MBIO ZA VODACOM 5KM FUN RUN ZAFANA MJINI MOSHI!

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini Musa Samizi wa pili toka kushoto akimpatia zawadi yake mshindi wa kwanza wa mbio za kujifurahisha za 5 kilometa Vodacom Fun run Bw.Wilbrodi Kidaga aliyejinyakulia simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi elfu 60 pamoja na fedha alizopewa kwa njia ya M pesa shilingi Elfu 70 asubuhi hii mjini Moshi. Kushoto ni katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru.


Naibu Waziri wa Habari na Michezo Joel Bendera na Mkurugenzi Mkuu wa wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Nector Foya kushoto wakiwa tayari kwa kuanza mbio za 5 kilometa Vodacom Fun run zilizofanyika mjini Moshi leo


washiriki wakichuana mjini Moshi leo


washiriki wa mbio hizo wakikata mbuga leo Moshi

WANARIADHA kutoka Kenya leo wamedhihirisha umahiri wao baada ya kufanya kweli kwa kunyakua nafasi za juu katika mbio za nane za marathoni za Kilimanjaro zilizofanyika jana mkoani Kilimanjaro na kushuhudiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCoBS) mjini Moshi.

Lakini pamoja na hayo Mtanzani Fabian Joseph aliiweza kuing’arisha Tanzania katika mbio za nusu marathoni baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza akiwa amevunja rekodi ya mbio hizo akiwa ametumia muda 1:03:59.

Rekodi ya iliyokuwa inatamba yam bio hizo ilikuwa ni saa 1:o4:15 ambayo ilivunja hiyo jana na bingwa wa zamani wa mbio za nusu marathoni za dunia Joseph kwa kuweka rekodi hiyo mpya baada ya kuwaacha mbali wapinzani wake katika kitimtim hicho na kujinyakulia medali na Sh milioni 1.5.

Nafasi ya pili katika mbio hizo ilichukuliwa pia na Mtanzania mwingine Dickson Marwa ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:04:19 na kujinyakulia kitita cha Sh. 750,000 wakati nafasi ya tatu nayo ilikwenda kwa mwanariadha kutoka Jehi la kujenga Taifa (JKT),Damian Chopa ambaye alitumia muda wa saa 1:04:26 akifuatiwa na Mkenya Mgundu Sagwa alitumia muda wa saa 1:04:28.

Na kuanzia nafasi ya tano hadi kumi zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya ambao walionekana kutamba katika mbio za mwaka huu na kuwafunika wenyeji.

Kwa upande wa wanawake kwenye mbio hizo washindi walikuwa ni Naomi Maiyo kutoka Kenya ambaye alitumia muda wa saa 1:16:26 akifuatiwa na Mkenya mwenzie , Beatrice Ruto aliyetumia muda wa saa 1:16:34 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mtanzania Restituta Joseph aliyetumia muda wa saa 1:16:47.

Lucy Kirimi kutoka Kenya alishika nafasi ya nne akifuatiwa na mshindi wa pili wa mbio hizo kwa mwaka jana ambaye pia alikuwa mwanamichezo bora wa mwaka jana aliyechaguliwa na Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) , Mary Naali aliyeshika nafasi ya tano.

Katika mbio kamili za marathoni za kilometa 42 , nafasi zote tatu za juu kwa upande wa wanaume na wanawake zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya ambapo Steven Chebosus aliyetumia muda wa saa 2:15:32 akifuatiwa na David Kiprono aliyetumia saa 2:16:46 na Julius Tumakar alishika nafasi ya tatu akitumia 2:16:56.

Nafasi za nne na tano zilichukuliwa na wenyeji Tanzania ambapo Ali Juma alishika nafasi ya nne akitumia muda wa saa 2:19:16 na Daud Joseph alinyakua nafasi ya tano na nasi za 6 hadi kumi zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya.

Kwa upande wa wanawake Frida Lodepha ndie alikuwa mshindi wa kwanza akitumia muda wa 2:40:22 akifuatiwa na Evelyn Nyamu aliyetumia saa 2:40:26 na Leah Kusara 2:42:23 akifuatiwa na Truphema kuraui . mbio za hizo kwa wanawake zilitawaliwa na wanariadha kutoka Kenya ambao walishika nafasi zote 10 za juu.

Washindi wa kwanza wa mbio kwa upande wa wanawaume na wanawake walijinyakulia medali na pamoja na Sh milioni tatu kila mmoja .

Katika mbio za kujifurahisha za kilometa tano maarufu kama ‘Vodacom Fun Race’ ambazo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alishiriki pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali,Wilbroad Kidaga aliibuka mshindi wa kwanza na kuzawadiwa simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wa Sh 20,000 na fedha Sh 70,000 kupitia huduma ya M-Pesa .

Wakati Paulo Kalera alishika nafasi ya pili na kujishindia simu pia pamoja na muda wa maongezi wa Sh 20,000 na fedha Sh 50,000 kupitia huduma ya M-Pesa na Doto Ramadhan alishika nafasi ya tatu na ye alizawadiwa simu, muda wa maongezi pamoja na fedha taslimu.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment