Kocha wa Bolton atimuliwa

Aliyekuwa kocha wa Bolton Gary Megson.

Kocha wa timu ya Bolton Gary Megson amefukuzwa kazi.
Megson alizomewa na mashabiki siku ya Jumanne baada ya timu yake kutoka sare ya 2-2 na Hull.
Megson amedai kuwa tabia kama hiyo ya kuzomewa inaathiri timu hiyo.
Meneja msaidizi Chris Evans na kocha wa kikosi cha kwanza Steve Wigley ndio watasimamia timu hiyo iliyo katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Megson anakuwa kocha wa tatu wa ligi kuu ya England kufukuzwa kazi msimu huu, ikiwa ni siku chache baada ya Mark Hughes wa Manchester City kufukuzwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment