RASHID MATUMLA NA JOSEPH MARWA KUTWANGANA KESHO UHURU!!

Mabondia Rashid Matumla (Snake Man) kulia na Joseph Marwa na (Smart Man) wakitunishiana misuli wakati walipokuwa wakitambiana baada ya kupima uzito kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo asubuhi mara baada ya kuongea na waandishi wa habari juu ya mpambano wao unaotarajiwa kupigwa kesho kwenye uwanja wa Uhuri jijini Dar es salaam.
Joseph marwa ana kilo 87 wakati Rashid matumla ana kilo 86 na pambano lao litakuwa la uzito wa 86 na litakuwa la Raundi 10 na Rashid Matumla ameshawahi kuchukua mataji ya IBU,WBU na WBA wakati Joseph Marwa amewahi kuchukua mataji ya PABA na UBO , kiingilio katika mapambo hayo kitakuwa kati ya 3000. 5000 na 10.000 waote mnakaribishwa ili kujionea masumbwi hayo mazito.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. hawa akina matumla njaa zitawaua.wote ni spent force wanatAFUTA NINI kwenye ring?

Post a Comment