SIKINDE WAFURAHIA SIKUKUU YA X-MASS!!


Kutoka kulia ni waimbaji wa bendi ya DDC Mlimani Park Abdalla Hemba,Bitchuka, Shaban Dede,Edo SangaHassan Kunyatana Karama Regesu.


Bendi ya muziki wa dansi ya hapa jijini DDC Mlimani Park maarufu kama Sikinde Ngoma ya Ukae imefurahia sikukuu ya krismasi kutokana na mashabiki wake walivyoipokea katika maonyesho yake wakati wa sikukuu hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 25/12.

Akizungumza na FULLSHANGWE ambayo ilitaka kujua mambo yaliyojiri katika sikukuu ya mwaka huu kutoka bendi hiyo kongwe nchini, kiongozi wa bendi ambaye pia ni mwanamuziki mkongwe hapa nchini Shaban Dede amesema wapenzi wa bandi yao walijitokeza kwa wingi na wamefurahia programu yao waliyowaletea katika sikukuu hiyo kubwa duniani.

Bw. Dede ameongeza kuwa wao kama sikinde wanajua kiu ya mashabiki wao na nini wanapenda hivyo waliamua kuwaletea nyimbo zilizopo kwenye Albam yo mpya ya (Supu umetia nazi) ambayo ina nyimbo sita kama Supu umetia nazi yenyewe,fitina mapenzi,Heshima,Upendo, jumamanga Tunduni na King Fish nyimbo ambazo ama kwa hakika washabiki wetu wanazipenda na wanazifurahia mara tunapozipiga katika kumbi mbalimbali za burudani hapa jijini na mikoa mbalimbali.

Ameongeza kuwa katika Programu yao ya sikukuu ya Krismasi pia waliongeza nyimbo mpya mbili ambazo ni (Tunu ya Upendo kuenziana) na (Ukubwa si umbo), nyimbo hizi hazipo kwenye Albam yetu hii mpya lakini tumekuwa tukizipiga sana katika maonyesho yetu ya hivi karibuni na tayari zimeanza kujizolea umaarufu mkubwa kwa mashabiki wetu hapa jijini Dar na kwingineko karibu nchi nzima.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment