ya taifa ya Cote d, Voire (Ivory Coast) katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa januari 4 kwenye uwanja wa Taifa.
Katika kampeni hii wanategemea kuweka mabango makubwa na madogo ya matangazo ikiwa ni pamoja na vipeperushi, matangazo ya redio, magazeti na televisheni pamoja na vijarida ili kuhamasisha mashabiki mbalimbali kujitokeza na kwenda kushangilia timu yao kama inavyoonekana katika kipeperushi hiki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment