MASHUJAA MUSIC BAND YA "ELYSTONE ANGAI" YAJA KIVINGINE!!

Kundi zima la Mashujaa Music Band linaloongozwa na mwanamuziki mahiri na mpiga gitaa la solo Elystone Angai wakipiga picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam, ambapo wameelezea kuwa bendi hiyo imeundwa rasmi januari 1 2010 ikiwa na wanamuziki 25.
Elystone Angai amesema bendi hiyo imekaa kambini kwa siku 40 huko Kigamboni ikijiandaa na kufanya mazoezi kwa ajili ya kutoa nyimbo 6 mpya, baadhi ya nyimbo hizo ni
Moshi wa Sigara, Mwanike, Safari ya Vikwazo na wimbo wa mwanike umeimbwa katika lugha mbalimbali ambazo ni kihaya, kiswahili na Kisukuma, hivyo wakazi wa kanda ya ziwa wakae mkao wa kula.
Ameongeza kuwa bendi hiyo itaendelea kutoa burudani kwenye ukumbi wake wa nyumbani pale Mashujaa Night Club Vingunguti kila alhamisi na kutoa burudani nyingine Ijumaa kwenye ukumbi wa Msasani Club, lakini pia uongozi unafanya mipango ili kupata ukumbi wa Makumbusho kwa ajili ya maonyesho zaidi.
Anamalizia kwa kusema wapenzi wa bendi hiyo wakae mkao wa kula kwani Mashujaa Band ambayo tayari imejifua vyakutosha inawahakikishia mashabiki wake burudani na si siasa kama zilivyo bendi zingine.

Rapa wa bendi ya Mashujaa "Mirinda Nyeusi" akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo wakatika wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam leo.



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment