VODACOM YADHAMINI KOMBE LA MAPINDUZI!!

Naibu Waziri kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo Ali Juma Shamhuna (kushoto)akikabidhi vifaa vya michezo kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu wa timu ya Simba Mohamed Kajole mara baada ya kukabidhiwa na Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa kombe la Mapinduzi (katikati)Maneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Atilio Lupala.


Kampuni ya simu za mikononi Vodacom Tanzania imedhamini mashindano ya soka ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka huu kwa zaidi ya Shilingi milioni 68.
Meneja udhamini wa Vodacom Tanzania, Emillian Rwejuna alisema kuwa udhamini huo ni wa vifaa vya michezo na fedha taslim.
Akiongea wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo na kusaini mkataba mpya wa kombe la mapinduzi kwa ZFA na kukabidhi vifaa hivyo kwa Waziri kiongozi Habari na Michezo Juma Ali Shamhuna tayari kwa ligi hiyo kuanza rasmi, alisema kuwa vifaa hivyo ni imara na vya kisasa ambavyo vinafaa katika hali ya kimchezo hapa nchini na kimataifa pia. Alisema lengo la udhamini huo ni kutaka kuendeleza michezo hapa nchini na kuweza kupata wawakilishi wazuri watakaopeperusha vyema bendera ya nchi yetu katika jukwaa la kimataifa.
Rwejuna alisema mashindano haya hujumuisha timu kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani na kushindana kama ligi zikiwa katika kundi moja, alizitaja timu hizo kuwa Simba,Yanga,Mtibwa zikitokea Tanzania bara,na Tanzania Visiwani ni Malindi,Miembeni,Mafunzo na Ocean View.
“Nae Waziri kiongozi Juma Ali Shamhuna ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kuwa kampuni inayojishughulisha na maendeleo ya Michezo hapa nchini na kuwapa changamoto makampuni mengine yaweze kujitokeza ili kuendeleza sekta hii ya michezo.
Shamhuna alisema mashindano haya yamekuwa yakifanyika kila mwaka mwezi wa kwanza kama sehemu ya kuadhimisha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kutukumbusha mazuri yaliyotokea kwa kujitawala wenyewe mnamo januari 12 1964.
Aliongeza kuwa kwa kawaida mashindano haya huanza mwezi wa kwanza na kufikia tamati tarehe 12 siku ambayo ndiyo kilele cha sherehe za Mapinduzi ambako zitafanyika Gombani Pemba.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment