EAST AFRICAN BREWERIS YATIA UBANI KOMBE LA MAREALLE

Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Marealle akiongea na waandishi wa habari kutangaza East African Breweries Foundation kama wadhamini wa mashindano ya Chifu Marealle 2009. Kulia kwake ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Ibrahim Kyaruzi.


Taasisi ya EABL Foundation chini ya kampuni ya East African Breweries ndiyo itakuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kombe la Chifu Marealle yanayotarajiwa kufanyika Mjini Moshi kuanzia tarehe 27 Desemba 2009 mpaka tarehe 2 Januari 2010.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masuala ya Jamii wa East African Breweries, Bw. Ken Kariuki amesema “Sisi EABL tumedhamiria kuboresha maisha ya watu hapa Afrika Mashariki katika njia endelevu”.
Mashindano haya pia yanatumika kutoa elimu kwa vijana kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi na kuwafundisha vijana jinsi ya kuishi maisha bora. "Tunaamini kuwa mashindano haya yataunganisha watu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuweka msingi imara wa vijana na maendeleo ya michezo na kuchangia kutoa elimu kuhusu Ukimwi”, alisema Kariuki.
Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waandaaji wa mashindano hayo Aggrey Marealle alisema zaidi ya timu 14 za soka, timu 7 za netiboli na timu 10 za pool kutoka wilaya za Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha, Hai na Vunjo zote za mkoa wa Kilimanjaro zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu. Mashindano hayo yatafanyika katika kata mbalimbali za manispaa ya Moshi kama vile Pasua, Ikulu KDC, Majengo na viwanja vya George Memorial. Fainali zitafanyika katika uwaja wa MUCCOBS siku kumi baada ya uzinduzi. Timu za soka zitakazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Majengo, Bondeni, Lambo FC, Mawenzi , Kiboriloni, Korongoni, Longuo, Miembeni, Rau, Karanga, Kiyungi, Msaranga, Mji Mpya, Pasua, Soweto, Forest, Njoro, Kilimanjaro, Pasua B, Kaloleni, Langasani na Bafana Bafana

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment