MAANDALIZI YA KUPOKEA WAGENI WORLD CUP 2010 HAPA NCHINI YANAKWENDA VYEMA- DR.KAWAMBWA!!

Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Wizara hiyo leo asubuhi wakati alipoelezea maandalizi ya kamati hiyo juu ya kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo.
Dr. Kawambwa amesema jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni hiyo ikiwa ni mambo ya matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni wengine baadhi ya mambo wakati watakapokuwa hapa nchini, mpaka sasa televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.
Ameongeza kwamba kwa upande wa Timu ya Ivory Coast itawasili hapa nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo, waliopo kwenye picha kutoka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu
Naye Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Rodger Tenga amesema tayari wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini, na amezitaja nchini hizo kuwa ni Ujerumani, Italia,DenmarkNew Zealand, Brazil,Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment