Al Shabaab wafurusha wafanyikazi wa WFP, Somalia!

Moja ya picha inayoonyesha wafanyakazi wa shirika la mpango wa chakula duniani wakiwa kazini Nchini Somalia
Kundi la wapiganaji wa kislamu nchini somalia, Al-shabaab, wameamrisha shirika la Umoja wa Mataifa wa mpango wa chakula, WFP, kusimamisha shughuli zake na kuondoka nchini humo.
Kundi hilo linalodhibiti maeneo mengi ya kusini mwa nchi hiyo, limesema kuwa litachukua hatua dhidi ya raia yeyote wa Somalia anayeshirikiana na shirika hilo la WFP.
Kundi hilo limesema WFP linaangamiza wakulima nchini humo kwa kusambaza chakula cha bure nchini humo.

TRAVELTINE YARINDIMA KWA MIDUNDO YA MIAMBA YA TAARAB NCHINI!!

Malkia wa taarab Bi. Kidude Baraka akitumbuiza usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Travertine, Magomeni Mapipa, jijini Dar katika onyesho kabambe akishirikiana na Jahazi Modern Taarab, Mwanahawa Ally na Babu Ayubu. Bi. Kidude ambaye yupo Dar kwa ziara fupi alikonga nyoyo za mamia ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo kwa kibao chake kisichochuja cha MUHOGO WA JANG'OMBE.

Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, akimtambulisha malkia

Babu Ayubu alichangamsha na kibao chake kipya cha 'Jipu la kwapa' na 'Chaja ya Kobe' nyimbo ambazo anaigiza sauti ya Bi. Kidude na kuleta raha ya aina yake

Huu ni umati mkubwa wa mashabiki uliohudhuria katika onyesho hilo la kukata na shoka kweli lilikuwa ni onyesho kabambe
Bi. Kidude akiwa na Promota wa onyesho hilo John Tall (kushoto) na mwenyeji wake, Yasmin Razak

MBIO ZA VODACOM 5KM FUN RUN ZAFANA MJINI MOSHI!

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini Musa Samizi wa pili toka kushoto akimpatia zawadi yake mshindi wa kwanza wa mbio za kujifurahisha za 5 kilometa Vodacom Fun run Bw.Wilbrodi Kidaga aliyejinyakulia simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi elfu 60 pamoja na fedha alizopewa kwa njia ya M pesa shilingi Elfu 70 asubuhi hii mjini Moshi. Kushoto ni katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru.


Naibu Waziri wa Habari na Michezo Joel Bendera na Mkurugenzi Mkuu wa wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Nector Foya kushoto wakiwa tayari kwa kuanza mbio za 5 kilometa Vodacom Fun run zilizofanyika mjini Moshi leo


washiriki wakichuana mjini Moshi leo


washiriki wa mbio hizo wakikata mbuga leo Moshi

WANARIADHA kutoka Kenya leo wamedhihirisha umahiri wao baada ya kufanya kweli kwa kunyakua nafasi za juu katika mbio za nane za marathoni za Kilimanjaro zilizofanyika jana mkoani Kilimanjaro na kushuhudiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCoBS) mjini Moshi.

Lakini pamoja na hayo Mtanzani Fabian Joseph aliiweza kuing’arisha Tanzania katika mbio za nusu marathoni baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza akiwa amevunja rekodi ya mbio hizo akiwa ametumia muda 1:03:59.

Rekodi ya iliyokuwa inatamba yam bio hizo ilikuwa ni saa 1:o4:15 ambayo ilivunja hiyo jana na bingwa wa zamani wa mbio za nusu marathoni za dunia Joseph kwa kuweka rekodi hiyo mpya baada ya kuwaacha mbali wapinzani wake katika kitimtim hicho na kujinyakulia medali na Sh milioni 1.5.

Nafasi ya pili katika mbio hizo ilichukuliwa pia na Mtanzania mwingine Dickson Marwa ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:04:19 na kujinyakulia kitita cha Sh. 750,000 wakati nafasi ya tatu nayo ilikwenda kwa mwanariadha kutoka Jehi la kujenga Taifa (JKT),Damian Chopa ambaye alitumia muda wa saa 1:04:26 akifuatiwa na Mkenya Mgundu Sagwa alitumia muda wa saa 1:04:28.

Na kuanzia nafasi ya tano hadi kumi zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya ambao walionekana kutamba katika mbio za mwaka huu na kuwafunika wenyeji.

Kwa upande wa wanawake kwenye mbio hizo washindi walikuwa ni Naomi Maiyo kutoka Kenya ambaye alitumia muda wa saa 1:16:26 akifuatiwa na Mkenya mwenzie , Beatrice Ruto aliyetumia muda wa saa 1:16:34 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mtanzania Restituta Joseph aliyetumia muda wa saa 1:16:47.

Lucy Kirimi kutoka Kenya alishika nafasi ya nne akifuatiwa na mshindi wa pili wa mbio hizo kwa mwaka jana ambaye pia alikuwa mwanamichezo bora wa mwaka jana aliyechaguliwa na Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) , Mary Naali aliyeshika nafasi ya tano.

Katika mbio kamili za marathoni za kilometa 42 , nafasi zote tatu za juu kwa upande wa wanaume na wanawake zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya ambapo Steven Chebosus aliyetumia muda wa saa 2:15:32 akifuatiwa na David Kiprono aliyetumia saa 2:16:46 na Julius Tumakar alishika nafasi ya tatu akitumia 2:16:56.

Nafasi za nne na tano zilichukuliwa na wenyeji Tanzania ambapo Ali Juma alishika nafasi ya nne akitumia muda wa saa 2:19:16 na Daud Joseph alinyakua nafasi ya tano na nasi za 6 hadi kumi zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya.

Kwa upande wa wanawake Frida Lodepha ndie alikuwa mshindi wa kwanza akitumia muda wa 2:40:22 akifuatiwa na Evelyn Nyamu aliyetumia saa 2:40:26 na Leah Kusara 2:42:23 akifuatiwa na Truphema kuraui . mbio za hizo kwa wanawake zilitawaliwa na wanariadha kutoka Kenya ambao walishika nafasi zote 10 za juu.

Washindi wa kwanza wa mbio kwa upande wa wanawaume na wanawake walijinyakulia medali na pamoja na Sh milioni tatu kila mmoja .

Katika mbio za kujifurahisha za kilometa tano maarufu kama ‘Vodacom Fun Race’ ambazo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alishiriki pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali,Wilbroad Kidaga aliibuka mshindi wa kwanza na kuzawadiwa simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wa Sh 20,000 na fedha Sh 70,000 kupitia huduma ya M-Pesa .

Wakati Paulo Kalera alishika nafasi ya pili na kujishindia simu pia pamoja na muda wa maongezi wa Sh 20,000 na fedha Sh 50,000 kupitia huduma ya M-Pesa na Doto Ramadhan alishika nafasi ya tatu na ye alizawadiwa simu, muda wa maongezi pamoja na fedha taslimu.



MAKUMBUSHO VILLAGE NA MZALENDO PUB KULIWAKA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO!!

Elystone Angai ambaye ni kiongozi wa bendi ya Mashujaa Music Band akiimba jukwaani wakati bendi hiyo ilipofanya onyesho lake la kwanza kwenye vijiji vya makumbusho kwa mafanikio makubwa huku ikifanikiwa kuteka hisia za mashabiki waliohudhuria kwenye onyesho hili, kutokana na wanamuziki wa bendi hiyo kufanya mambo makubwa katika kila idara hivyo kulimudu vyema jukwaa la vijiji vya Makumbusho ambalo awali bendi ya FM academia ilikuwa ikifanya onyesho lao hapo kila jumamosi lakini sasa ni wakati mwingine na ni zamu ya wana Mashujaa Music Band, hebu mdau watembelee kila jumamosi uone shughuli yao pevu.


Hapa ni shoo kwa kwenda mbele kama unavyoona wanenguaji hawa wakinyonga viuno vyao kisawasawa.

Elystone Angai kiongozi wa Bendi hiyo kulia akiongoza mashambulizi jukwaani huku akiwa analikung'uta gitaa la solo.
Mashabiki mbalimbali wa bendi hiyo wakijimwaga ukumbini hapo wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza kwenye vijiji vya Makumbusho usiku kwa kuamkia leo jijini Dar es salaam.
Yohana "ndugu yake na hela" wapili kulia ambaye ni mdau mkubwa wa Mashujaa Music Band naye alikuwepo kushuhudia burudani hiyo kali kutoka kwa vijana hao ambao wanakuja kwa kasi ya ajabu akiwapa stori marafiki zake.

Huyu ndiye Flora Bamboocha mmoja wa wanenguaji wa Mashujaa Band hapa akifanya vitu vyake jukwaani.
Hawa ndiyo vimwana wa bendi ya Mashujaa Music Bandi iliyokuwa ikiporomosha burudani kali pale vjiji vya Makumbusho usiku wa kuamkia leo.

Dj Makay akiwa kwenye mashine na kufanya mambo makubwa yaliyowafanya wapenzi wa muziki kushindwa kukaa kwenye viti vyao na kucheza muziki kwa muda wote pale Mzalendo Pub Makumbusho, kushoto ni Dj Juice, kulia ni eorge Nzunda na Jofrey Mwakibete kutoka Mo Blog.
Dj Bony Luv katikati na Dj Makay kushoto na rafiki yao wakishoo love.
Wapenzi wa muziki wakitibwilika kwenye ukumbi wa Mzaleno Pub ambapo kila jumamosi kunapigwa disko la kukata na shoka kutoka kwa Dj Bony Luv, Dj Maky na wengine hii ilikuwa usiku wakuamkia leo.

SIMBA YAITANDIKA ZESCO 4-1 UHURU, YANGA BABA JENI BAIBAI!!

Wachezaji wa Simba na Zesco wakichuana vikali wakati wa pambano lao la kujipima nguvu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar leo.
Mashabiki mbalimbali wakiwa wamekaa jukwaa kuu wakiangalia pambano hilo.

Timu ya Simba ya jijini Dar leo imetoka kifua mbele katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam baada ya kuifunga timu ya ZESCO kutoka nchini Zambia magoli 4-1 katika mchezo wa kirafiki uliokuwa mkali wakati wote.
Simba ikicheza kwa kujiamini iliweza kupata magoli mawili kupitia kwa wachezaji wake Nico Nyagawa na Make Barasa kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo huku kila upande ukionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo.
Katika kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani zikitafuta magoli, hata hivyo walikuwa simba tena walioliandama lango la ZESCO na kuongeza magoli mengine mawili kupitia kwa mchezaji wake yuleyule Mike Barasa ambaye alionekana kuwa mwiba mkali kwenye ngome ya timu hiyo ya Zambia
ZESCO walijitutumua na kupata goli moja kwenye kipindi cha pili lililofungwa na mchezaji wao Enock Kasala hivyo kufanya timu hizo kutoka nje zikiwa Simba 4-Zesco 1 mara baada ya mpira kumalizika.
Wakati huohuo taarifa kutoka kwa msemaji wa timu ya Yanga Louis Sendeu zinasema Timu hiyo imefurushwa mbali katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufungwa goli moja na timu ya FC Lupopo katika mchezo uliochezwa katika jimbo la Katanga nchini DRC goli lilifungwa na mabeki wa Yanga baada ya kubabatizwa na washambuliaji wa FC Lupopo katika Dakika ya 89 ya mchezo hivyo Yanga imetolewa kwa magoli 4-2

Rais Kikwete ashiriki Mazishi ya Balozi Daudi Mwakawago jijini Dar!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Seif Shariff Hamad wakati wa mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia Marehemu Balozi Daudi Mwakawago yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni.Katikati ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Wiliam Mkapa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Balozi Daudi Mwakawago wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo mkongwe yaliyofanyika katika makaburi ya kisutu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)


Hitma ya Mzee Kawawa yafanyika leo nyumbani kwake madale!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisamiliana jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Captain John Chiligati na Kingunge Ngombale Mwiru. Rais Kikwete aliktana na viongozi hao katika hitma ya Mzee Rashid Kawawa nyumbani kwake Madale jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (akatikati) akiwa kwenye hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa jana jijini Dar es salaam , wengine ni Mtoto wa Marehemu Vita Kawawa(kulia) na kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Mussa Salum.

Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika jana jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete.

Baadhi ya wakina mama wakiwa katika hitma ya hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika jana jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete.Picha zote Tiganya Vincent-MAELEZO




JARIDA LA KITAALUMA LAZINDULIWA JIJINI DAR!!

Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (SJMC) Dkt Bernadeta Killian ( kulia) akizundua jana jijini Dar es salaam jarida la kitaalum la Scribes liloandaliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) . Katikati ni Rais wa MCT Jaji Robert Kisanga na kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga.
Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (SJMC) Dkt Bernadeta Killian ( kulia) akionyesha machapisho ya majarida mbalimbali baada ya kuyazindua jana jijini Dar es salaam yanayohusu tasnia ya uandishi wa habari ambayo yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) . Katikati ni Rais wa MCT Jaji Robert Kisanga na kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga.
Picha zote na Tiganya Vincent -MAELEZO


SHEREHE ZA MIAKA 33 YA CCM KUFANYIKA UINGEREZA!

CHAMA CHA MAPINDUZI
TAWI LA UINGEREZA
SHEREHE YA KUZALIWA KWA
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
MIAKA 33 YA CCM
Wanachama Wote - C C M
Wakereketwa Wote - C C M
Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote
Tarehe: 06/03/2010 Saa: 10 jioni Hadi Saa 5 usiku
WAPI:
UKUMBI WA: THE WAREHOUSE
1 CUMBERLAND ROAD
READING
RG1 3LB
Mgeni Rasmi
Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara: Mhe Pius Msekwa
Watanzania ambao wangependa kujiandikisha, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size
mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya
uanachama ya mwaka mzima).
Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:
Moses Katega - 07727475313
Victor Mgoya – 07501083328
Maira Migire – 07799212095
Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio, na Muziki Baada ya Shughuli Zote.
Kiingilio – BURE!!!

Mwanamziki mkongwe Hamisi Kitambi ! Amefariki Dunia!

Mwanamziki mkongwe HAMISI KITAMBI amefariki dunia leo 26 February 2010 Dar-es-salaam,
MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI saa 7.00 mchana 27-02-2010 MAGOMENI,Ifunda ,jirani na shule ya
Mzimuni,Jijini Dar-es-salaam.

Mwanamziki mkongwe wa dansi Bw.Hamisi Kitambi,amefariki dunia siku Ijumaa alfajiri ya tarehe 26/02/2010
katika Hospatali ya Muhimbili.
Marehemu aliwahi kupigia bendi za Msondo Ngoma ,kabla ya kupata maumivu ya mguu yaliotokana katika hajali
alipokuwa safarini na bendi ya msondo ngoma .
marehemu pia alikuwa mwanamziki nyota enzi za Tabora jazz,ambako alipigia bendi ya Tabora kabla ya kuhamia
Juwata Jazz sasa Msondo Music band.

Kwa taarifa zaidi tafadhali mnaweza kuwasiliana kwa simu na familia ya marehemu kwa simu namba 0713 802370 Almasi Kassanga.
au Bi.Mwamini Kitambi simu namba 0712 217740

Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi

Rais Kikwete aifariji familia ya marehemu Balozi Daudi Mwakawago jijini Dar es Salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia marehemu Balozi Daudi Mwakawago nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Daisy Mwakawago mjane wa Marehemu Balozi Daudi Mwakawago aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam.Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho jijini Dar es Salaam.Rais alikwenda nyumbani kwa marehemu kuifariji familia yake.Marehemu ameacha mjane na watoto watatu Lulu Mwakawago,Kie Mwakawago na Mtage Mwakawago (picha na Freddy Maro)



MAANDALIZI YA KILI MARATHON 5KM FUN RUN YAENDELEA MJINI MOSHI!!

MAANDALIZI YA KILIMANJARO MARATHON YA VODACOM 5KM FUN RUN YANAENDELEA KWA WASHIRIKI KUJIANDIKISHA NA KUJIANDAA NA MAZOEZI MJINI MOSHI. WATU WENGI WAMEJITOKEZA KUSHIRIKI KATIKA MBIO HIZO MWAKA HUU AMABAZO ZITAANZIA NJE YA GETI LA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI - MUCCOBS URU ROAD, KUELEKEA MZUNGUKO WA YMCA, WAKIMBIAJI WATAPITA KIBO ROAD HADI MZUNGUKO WA MNARA WA SAA, KISHA WATAPANDA KUPITIA BOMA ROAD HADI MAHAKAMA YA WILAYA YA MOSHI KISHA KUELEKEA BARABARA YA ARUSHA HIMO HADI MZUNGUKO WA YMCA NA KURUDI UWANJA WA USHIRIKA.

WADAU WAKIENELEA NA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA.
WASHIRIKI MBALIMBALI WAKIJIANDIKISHA TAYARI KWA KUSHIRIKI MBIO HIZO ZINAZOTARAJIWA KUFANYIKA JUMAPILI.
WASANII WA KEMMON ENTERTAINMENTS WALIKUWEPO KUHAMASISHA MAMBO MBALIMBALI PAMOJA NA KUJIANDIKISHA KUSHIRIKI KATIKA MBIO HIZO.




DK. MWINYI ATAKA BARAZA LIPAMBANE NA ADUI RUSHWA N A UKIMWI!!

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja jijini leo kwa wajumbe wa Baraza kuu la wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa.(kulia) Ni Mnadhimu Mkuu Jeshini Lt. Jenerali Abdulrahman Shimbo.Picha na Mwanakombo Jumaa -Maelezo.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
BARAZA jipya la wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, limetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na tatizo la rushwa na Ukimwi ili kuweza kuimarisha maadili ya watumishi wa umma.
Agizo hilo lilitolewa jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Ali Mwinyi wakati wa uzinduzi wa baraza hilo , uliofanyika jijini Dar es Saalam, ambapo alisema rushwa na Ukimwi ni maadui hatari katika katika nchi yetu na sehemu kubwa ya ulimwengu.“Adui rushwa, huzaa upendeleo kazini, ufisadi wa mali ya umma, mapenzi holela katika sehemu za kazi na ubinafsi ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili ya utumishi wa umma.“Aidha adui Ukimwi yeye anaweza kuifuta wizara yetu kwa kuwaangamiza kidogokidogo watumishi wa umma, wapiganaji na maafisa wetu katika majeshi yetu. “Nawaombeni wote tubadili tabia ya kuwa na wapenzi wengi na tuimarishe ngono salama kwa ajili ya kulinda afya zetu na wenzetu,” alisisitiza Dk.
Mwinyi.Dk. Mwinyi aliwalitaka wajumbe wa baraza hilo, kuondoa dhana potofu ya kubaguana kwa kusema wafanyakazi fulani ni bora kuliko wafanyakazi wa aina nyingine na kuona kuwa wote ni kitu kimoja kama ulivyo mkono na vidole vyake vitano ambayo hutegemeana kwa kila jambo.Aliongeza kwamba majukumu ya baraza la wafanyakazi kulingana na Waraka wa Agizo la Rais Namba 1 la mwaka 1970 ni kushauri uongozi na kupanga sera bila ya malumbano. Wakati huohuo, Dk. Mwinyi alizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao utawawezesha watumishi wa wizara hiyo kutoa huduma zenye ubora zaidi.
Dk. Mwinyi alisema umuhimu wa kuanzishwa kwa mkataba huo ni kuwawezesha wateja na wadau wao kufahamu aina na viwango vya huduma zitakazotolewa na wizara hiyo kwa wakati na jinsi ya kuzipata.Aidha kwa kupitia mkataba huo, wizara hiyo itapata mrejesho wa hudumazake ili kuweza kuziboresha.

Profesa David mwakyusa azindua bodi mpya ya taaisisi ya utafiti wa madawa ya binaadamu- NIMR

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa akiwasili makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Madawa wa Binaadamu jijini Dar akiongozana na Katibu Mkuu wake Mh. Blandina Nyoni mchana huu kuzindua bodi ya taasisi hiyo. Nyuma toka shoto ni Dk. Mwele Malecela, Mganga Mkuu Kiongozi, Dk. Deo Mtasiwa na mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Profesa Samuel Maselle

Profesa David Mwakyusa akiwa na Katibu Mkuu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Kiongozi katika picha ya pamoja na wajumbe wa bdoi mpya ya NMR aliyoizindua leo. Wajumbe wa bodi hiyo mpya ni pamoja na Mbunge wa Mbozi Magharibi Dk. Luka Siyame, Dr Hassan Mshinda, Dr. Edith Ngirwamungu, Jonathan Tangwa, Dr Alaick Abdallah Juma, Profesa Eligius Lyamuya, Dk. Catherine Kuwite, Bi. Elli Pallangyo, Elisa Mjema, Dk Salim Mohamed Abdullah na Dk. Mwele Malecela ndiye katibu wa bodi hiyo

LIGI YA KUMTAFUTA BINGWA WA MBAINGWA KICK BOXING KUMEKUCHA!!

Mwanadaaji wa ligi ya kumtafuta bingwa wamabingwa wa mchezo wa Kick Boxing Tanzania Japhet Kaseba akionyesha kipeperushi wakati alipoongea na wanahabari jijini Dar es salaam kuelezea mambo mbalimbali yatakayofanyika wakati wa mapambano mbalimbali yatakayofanyika kwenye ligi hiyo inayotarajiwa kuanza februari 27 /2010 saa kumi jioni kwenye ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa katika uzito wa Kgs70.
Amesema katika mapambano hayo mikoa saba itakutanisha wapiganaji wake ili kupata washindi watakaoingia kwenye nusu fainali na kisha fainali zinazotarajiwa kufanyika machi 6 /2010 huku zikikutanisha pia wapiganaji wanawake Upendo Njau kutoka Tanzania na Sarah Scott kutoka Afrika Kusini.
Mikoa inayotarajiwa kushiriki katika ligi hiyo na mabondia ni Chande Ali (Lindi), Charles Hangaya (Mwanza), Emmanuel Shija(Shinyanga), Master Shemboko( Muheza), Kanda Kabongo( Dar es salaam) Maiko Deus( Mara), Mrisho Shabaan(Musoma), Putile Gama(Ruvuma) na Khamis Mwakinyo( Tanga)
Zawadi ya mshindi wa kwanza katika ligi hiyo ni Pikipiki kubwa yenye thamani ya shilingi milioni 6 na mipango inafanywa ili kuboresha zawadi kwa washindi wengine wa pili na wa tatu hivyo Japhetn Kaseba ambaye ni mwandaaji ametumia nafasi hiyo kuwaomba watu na makampuni mbalimbali wenye mapenzi mema na mchezo huo, kujitolea na kudhamini ligi hiyo ili kuwapa moyo wachezaji wetu ambao pia inatarajiwa kuwa timu ya taifa ya mchezo huo itatoka katika michezo hiyo.

MASHUJAA MUSIC BAND YA "ELYSTONE ANGAI" YAJA KIVINGINE!!

Kundi zima la Mashujaa Music Band linaloongozwa na mwanamuziki mahiri na mpiga gitaa la solo Elystone Angai wakipiga picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam, ambapo wameelezea kuwa bendi hiyo imeundwa rasmi januari 1 2010 ikiwa na wanamuziki 25.
Elystone Angai amesema bendi hiyo imekaa kambini kwa siku 40 huko Kigamboni ikijiandaa na kufanya mazoezi kwa ajili ya kutoa nyimbo 6 mpya, baadhi ya nyimbo hizo ni
Moshi wa Sigara, Mwanike, Safari ya Vikwazo na wimbo wa mwanike umeimbwa katika lugha mbalimbali ambazo ni kihaya, kiswahili na Kisukuma, hivyo wakazi wa kanda ya ziwa wakae mkao wa kula.
Ameongeza kuwa bendi hiyo itaendelea kutoa burudani kwenye ukumbi wake wa nyumbani pale Mashujaa Night Club Vingunguti kila alhamisi na kutoa burudani nyingine Ijumaa kwenye ukumbi wa Msasani Club, lakini pia uongozi unafanya mipango ili kupata ukumbi wa Makumbusho kwa ajili ya maonyesho zaidi.
Anamalizia kwa kusema wapenzi wa bendi hiyo wakae mkao wa kula kwani Mashujaa Band ambayo tayari imejifua vyakutosha inawahakikishia mashabiki wake burudani na si siasa kama zilivyo bendi zingine.

Rapa wa bendi ya Mashujaa "Mirinda Nyeusi" akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo wakatika wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam leo.



ESTERIANO MAHINGILA WA (BRELLA) APEWA TUZO NA ARIPO!!

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa (ARIPO) African Regional Intellectual Property Organization na Mkurugenzi mtendaji wa Msajili wa makampuni (BRELLA)Bw. Esteriano Mahingila akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati taasisi hiyo ya ARIPO ilipoongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu kusaidia nchi wanachama wa shiriki hilo Afrika katika kulinda na kuelimisha juu ya miliki haki ubunifu, ambapo pia taasisi hiyo inaendesha semina jijini Dar es salaam katika hoteli ya New Africa , inayohusu haki miliki ubunifu katika sekta ya kilimo, wanaofuatia katika picha ni Emanuel Sackey Mkuu wa utafiti RIPO, Grolia Binamungu Ofisa mkuu wa Leseni BRELLA na mwisho ni Flora Mpanju afisa kutoka ARIPO African.
Mkuu wa Utafiti wa shirika la ARIPO Emmanuel Sackey kulia akimkabidhi ngao Mkurugenzi Mtendaji wa Msajili wa Makapuni BRELLA Esteriano Mahingila kama heshima na kutambua mchango wa kazi zake wakati alipokuwa mwenyekiti wa tasisi hiyo ya ARIPO barani Afrika ambapo aliiongoza miaka miwili kwa mafanikio ARIPO ina wanachama 17 katika bara la Africa.

Obama ashindwa kuwashawishi wapinzani!



Rais Barack Obama alifanya kongamano la saa saba na wanasiasa wa Republican katika jaribio la kuwashawishi waunge mkono mpango wake wa bima ya afya.
Lakini baada ya mkutano huo wapinzani hao walisalia na msimamo ule ule. Seneta mmoja wa Republican Lamar Alexander alimweleza Rais Obama kuwa kongamano lake lilikuwa kama muuzaji wa magari anayejaribu kuuza gari lile lile lililokataliwa hapo awali.
Kufuatia msimamo huo Rais Obama amesema atalazimika kusonga mbele na mpango wake hata kama chama cha Republic kitakataa kumuunga mkono.
Rais huyo wa Marekani anapendekeza mfumo ambao utawaruhusu zaidi ya Wamarekani milioni 30 zaidi kupata Bima ya afya.
Mpango huo utagharimu serikali ya Marekani takriban dola bilioni 50 kila mwaka, kiasi ambacho warepublican wanasema ni cha juu sana kwa walipa kodi wa Marekani.

HAPA NI KAMA ANASEMA "MZEE KILA KITU KIKO SAWA"

Rais Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa katika ziara ya kikazi Mashariki ya Kati. Mwingine katika Picha ni Kingunge Ngombale Mwiru.


Mapigano yavunja mkataba wa Darfur!

Imearifiwa kuzuka upya mapigano katika jimbo la Darfur licha ya Rais wa Sudan Omar al-Bashir kutangaza kusitishwa kwa vita eneo hilo la magharibi.
Kundi la kutoa misaada ya utabibu la Ufaransa liitwalo Medecins du Monde limesema limesimamisha harakati zake katika eneo la kati la Darfur la Jebel Marra.
Kundi la waasi wa Sudan Liberation Army (SLA) limedai kumetokea mapigano makali usiku wa Jumatano.
SLA hawakuafikiana na mkataba wa kusitisha mapigano ambao wiki hii serikali ya Sudan ilikubaliana na kundi jingine kubwa la waasi la Jem.
Msemaji wa kundi linalounga mkono SLA Abdel Wahid Mohamed el-Nur amesema majeshi ya serikali yalishambulia maeneo kadha ya milimani, ukiwemo mji wa Deribat.
Hata hivyo upande wa jeshi la Sudan umekanusha kutokea mapigano yoyote. http://www.bbcswahili.com/

SH. BILIONI 38 ZAHITAJIKA KUREJESHA MAKAZI YA KAWAIDA YA WAHANGA WA MAFURIKO KILOSA!!

Makambi ya wahanga wa mafuriko Kilosa.

JUMLA ya sh. bilioni 38 zinahitaji wilayani Kilosa kwa ajili ya kurejesha hali ya kawaida kwa wahanga wa mafuriko.Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego wakati akizungumza na Idara ya Habari (MAELEZO) kuhusu jitihada zinazofanyika kurejesha hali ya makazi ya wahanga wa mafuriko hayo ambayo yalitokea mwishoni mwa Desemba mwaka jana na kuathiri watu 26,000. “Tunahitaji sh. bilioni 38 ili kuweza kurudisha hali ya makazi kwa wahanga wa mafuliko kama ilikuwa awali.
Fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na mahitaji muhimu ya jamii mfano shule na huduma za maji,” alisema mkuu huyo.Alisema ili kuweza kupata fedha hizo wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaomba kuchangia.Aliongeza kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuwatafutia makazi ya kudumu wahanga hao hadi juzi(jana) tayari viwanja 500 vimeshapimwa kwenye maeneo ambayo hayana athari za mafuriko na kazi hiyo bado inaendelea.
Akizungumzia kuhusu hali ya chakula Mratibu wa Maafa, Jenerali Natason Mdeo kutoka Kitengo cha Maafa Osifi ya Waziri Mkuu alisema hakuna tatizo la chakula kwa wahanga hao, hivyo zaidi ya tani 236 za mahindi zimetolewa ambacho kitatosheleza kwa kipindi cha miezi minne na wataongeza nyingine kwa ajili ya cha kukidhi miezi mitatu ijayo.Jenerali Mdoe alisema kwamba wametoa kiasi cha fedha cha zaidi sh.milioni 282 kwa ajili ya kununua mafuta, maharagwe na mbegu huku akiongeza tani 19 za mbegu za aina ya mtama, mahindi na maharagwe zimetolewa pia.
Aliongeza kuwa kitengo hicho kimetoa magodoro 3,000 na vyandarua 6,000Alisema misaada iliyotolewa na jumuiya ya watu Libya imeshawafikia wananchi. Hivi karibuni jumiya hiyo iltoa msaada wa magaro 1,100, blanketi, 400, mahema 1300 na mito 1,200 na maboksi ya madawa vikiwemo vifaa vya huduma ya kwanza na nyumba 15 (mabweni) kati ya 200 zimeshajengwa.

Rais Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa PCCB Mwanza!!

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo unaofanyika mjini Mwanza leo asubuhi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia viongozi waandamizi wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo mjini Mwanza leo asubuhi.

Baadhi ya maafisa waandamizi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo mjini Mwanza leo asubuhi katika ukumbi wa Benki Kuu(picha na Freddy Maro).