Obama ashindwa kuwashawishi wapinzani!



Rais Barack Obama alifanya kongamano la saa saba na wanasiasa wa Republican katika jaribio la kuwashawishi waunge mkono mpango wake wa bima ya afya.
Lakini baada ya mkutano huo wapinzani hao walisalia na msimamo ule ule. Seneta mmoja wa Republican Lamar Alexander alimweleza Rais Obama kuwa kongamano lake lilikuwa kama muuzaji wa magari anayejaribu kuuza gari lile lile lililokataliwa hapo awali.
Kufuatia msimamo huo Rais Obama amesema atalazimika kusonga mbele na mpango wake hata kama chama cha Republic kitakataa kumuunga mkono.
Rais huyo wa Marekani anapendekeza mfumo ambao utawaruhusu zaidi ya Wamarekani milioni 30 zaidi kupata Bima ya afya.
Mpango huo utagharimu serikali ya Marekani takriban dola bilioni 50 kila mwaka, kiasi ambacho warepublican wanasema ni cha juu sana kwa walipa kodi wa Marekani.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment