Prof J. aka Mr. Red Carpet katikati na Dj Choka kulia, kushoto ni msanii mwenzie wa Hardblasters Willy wakipozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.
Kundi la muziki wa kizazi kipya bongofleva lililojulikana kama Hrdblasters na lililotamba na Albam yake ya Funga Kazi 2000 likijumuisha wasanii watatu ambao ni joseph Haule Pro. J. Fanani na Willy katika miaka ya 1999 na 2000 sasa linarudi tena kwenye gemu baada ya ukimya wa Takriban miaka kumi hivi.
wakizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE kwenye ufukwe wa Coco Beach wasanii wa kundi hilo Prof. J. na Willy walisema kuanzia mwaka ujao wa 2009 wanayo project ya kurekodi Albam ambayo itakuwa ni tishio katika muziki wa kizazi kipya, albam hii inaweza kushangaza watu kwani vile vichwa vitatu yaani Joseph Haule aka (Prof.J.) Terry aka (Fanani) NaWilly ambavyo ndiyo vilivyoandika mistari na vina katika wimbo wa Chemsha Bongo uliokuwa katika Albam yetu ya Funga Kazi 2000 vinarudi tena kufanya kazi pamoja kama Hardblasters yaani usipime mtu wangu.
Kama unavyojua kwamba wimbo wa Chemsha bongo kutoka Hardblasters kwa wakati ule ndiyo ulichangia kwa kiasi kikubwa sana kuwashawishi wazazi kuwaruhusu watoto wao kuanza kuimba muziki huu, kwani kwa kipindi hicho ulikuwa ukionekana kama muziki wa wahuni.
Prof J. au Mr. Red Carpert anasema kwakweli wamejiweka sawa Terry yuko fiti kabisa willy alikuwa amebanwa na majukumu mengi ya kifamilia na mimi programu yangu inaniruhusu kwakuwa niko kwenye gemu kwa muda wote wa maisha yangu hivyo mkakati wetu uko makini na tumeshaanza kuandika nyimbo za kutosha kwa ajili ya Albam hiyo.
Utengezaji wa Albam hiyo utakuwa chini ya Maproducer ambao ni Producer Q. , Rudigo na Dj Choka ambaye niko naye katika ziara zangu nyingi ninazofanya Ulaya, Marekani na Afrika kwa ujumla na ameonyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mashine kwenye maonyesho yangu.
Naye masanii wa kundi hilo Willy amesema yuko tayari kabisa kwa sasa na pia akasema mwenzao Fanani naye yuko sawa kwa kazi ya kuirudisha tena Hardblasters ya miaka kumi iliyopita na amesema ana imani kuwa hardblasters ya sasa itakuwa ya kisasa zaidi na itapiga hatua zaidi kwa kuwa wanaye mwenzao Prf. J. ambaye yeye tayari anajua muziki huu kwa sasa uko kwenye kiwango gani kimataifa kwani tayari ameshashiriki kwenye maonyesho mengi ya kimataifa na kufanya vizuri.
Mbali ya kutamba na wimbo wa Chemsha Bongo Hardblasters pia ilitamba na nyimbo kama mamsap, niamini nataka niwe na wewe, chuzi limekubali na nyingine nyingi zilizochengua vijana wanaoupenda zaidi muziki huo.
0 comments:
Post a Comment