Swissport yakabidhi jengo jipya Makao ya Taifa ya watoto Yatima Kurasini

Meneja Mafunzo wa Kampuni ya Swissport Tanzania Ltd, Nyasso Gama (kulia), akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi jengo kwa Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Kurasini Kulelea Watoto Yatima, Margareth Mkandawile (aliyeshika utape) katika hafla iliyofanyika katika Makao hayo, Dar es Salaam jana. Jengo hilo lililojengwa kwa gharama ya sh. milioni 48 zilizochangwa na wafanyakazi wa Swissoprt, lina vyumba viwili vya madarasa, Ofisi ya walimu na vyoo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Meneja Mafunzo wa Kampuni ya Swissport Tanzania Ltd, Nyasso Gama (kulia), akikata utepe akimkabidhi Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Kurasini ya Kulelea Watoto Yatima, Margareth Mkandawile msaada wa mbuzi na vyakula mbalimbali vyenye thamani ya sh. 720,000 katika hafla iliyofanyika sambamba na kukabidhi Jengo lililojengwa kwa gharama ya sh. milioni 48 zilizochangwa na wafanyakazi wa Swissoprt. Hafla hiyo ilifanyika katika makao hayo, Dar es Salaam juzi.

Jengo lenyewe hili

Watoto Yatima wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Kurasini, Dar es Salaam, wakiimba wimbo wa kuisifia Kampuni ya Swissport Tanzania Ltd, kwa kukabidhi jengo lililojengwa kwa gharama ya sh. milioni 48 zilizochangwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo. Hafla ya kukabidhi jengo hilo ilifanyika katika Makao hao jana.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment