Rais Kikwete aifariji familia ya marehemu Balozi Daudi Mwakawago jijini Dar es Salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia marehemu Balozi Daudi Mwakawago nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi.Daisy Mwakawago mjane wa Marehemu Balozi Daudi Mwakawago aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam.Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho jijini Dar es Salaam.Rais alikwenda nyumbani kwa marehemu kuifariji familia yake.Marehemu ameacha mjane na watoto watatu Lulu Mwakawago,Kie Mwakawago na Mtage Mwakawago (picha na Freddy Maro)



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Katika picha ambazo kikwete alishawahi kuonyesha heshima na compassion, hii ni mojawapo. Nimeipenda sana hii photo.

Post a Comment