KAPUMZIKEA MAHALA PEMA PEPONI HAYATI MZEE RASHID MFAUME KAWAWA!!

Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa enzi za uhai wake.

Habari zilizotufikia zinasema Mzee Rashid Mfaume Kawawa Simba wa Vita amefariki dunia leo asubuhi yapata saa 3:20 asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu
Habari zilizotolewa na Daktari aliyekuwa akimtibu katika hospitali hiyo Dr. Mpoki Ulisubisya ambaye ni mkuu wa idara ya Usingizi na wagonjwa mahututi zinasema mzee Rashid Kawawa amefariki kwa ugonjwa wa kisukari na mwili wake umehamishiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya serikali na Familia kukaa kikao na kujadili kwa pamoja mambo muhimu ya kufanya kwa ajili ya msiba huu mkubwa wa kitaifa.
Mzee Kawawa ambaye alizaliwa Liwale Mkoani Lindi mwaka 1926 aliwahi kushika nyazifa nyingi Serikalini ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri mkuu mwaka 1962 mpaka mwaka 1977 na baadae katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi CCM kabla ya kustaafu

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment