MASHABIKI WA AFRICAN STARS WASUGUA KISIGINO LANDMARK!!

Wanenguaji wa Bendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao lililofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Land Mark Ubungo jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo katika kusherehekea sikukuu ya Krismass, hivi sasa bendi ya African Stars ni moja ya bendi zinazofanya vizuri sana kwenye maonyesho yake na kufanya mashabiki wengi kujitokeza katika maonyesho ya bendi hiyo ili kupata burudani, heko wana wa kutwanga na kusugua kisigino.
Mashabiki wakisugua kisigino na Twanga.
Mashabiki wakipagawishwa na wanenguaji wa bendi hiyo.
Hapa waimbaji wa Bendi hiyo wakiimba jukwaani.
Mwandishi bora wa jumla wa mwaka 2009 Jerry Murro kutoka TBC kushoto akiwa katika picha ya pamoja na mwandishi mwanadamizi wa New Habari 2006 Siddy Mgumia katikati pamoja na mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars Saleh Kupaza wakati bendi hiyo ilipofanya onyesho la sikukuu ya Krismass kwenye ukumbi wa Hoteli ya Land mark Ubungo jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Jerry Murro mtangazaji wa TBC akiwa na rafiki yake mamaa Jennifer wakifuatilia kwa karibu onyesho la bendi ya African Stars wana wa Kutwanga na Kupepeta kwenye ukumbi wa LandMark usiku wa kuamkia leo katika kusherehekea sikukuu ya Krismass.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. mamaaaaaaaaa siddy wakilisha nakuona sana wakilisha weru2 product ya mama msuya nikija lazima nikutafute tu! naona mambo yako sio mchezo

  2. hongera sana full shangwe unajitahidi kutupa vile vitu moto, hivi huyu muro tangu atemewe mate na mzungu amepata chati sana maana hamuishi kutoka katika habari kama hiyo deal ngoja nami nikirudi bongo nitafute issue

Post a Comment