AFANDE KOVA AWATAKA WAKAZI WA JIJI KUWA WATULIVU!!

Afande Sul;eiman Kova.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wakati huu wa sikukuu ya mkesha wa mwaka mpya 2010 unaofanyika leo kote duniani.
Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi kanda maalum ya mkoa wa Dar es salaam afande Suleiman Kova alipoongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, amesema wakazi wa jiji wasiwe na wasiwasi lakini pia wanatakiwa kuwa watulivu wakati wote wa sikukuu ya mwaka mpya huku wakisaidiana na polisi katika kubaini wahalifu.
Ameongea kuwa hali ni shwari na watu wasiwaache watoto wakizurura peke yao na pia waachane na vitendo vinavyoweza kupelekea uhalifu ikiwa ni pamoja na kulewa kupita kiasi na kufanya fujo mbalimbali mitaani kwani jeshi hilo limejipanga kikamilifu ili kupambana na uhalifu wowote utakaotokea wakati huu wa sikukuu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment