TANZANIA TUMRUDIE MUNGU!! (MTUME APOSTLE MATAMBO).

Mtume Apostle Matambo akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo akisema ametumwa na mungu kuja kuwaambia Watanzania watubu dhambi zao na kumrudia mungu ili wasamehewe, akinukuu baadhi ya vifungu katika Biblia takatifu amesema Mungu anatuagiza watu wote tutubu (mdo. 17:30)bila kuangalia dini wala dhehebu la watu (Yona.3:4-10) mfalme ilibidi atangaze toba kwa nchi nzima(lk.13:3 tusipotubu tutaangamia (mdo.3:19)mungu anasema nirudieni mimi (Yoel.2:12-13) mwisho mungu atatusamehe dhambi zetu zote (Isaya.55:7). akamalizia mtume huyo, kulia ni afisa habari wa Iadara ya habari maelezo Bw.Tiganya
Waandishi hawa wakionekana wanyenyekevu wakati wa maombi waliyoombewa na mtume Apostle Matambo ili waweze kufanya kazi zao kwa haki na waongezewe vipato vyao na waajiri wao.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiombewa katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo wakati mtume Apostle Abraham Matambo wa kanisa la Holy City Tample Ministry alipoongea na wasandishi wa habari na kusema kwamba ameletewa ujumbe na mwenyezi mungu juu ya watanzania kutakiwa kumrudia mungu na kuomba Toba ili wasamehewe dhambi zao.

SALAAM ZA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MWANABLOG MWENZETU WA CHANGAMOTO YETU BLOG

Heri ya mwaka mpya toka CHANGAMOTO YETU BLOG
Amani Heshima na Upendo kwako ndugu. Natumai kuwa u-mwema na unamalizia mwaka vema. Basi napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa mchango wako wa namna moja ama nyingine katika nyanja hii ya blog. Uwepo wako ni muhimu sana na kwa hakika tunajifunza mengi. Natumani (pamoja na wana-changamoto wote) kuwa mwaka ujao utakuwa mwema zaidi na tutaendelea vema katika ile nia ya KUIELIMISHA, KUIBURUDISHA NA KUIKOMBOA JAMII YETU kwa kadri ya uwezo wetu.
Heri ya mwaka mpya wa 2009 toka CHANGAMOTO YETU BLOG.

JESHI LA POLISI LAPOKEA MSAADA WA PIKIPIKI NA GARI!!

IGP Said Mwema akitoa shukurani zake kwa makampuni yaliyotoa msaada wa pikipiki 16 na gari moja aina ya Landrover vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 129 ili kusaidia jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu hapa nchini makabidhiano yamefanyika katika makao makuu ya wizara hiyo jijini leo picha zote na (Mwanakombo Jumaa wa Maelezo).
Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya CMC Automobale Ltd Bw.Abdull Haji akikabidhi funguo za gari aina ya Randrover lenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi Bw. Patrick Rutabanzibwa ili kusaidia juhudi za jeshi la polisi nchini katika kupambana na uhalifu katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Abas Kandoro na kulia ni mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema makabidhiano yamefanyika katika makao makuu ya wizara hiyo jijini leo.


Katibu mkuu Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi Patrick Rutabanzibwa katikati akikata utepe kuzindua Pikipiki 11 zenye thamani ya shilingi milioni 54 zilizotolewa na Baraza la Usalama Barabarani na kukabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Mh. Abas kandoro kushoto ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza hilo leo jijini kulia ni mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema.

Zain Yatangaza mshindi wa milioni moja kutoka Karatu!!


Mfanyakazi wa Zain Tanzania, Ramadhan Hassan akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kumpata mshindi wa sh. milioni 1 wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Aloyce Yambi wa Karatu, Dar es Salaam jana (Desemba 29, 2008). Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju, Meneja Masoko (Kitengo cha Wateja) wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa na kulia ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Kahatu.

kampeni ya JK ya upimaji wa ukimwi kwa hiari yafanikiwa kutoka watu milioni 2 hadi 6.8

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akiongea katika moja ya mikutano aliyowahi kuzungumza na wadau mbalimbali wa Afya.

NA ZAWADI MSALLA NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

IMEELEZWA kuwa ya idadi ya watu wanaopima virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwa hiari baada ya kuzinduliwa Kampeni ya Kitaifa ya Upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari, imeongezeka kwa kiasi kikubwa, kutoka watu milioni 2,000,000 kipindi cha mwaka 2005 hadi kufikia watu milioni 6,836,450 mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa wakati alipokuwaakiwasilisha taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya nne katika kipindi cha miaka mitatu na kuzungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
“Ongezeko kubwa la waliopima kwa hiari virusi vya UKIMWI limetokana na Kampeni ya Kitaifa iliyozinduliwa na kuongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete Julai 14, mwaka 2007,” alisema Profesa Mwakyusa.
Profesa Mwakyusa aliongeza kuwa katika kipindi cha Disemba 2005 hadi Disemba 2008, kumekuwa na ongezeko la huduma katika maeneo mbalimbali za kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Alisema idadi ya vituo vya upimaji wa Ukimwi kwa hiari vimeongezeka kutoka vituo 515 mwaka 2005 na kufikia vituo 1,643 mwaka huu.
Aliongeza kuwa idadi ya wagonjwa wapatiwa dawa za kurefusha maisha(ARVs) imepanda kutoka wagonjwa 23,951mwaka 2005 hadi wagonjwa 189,050 sambamba na kuonzeka kwa idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya tiba na matunzo ambayo ilikuwa ni vituo 96 na kufikia vituo 400 katika kipindi hicho.
Alisema kutokana na mapambana hayo viwango vya maambukizi ya virusi vya ukimwi hapa nchini vimeshuka kutoka wastani wa asilimia 7 mwaka 2005 kufikia asilimia 4.8 mwaka 2008, kufuatia kampeni ya hiyo.
Waziri Mwakyusa alisema asilimia 34 ya wanawake wote wajawazito wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi walipata dawa za kuzuia maambukizi hayo yasiende kwa watoto wao na kuongeza kwamba idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto vimeongezeka kufikia vituo 2,474 ukilinganisha na ile ya awali ya vituo 544 wakati wa kipindi hicho.
“Wizara imeandaa Mpango Mkakati mpya wa Kisekta wa Kudhibiti Ukimwi kwa kipindi cha miaka mitano 2008-2012. Mpango huo unalenga kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu za kudhibiti na kutibu Ukimwi nchini,” alisisitiza.
Wakati huohuo Waziri Mwakyusa alizungumzia kuhusu Huduma za Maabara na Ufundi wa Vifaa Tiba, ambapo alisema, maabara zote za Rufaa na Mikoa zimepewa mashine za kuchunguza damu na uwezo wa figo na ini pamoja na chembe chembe za kinga – CD4 kwa ajili ya uanzishwaji na ufuatiliaji wa matibabu ya wagonjwa wa Ukimwi.
Pia maabara zote za wilaya zimepewa mashine za kuchunguza damu na uwezo wa figo na ini kwa ajili ya ufuatiliaji wa matibabu ya wagonjwa wa Ukimwi na maabara zote za Kanda zimepewa mashine maalum (DNA PCR) kwa ajili ya kuchunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) kwa watoto wachanga chini ya miezi 18.
“Utaratibu wa kitaifa wa upimaji wa haraka wa VVU (National HIV rapid testing algorithm umebadilishwa kutoka utaratibu wa ‘Capillus’ iliyohitaji kutunzwa kwenye ubaridi na kutumia utaratibu wa ‘SD Bioline usiyohitaji kutunzwa kwenye ubaridi,” alisema.

Kwa upande lishe na Ukimwi alisema watoa huduma majumbani 111 katika wilaya 37 za mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Mbeya, Rukwa na Iringa wamepata mafunzo kuhusu lishe kwa wagonjwa wenye Ukimwi na nakala 17,000 za mwongozo wa kitaifa kuhusu lishe bora kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wenye Ukimwi, zimechapishwa na kusambazwa kwenye hospitali, Vyuo vya Afya na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya ugonjwa huoI.
Alisema utafiti wa chakula kinachofaa kuongeza virutubishi vya vitamini na madini kwa ajili ya watu wanaoishi na virusi vya hivyo na wenye ugonjwa huo umefanyika ambapo tafiti hii imeonyesha chakula hiki ambacho kinatokana na mazao yanayopatikana hapa nchini yameonyesha uwezo wa kuboresha afya ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wenye Ukimwi .

Mwakyusa alisema chakula hicho kinatokana na mchanganyiko wa unga wa mahindi, soya pamoja na virutubishi vya madini na vitamini ambavyo vyote vinapatikana nchini,hivyo matokeo ya awali yameonyesha kuwa afya ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wenye Ukimwi waliotumia chakula cha namna hiyo imeimarika.

Mh. Adam Malima aongea na waandishi wa habari kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta!!


Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Adam Malima akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta na kupanda kwa bei nchini leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Waumini wa kkkt usharika wa mtongani watoa msaada katika hospitali ya temeke

Hidaya Utawangu ambaye ni Afisa Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Temeke akivihesabu vyandarua 100 walivyopewa na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mtoni Mtongani baada ya kuwapatia vyandarua 100 kwa ajili ya kutumika katika wodi za hospitali hiyo .

Na Anna Nkinda
29/12/2008 Dar es Salaam Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Mtoni Mtongani wamewaomba wananchi wenye uwezo kuwakumbuka wagonjwa na watu wasiojiweza kwa kuwapa misaada mbalimbali ambayo itawafariji na kuwasaidia katika maisha yao.
Waumini hao waliyasema hayo hivi karibuni walipowatembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea sikukuu ya Christimas.
“Kanisa letu linatoa huduma mbalimbali za kijamii hivyo basi huduma hii tunayoitoa leo ni mojawapo ya huduma tunazozitoa ila huwa tunawahudumia wagonjwa waliopo majumbani lakini leo kwa mara ya kwanza tumeweza kuwahudumia na wagonjwa waliolazwa Hospitalini”, walisema waumini hao kwa furaha.
Mchungaji wa Kanisa hilo Leah Mwankenja ambaye alikuwa ni Kiongozi wa msafara huo alisema kuwa ni agizo la Bwana Yesu wanahuduma na kuwafariji wagonjwa hivyo basi nao wameona kwa kipindi hiki cha sikukuu watimize agizo hilo.

Mchungaji huyo aliendelea kusema kuwa huduma hiyo itakuwa endelevu na kuwataka watu wenye uwezo na afya njema watumie baraka za Mungu kuwajali wahitaji.

Naye Hidaya Utawangu Afisa Muuguzi wa hospitali hiyo ambaye pia siku ya tukio alikuwa ni msimamizi wa zamu aliwashukuru waumini hao kwa msaada walioutoa kwani katika mkoa wa Dar es Salaam hospitali ni nyingi hivyo basi kwa kuwafikiria wao ni upendo wa kipekee.

Afisa huyo alisema kuwa vyandarua walivyopewa vitasaidia sana ingawa ni vichache kutokana na mahitaji ya hospitali kwani vitanda ni zaidi ya vyandarua walivyopewa hivyo aliziomba Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali , watu binafsi na mashirika ya umma wawapatie msaada pindi watakapopata nafasi.

Alimalizia kwa kusema kuwa taratibu za kwenda kuwatembelea wagonjwa na kutoa msaada hospitalini hapo ni kuandika barua ya maombi utawala ukishakubaliwa unapangiwa siku nzuri yenye nafasi.

Aidha wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo waliwashukuru waumini hao kwa kitendo cha kuacha kufanya starehe kama wafanyavyo wengine na kwenda kusherehekea sikukuu pamoja nao .
“Tumepata faraja kubwa sana kwani kwa kawaida anapokuja kukuona mtu ambaye hamfahamu na kukupa pole unafarijika kwa kuwa ni kitu ambacho hukukitegemea”, walisema wagonjwa hao.
Waumini hao walitoa vyandarua 100 ambavyo vitatumika mawodini, sabuni za kufulia na kuogea, biskuti, pipi, juice ambazo waliwakabidhi wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi za wazazi, wanawake, watoto na wanaume.

WAISLAMU WAANDAMANA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA!!

hapa wakionekana watoto kwa wakubwa katika maandamano hayo yaliyofanyika leo jijini.

Waumini mbalimbali wa Dini ya kiislamu wakiandamana katika barabara ya Bagamoyo maeneo ya Salender Bridge kuelekea barabara ya umoja wamatifa katika kuukaribisha mwaka mpya wakiislamu leo jijini.

EMMANUEL NA HAPPNESS WAMEREMETA!!

Emmanuel na Mke wake Happness wakimeremeta katika sherehe yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ngorongoro Hall uliopo kwenye viwanja vya maonyesho vya mwalimu Julius K. Nyerere barabara ya Kirwa mara baada kufunga pingu za maisha kwenye kanisa la KKKT Usharika wa Temeke Wailesi jumamosi iliyopita jijini.
Ngoja tucheze kidogo muziki jamani!!

Pozi la kuanza maisha mapya katika ndoa kama wanavyoonekana Emnanuel na mke wake Happness.

Wakati wa kupata mapoichopocho.

Dada Zake na Immanuel katika picha ya Pamoja kulia ni Jaqulin kati Annet Mdamu na Rafiki yao.

Hapa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzie.

Hapa afanya kazi wenzie na Emmanuel kutoka kampuni ya mafuta MOGAS wakimpongeza katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ngorongoro Hall ulioko kwenye viwanja vya maonyesho vya mwalimu Julius K. Nyerere Barabara ya Kirwa.

BAADA YA MIAKA KUMI HARDBLASTERS KURUDI KWA KISHINDO!!

Prof J aka Mr. Red Carpert kulia akiwa na mzee wa FULLSHANGWE mara baada ya mazunguzo yao.


Prof J. aka Mr. Red Carpet katikati na Dj Choka kulia, kushoto ni msanii mwenzie wa Hardblasters Willy wakipozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.

Kundi la muziki wa kizazi kipya bongofleva lililojulikana kama Hrdblasters na lililotamba na Albam yake ya Funga Kazi 2000 likijumuisha wasanii watatu ambao ni joseph Haule Pro. J. Fanani na Willy katika miaka ya 1999 na 2000 sasa linarudi tena kwenye gemu baada ya ukimya wa Takriban miaka kumi hivi.
wakizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE kwenye ufukwe wa Coco Beach wasanii wa kundi hilo Prof. J. na Willy walisema kuanzia mwaka ujao wa 2009 wanayo project ya kurekodi Albam ambayo itakuwa ni tishio katika muziki wa kizazi kipya, albam hii inaweza kushangaza watu kwani vile vichwa vitatu yaani Joseph Haule aka (Prof.J.) Terry aka (Fanani) NaWilly ambavyo ndiyo vilivyoandika mistari na vina katika wimbo wa Chemsha Bongo uliokuwa katika Albam yetu ya Funga Kazi 2000 vinarudi tena kufanya kazi pamoja kama Hardblasters yaani usipime mtu wangu.
Kama unavyojua kwamba wimbo wa Chemsha bongo kutoka Hardblasters kwa wakati ule ndiyo ulichangia kwa kiasi kikubwa sana kuwashawishi wazazi kuwaruhusu watoto wao kuanza kuimba muziki huu, kwani kwa kipindi hicho ulikuwa ukionekana kama muziki wa wahuni.
Prof J. au Mr. Red Carpert anasema kwakweli wamejiweka sawa Terry yuko fiti kabisa willy alikuwa amebanwa na majukumu mengi ya kifamilia na mimi programu yangu inaniruhusu kwakuwa niko kwenye gemu kwa muda wote wa maisha yangu hivyo mkakati wetu uko makini na tumeshaanza kuandika nyimbo za kutosha kwa ajili ya Albam hiyo.
Utengezaji wa Albam hiyo utakuwa chini ya Maproducer ambao ni Producer Q. , Rudigo na Dj Choka ambaye niko naye katika ziara zangu nyingi ninazofanya Ulaya, Marekani na Afrika kwa ujumla na ameonyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mashine kwenye maonyesho yangu.
Naye masanii wa kundi hilo Willy amesema yuko tayari kabisa kwa sasa na pia akasema mwenzao Fanani naye yuko sawa kwa kazi ya kuirudisha tena Hardblasters ya miaka kumi iliyopita na amesema ana imani kuwa hardblasters ya sasa itakuwa ya kisasa zaidi na itapiga hatua zaidi kwa kuwa wanaye mwenzao Prf. J. ambaye yeye tayari anajua muziki huu kwa sasa uko kwenye kiwango gani kimataifa kwani tayari ameshashiriki kwenye maonyesho mengi ya kimataifa na kufanya vizuri.
Mbali ya kutamba na wimbo wa Chemsha Bongo Hardblasters pia ilitamba na nyimbo kama mamsap, niamini nataka niwe na wewe, chuzi limekubali na nyingine nyingi zilizochengua vijana wanaoupenda zaidi muziki huo.

SIKINDE WAFURAHIA SIKUKUU YA X-MASS!!


Kutoka kulia ni waimbaji wa bendi ya DDC Mlimani Park Abdalla Hemba,Bitchuka, Shaban Dede,Edo SangaHassan Kunyatana Karama Regesu.


Bendi ya muziki wa dansi ya hapa jijini DDC Mlimani Park maarufu kama Sikinde Ngoma ya Ukae imefurahia sikukuu ya krismasi kutokana na mashabiki wake walivyoipokea katika maonyesho yake wakati wa sikukuu hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 25/12.

Akizungumza na FULLSHANGWE ambayo ilitaka kujua mambo yaliyojiri katika sikukuu ya mwaka huu kutoka bendi hiyo kongwe nchini, kiongozi wa bendi ambaye pia ni mwanamuziki mkongwe hapa nchini Shaban Dede amesema wapenzi wa bandi yao walijitokeza kwa wingi na wamefurahia programu yao waliyowaletea katika sikukuu hiyo kubwa duniani.

Bw. Dede ameongeza kuwa wao kama sikinde wanajua kiu ya mashabiki wao na nini wanapenda hivyo waliamua kuwaletea nyimbo zilizopo kwenye Albam yo mpya ya (Supu umetia nazi) ambayo ina nyimbo sita kama Supu umetia nazi yenyewe,fitina mapenzi,Heshima,Upendo, jumamanga Tunduni na King Fish nyimbo ambazo ama kwa hakika washabiki wetu wanazipenda na wanazifurahia mara tunapozipiga katika kumbi mbalimbali za burudani hapa jijini na mikoa mbalimbali.

Ameongeza kuwa katika Programu yao ya sikukuu ya Krismasi pia waliongeza nyimbo mpya mbili ambazo ni (Tunu ya Upendo kuenziana) na (Ukubwa si umbo), nyimbo hizi hazipo kwenye Albam yetu hii mpya lakini tumekuwa tukizipiga sana katika maonyesho yetu ya hivi karibuni na tayari zimeanza kujizolea umaarufu mkubwa kwa mashabiki wetu hapa jijini Dar na kwingineko karibu nchi nzima.

FULLSHANGWE INAWATAKIENI X-MASS NJEMA NA HERI YA MWAKA MPYA 2009!!

Nawatakieni sikukuu jema ya X-Mass na mwaka mpya nina imani picha hii ya mwanapunda itawakumbusha matendo makuu mengi yaliyotokea wakati ule mwana wa mungu Yesu kristo alipozaliwa kule Yerusalem, na kwa kupitia picha hii wengi wanaweza kumrudia mungu na kuachana na matendo maovu yamchukizayo mungu wetu mwema.

Sauti za Busara Festival Artists 2009!!

The Moreira Project
style
jazz
festivals
Sauti za Busara 2009
website
recordings
THE MOREIRA PROJECT - Volume 1; The Journey (2005)
31 year old Moreira Chonguica is a celebrated Cape Town based musician, originally from Mozambique.
Moreira located to Cape Town to further his music studies where he graduated from the University of Cape Town's South African College of Music with a degree in jazz performance and an honors degree in Ethnomusicology (cum laude) in 2000. Since his move to Cape Town, Moreira has established an impressive list of credits to his name.
Moreira's debut album, THE MOREIRA PROJECT Volume 1 - the Journey was released in December 2005 and has been received with overwhelming response from the industry as well as the media on both local and international levels. The album expresses not only his phenomenal song writing ability and energetic performances but also his major personal coup of securing the support and talent of international jazz legend - NAJEE on several tracks.
Working with such an accomplished musician is a dream come true for Moreira. States an elated Moreira, "Najee and I first met at the B.E.T Festival in Durban a few years ago. Then a year later we both performed at the Joy of Jazz Festival. We spoke at length and he promised to send me a better saxophone. True to his word, he actually did! It arrived on 13 December 2003 - I will never forget the date or the gesture. This is someone I grew up listening to, along with the likes of Grover Washington Jr and others. And now here I am Mozambican born and bred, buttered in Cape Town”‘with this legend coming halfway around the planet to perform on my album. It's just unbelievable"
The album specializes in contemporary African fusion jazz and was recorded by Moreira's own independent recording label, More Star Entertainment (Pty) Ltd. Produced by Mark Fransman and Moreira, the album has created a new awakening in jazz lovers as well as capturing a niche for the 'fresh ear'.
Not only is Moreira a consummate performer, but he is also strongly involved in the promotion of education. When the album was launched in his home town of Maputo, he donated R10 000 to start a campaign to renovate the Escola Nacional de Musical (National School of Music) the school which he attended as a youth. Whenever he goes back to Maputo, he makes sure to spend some time at the school conducting workshops. In Cape Town Moreira is involved with a community school in Kensington called Xulon Musictech run by Camillo Lombard and Ezra Delport. Here he teaches saxophone and life skills to young aspiring musicians on a regular basis. In additional, he tutors young aspiring saxophonists free of charge on an ad hoc basis.
In 2000 Moreira was chosen by City of Chicago to be part of the Cultural Exchange programme co-ordinated by Ernest Dawkins alongside other South African musicians


ZAIN YAANGUSHA PATY YA NGUVU KUUAGA MWAKA 2008 NA KUMKABIDHI CHETI MFANYAKAZI BORA!!


Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania Khalid Muhtadi baada ya kuibuka mfanyakazi bora wa kitengo cha uhusiano wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuuaga mwaka 2008, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wiki hii.


Wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Zain Tanzania, wakishangilia huku wakiinua juu kombe baada ya kuibuka washindi wa kudansi wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii.

Mameneja Masoko wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto) na Costantine Magavilla wakitumbuiza kwa kuimba wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii



Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya (kulia) na Dangio Kaniki wakiwaongoza wenzao wa idara ya utawala na uhusiano wa umma kucheza wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii.


Meneja Kumbukumbu wa Zain Tanzania, Hilda Nakajumo (mbele) akiwaongoza wenzake kucheza dansi wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Zain kuaga mwaka 2008, Dar es Salaam wiki hii.


USAFIRI WA AZAM FC CLUB, WAKO JUU HAWA!!


Azam Fc Club wanasema wameipania ligi kuu mzunguko wa pili itakayoanza januari mwaka ujao lakini si hivyo tu pia wamejizatiti kwa mambo mengi hebu ucheki usafiri wao ulivyo mkali ni hili ni basi dogo kuna lingine kubwa zaidi ya hili jamani mpira ni pesa na mipango sio maneno tu.

WANAMUZIKI WA B. BAND NA POZI ZAO!!

Banana Zoro kijana matata sana katika muziki wa bongo fleva na ambaye amejijengea heshima kubwa kwa kumiliki bendi yake mwenyewe hiyo ni hatua kubwa jamani naye pia ana pozi zake anapokuwa anaimba jukwaani hebu icheki hii unaionaje mdau.
Ismail wa Bendi ya B. Band inayomilikiwa na Banana Zoro yeye anapenda kupozi hivi kwenye picha unaionaje hiyo mdau wa shangwe.


MSHINDI WA MARCEDES BENZ YA GLOBAL PUBLISHERS APATIKANA!!

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera akisoma jina la mshindi wa bahati nasibu iliyoendesha na kampuni ya Globar Publishers ianyochapisha magazeti ya ijumaa, Champion, Amani na Risasi kulia kwake ni meneja mkuu wa kampuni hiyo Abdalla Mrisho.
Gari aina ya Marcedes Benz ambayo tayari imenyakuliwa na mshindi kutoka Dar es alaam Bw. Komanya Hosea.

Naibu Waziri wa habari, Utamaduni na michezo Mh. Joel Bendera akichagua na kusoma kuponi ya mshindi wa Mercedes benzi katika droo iliyofanyika viwanja vya biafra Kinondoni Jumatatu iliyopita. Droo iliendeshwa na Global publishers kupitia magazeti yake ya Uwazi, Ijumaa,Championi, Risasi na amani. Mkazi wa gerezani Dar es salaam, KomanyaHoseah aliibuka mshindi.


Ujenzi wa mradi wa umeme wa Somanga Fungu- Lindi Waendelea!!


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. Adamu Malima akipata maelezo kuhusu maendeleo ya mradi wa Umeme wa Somanga Fungu kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wa mradi huo Bw.Edwin Nyakarashi alipotembelea eneo la mradi huo Kilwa kusini. (picha na Aron Msigwa)

CHAMA CHA MPIRA WA NETIBOLI NCHINI CHAOMBA UDHAMINI NA MISAADA KWA WADAU WA MICHEZO!!

Mwenyekiti wa chama cha Netiboli nchini Anna Bayi kushoto akiongea mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo, kuzungumzia mikakati ya chama hicho katika kuendeleza mchezo huo nchini, katikati ni Shyrose Bhanji makamu mwenyekiti na mwisho ni Rose Mkisi katibu msaidizi.

MAELEZO YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA NETIBOLI NCHINI – CHANETA- ANNA BAYI KATIKA KIKAO CHA UONGOZI MPYA WA CHANETA NA WAANDISHI WA HABARI – UKUMBI WA MAELEZO- DSM 23/12/2008.
Awali ya yote nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati kwa kuitikia wito wetu wa kukuta leo hii na uongozi mpya wa CHANETA ambao uliingia madarakani tarehe 6/12/2008. ASANTENI SANA.
Tumeona ni vema kupitia kwenu tuweze kujitambulisha rasmi sisi viongozi tuliochaguliwa na vile vile kuelezea mikakati ya muda mrefu na muda mfupi na mipango ambayo tunadhani itasaidia mchezo huu wa netiboli kupiga hatua. ( UTAMBULISHO)
Kwanza kabisa lazima tukiri kwamba CHANETA ina mikakati mingi na mizuri, lakini kikubwa ambacho tunahitaji ni misaada pamoja na udhamini toka kwa wadau mbalimbali ili kuangalia jinsi ganI tutasaidiana kuziba pengo la ukata ndani ya CHANETA.
Tunawaomba wadau wa mchezo huu, wale wasio wadau, wapenzi wa mchezo huu na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa hali na mali kusaidia chochote walichonacho kwa ajili ya kuuendeleza mchezo huu. Tutashukuru sana iwapo kila mtanzania kwa nafasi yake atauunga MKONO juhudi zetu CHANETA, ili wote kwa pamoja tusaidiane kuuendeleza mchezo huu.
Vile vile ni Imani yetu kwamba wadhamini mbalimbali, iwe ni makampuni binafasi au mashirika mbalimbali yataitikia wito wetu ili wajitokeze kwa ajili ya kudhamini mashindano mbalimbali ambayo yapo kwenye kalenda yetu ya mwaka kesho. Sisi pia tunawaahidi kwamba kampuni yoyote itayojitokeza kudhamini michezo yetu, timu zetu zitapata ari na moyo kama vile ilivyokuwa katika timu ya taifa ya soka- Taifa Stars.
Tunaomba viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi ya Serikali ya Mitaa, Wilaya, Mikoa na Taifa nao waunge mkono juhudi zetu na watusaidie kwa hali na mali na vile vile kuamsha ari ya mchezo huu ili uweze kupendwa na wadau mbalimbali.
Moja ya changamoto kubwa iliyoko mbele yetu ni kutafuta pesa kwa ajili ya mashindano mbalimbali yakiwemo ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka kesho huko mkoa wa Pwani. Mengine ni ligi daraja la kwanza ambayo yatashirikisha club 18, na ligi daraja la pili Taifa inayoshirikisha klabu bingwa za nchi zote. Vile vile kutakuwa na ligi za wilaya na mikoa.
Mwezi February, 2009 pia tunatarajia kuzindua rasmi kambi ya maandalizi ya mashindano ya timu ya Vijana U-21 yanayotarajiwa kufanyika Windhoek, Namibia mwezi March na Aprili 2009. Mashindano haya yanafanyika mara ya kwanza ili kuwaandaa vijana kwa ajili ya mashindano makubwa zaidi ya kimataifa. Mashindano haya yatashirikisha nchi zote za AFRICA ambao ni wanachama wa CANA) Conferederation of African Netball Associations. Tanzania ni mwanachama hai wa CANA.
Gharama zinazohitajika ni usafiri wa kuipeleka timu ya netiboli nchini Namibia kwenye mashindano haya, pamoja na gharama za vifaa na gharama zingine kwa ajili ya maandalizi ya kambi.
Kwa kumalizia ni Imani yetu vyombo vya habari vitatusaidia kuwahabarisha watanzania kuhusu maombi yetu ya kuomba misaada ya hali na mali na udhamini wa mashindano mbalimbali kwa lengo ya kuendeleza mchezo huu.

FARII IPUPA ANASWA NA VIMWANA WA BONGO, AWA MPOLE KAMA KONDOO!!

Hapa Farii Ipupa akiwa jukwaani akikonga nyoyo za mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho lake lakini akaishia mikononi mwa vimwana wa bongo pata matukio katika picha mbalimbali akiwa na vimwana hao


Hapa Joan kulia na Mboni wakiwa katika Picha ya Pamoja kwenye onyesho la mwanamuzik Farii Ipupa pale New Word Cinema Mwenge jijini juzi mwanamuziki huyo alifanya mambo makubwa katika onyesho hilo.

Joan na Farii Ipupa wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja kwenye hoteli ya Movenpick.


Farii Ipupa akiwa katikati ya vimwana Joan kushoto na Mboni Hoteli ya Movenpick ambako mwanamuziki huyo alikofikia.

Kunduchi Beach Wet an' Wild ni raha tu Weekend, nao Tanzanite wachizisha!!

Mwanamuziki John Mhina wa Tanzanite Band akiongoza wanamuziki wenzie katika kutoa burudani kwa watu mbalimbali walioenda katika ufukwe wa Kunduchi Beach Wet an' Wild ili kujipumzisha na familia zao mwishoni mwa wiki.
Watu wakiselebuka na muziki wa Bendi ya Tanzanite inayoongozwa na mwanamuziki John Mhina huku mabomba maalum yakiwamwagia maji hii ni moja ya burudani iliyoko kwenye ufukwe huo


Watu mbalimbali wakiogelea katika mabwawa ya kuogelea kwenye ufukwe wa kunduchi Beach Wet an'wild hii imekuwa ni sehemu muhimu kwa familia na watu mbalimbali kwenda kupumzika mwishoni mwa wiki.

Zain yawasaidia SOS Children's Villages!!

Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe
akimlisha mmoja wa watoto wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha SOS
Children's Village jijini Dar es Salaam juzi (Desemba 20, 2008). Zain pia ilitoa zawadi
kwa watoto yatima hao.

Zain Caribbean Beat kumbukumbu ya Luck Dube!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyeshiriki mashindano ya
Bongo Star Search 2007/2008, Malfred Mwasote (kulia) akiimba na mmoja wa
mashabiki wakati wa tamasha la Caribbean Beat lililoandaliwa kwa ajili ya
kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha nyota wa reggae wa Afrika Kusini,
Lucky Dube, Dar es Salaam juzi usiku, na kudhaminiwa na kampuni ya simu za
mkononi ya Zain.

Lita 67 za Damu zatolewa na wafanyakazi wa Barrick Bhulyanhulu,

Wasanii wa kikundi cha Nyangaria Group Investment kutoka Mjini Mwanza wakitumbuiza wakati wa sherehe ya siku ya familia katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu iliyofanyika jana mgodini hapo.


Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu Greg Walker akitolewa damu ambayo itatumika kwa wagonjwa wakati wa sherehe ya siku ya familia iliyofanyika jana mgodini hapo. Huku Dk. Ghuhen Mtaita ambaye ni Daktari mkuu wa mgodi huo (kulia) na Adrew Marko ambaye ni afisa mhamasishaji wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya ziwa (kushoto) wakiangalia jinsi damu hiyo inavyotoka.

Na Mwandishi wetu
21/12/2008 Bhulyanhulu, Kahama.Wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu pamoja na familia zao wamejitolea lita 67 za damu wakati wa sherehe ya siku ya familia iliyofanyika jana mgodini hapo.

Dk. Ghuhen Mtaita ambaye ni Daktari mkuu wa mgodi huo alisema kuwa waliamua mwaka huu katika siku ya familia wachangie damu ili itumike kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali waliopo hospitalini.

“Lengo lilikuwa ni kupata lita 100 za damu ingawa hatujatimiza lengo ila tunaamini kuwa katika miaka ijayo tutachangia kiasi kikubwa cha damu kwani hii ni kampeni mojawapo tuliyonayo”, alisema Dr. Mtaita.

Daktari huyo aliendelea kusema kuwa kwa kuwa hii ni mara ya kwanza katika migodi ya Barrick hapa nchini kwa wafanyakazi pamoja na familia zao kujitolea damu ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea sikukuu hiyo hivyo basi wameamua kufanya zoezi hilo mara tatu au mara nne kwa mwaka.


Naye Adrew Marko ambaye ni afisa mhamasishaji wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya ziwa aliwashukuru wafanyakazi wa mgodi huo pamoja na familia zao kwa ushirikiano wao waliouonesha hasa katika kuchangia damu.

Aliendelea kusema kuwa damu waliyoipata ambayo itatumika kwa wagonjwa 201 inatosha kwani wanachotaka wao ni ubora wa damu na si wingi wa damu.

Damu hiyo ambayo itapelekwa katika kituo cha kuchangia damu salama cha kanda ya ziwa kilichopo karibu na hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza, itatumika kwa wagonjwa ambao ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, mama wajawazito ambao huhitaji damu kabla na baada ya kujifungua, ajali mbalimbali, upasuaji wa dharula na kwa wagonjwa wengine watakao hitaji damu.

Marko alisema, “Kazi yetu sisi ni kukusanya damu na kuipima kisha kuzitawanya na kuzigawa katika hospitali za mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera na Mara pamoja na hospitali za wilaya za mikoa husika, hospitali za mashirika ya dini na hospitali za watu binafsi ambazo wameruhusiwa kuongeza wagonjwa damu chini ya mpango wa Taifa wa damu salama”.


Afisa huyo mhamasishaji alimalizia kwa kuwaomba watanzania kuwa na mazoea ya kuchangia damu mara kwa mara kwani mahitaji ya damu kwa wagonjwa ni makubwa na upatikanaji wake ni mdogo.

Aidha Meneja Mkuu wa mgodi huo Greg Walker alisema kuwa lengo la siku hiyo kuwakutanisha pamoja menejimenti ya mgodi, wafanyakazi pamoja na familia zao na kukaa pamoja ili kubadilishana mawazo kwani wote wanafanya kazi kwa lengo moja na wanashangilia mafanikio pamoja.

“Siku ya leo wafanyakazi wamepata nafasi ya kukaa pamoja na kula pamoja na familia zao pia watoto wamecheza michezo mbalimbali ambayo imewajenga kimwili na kiakili pia”, alisema Walker.

Lengo lingine la kuwa na sikukuu hiyo ni kujua kwa kipindi cha mwaka mzima ni mafanmikio gani waliyoyapata pamoja na matatizo waliyokumbana nayo na changamoto gani zinawakabili katika utendaji wao wa kazi za kila siku.

Katika kusherehekea siku hiyo ambayo inafanyika kila mwisho wa mwaka
familia zilipata nafasi ya kucheza michezo mbalimbali ikiwemo michezo ya kukimbia, kukimbiza kuku, kuogelea, kucheza muziki, kuvuta kamba, mashindano ya kula matunda ya apple na kuruka.