SOFAPAKA YAWABAMIZA NDUGU ZAO TUSKER 4-0!!

Timu ya Sofapaka kutoka nchini Kenya leo imeifunga timu ya Tusker pia kutoka Kenya magoli 4-0 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo.
Mchezo huo uliokutanisha ndugu wawili ulikuwa ni wa nusu fainali ya kombe la Tusker ambalo hufanyika kila mwaka hapa nchini, na kushirikisha timu za nyumbani na timu alikwa kutoka nchi jirani pia.
Ushindi huu wa timu ya Sofapaka ya Kenya unaifanya kutinga katika fainali za michuano hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa Jumapili mwishoni mwa wiki hii katika uwanja mkuu wa Taifa.
Timu hiyo hivi sasa inasubiri mshindi kati ya watani wa jadi kutoka hapa nchini Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa katika uwanja Mkuu wa Taifa kesho kuanzia saa moja jioni, hivyo timu yoyote itakayoshinda kesho kati ya Yanga na Simba ndiyo itakayocheza fainali na timu ya Sofapaka, na timu itakayofungwa kesho itakutana na Tusker kutafuta mshindi wa tatu mchezo utakaopigwa Jumamosi
Timu za Mafunzo ya Zanzibar na Mtibwa Sugar waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo tayari zimeshaaga michuano hiyo baada ya kutolewa katika hatua za awali

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment