AFRICAN STARS YATAMBULISHA WATATU KUTOKA FM ACADEMIA!!

Queenb Suzy akipiga msamba katika moja ya staili zake alizozionyesha jana wakati wakati bendi ya African Stars ilipotambulisha wanenguaji watatu iliowachukua kutoka bendi ya FM Academia kwenye viwanja vya Learders jijini Dar es salaam, bendi hiyo imeendelea kujizatiti kwa kuimarisha idara mbalimbaliza bendi ili kuboresha muziki na maonyesho yake.
Asha Sharapova akionyesha mgandisho kiuno kama unayoona kwenye picha mdau.
Mnenguaji Sabrina Pazi kutoka bendi ya FM Academia akionyesha uwezo wake kwa mashabiki.
Hawa wadau wa Muziki na wanazi wakubwa wa Yanga wakihamishia furaha yao Leaders baada ya timu yao ya Yanga kuibuka mabingwa wa Kombe la Tusker kwenye uwanja wa Uhuru jana ilipoifunga Sofapaka kutoka Kenya kwenye mchezo wa fainali, kati ni Jose Mara wa FM Academia Mac Temba kulia na rafiki yao Inocent.
Mashabiki mmbalimbali wakiangalia utambulisho wa wanenguaji wapya kutoka FM Academia waliojiunga na bendi ya African Stars jana kwenye viwanja vya Leaders.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment