MWILI WA HAYATI MZEE RASHID KAWAWA SIMBA WA VITA KUAGWA KESHO KARIMJEE!!

Hayati Mzee Rashid Kawawa.
Mwili wa Hayati Mzee Rashid Mfaume Kwawa unatarajiwa kuagwa kwenye ukumbi wa Karimjee kesho ambapo viongozi na wananchi mbalimbali watapata nafasi ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa keshokutwa Jumamosi nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaaam.
Akizungumzana wandishi wa habari jioni hii Naibu Katibu mkuu kiongozi wa Ikulu Mh George Yambesi amesema viongozi pamoja na watu mbalimbali ndugu na Jamaa wataanza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia saa nane mchana kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake Madale hiyo Jumamosi
Mwili wa hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo, hayati Mzee Rashid Kawawa amefariki leo asubuhi kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment