JUMLA ya sh. bilioni 38 zinahitaji wilayani Kilosa kwa ajili ya kurejesha hali ya kawaida kwa wahanga wa mafuriko.Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego wakati akizungumza na Idara ya Habari (MAELEZO) kuhusu jitihada zinazofanyika kurejesha hali ya makazi ya wahanga wa mafuriko hayo ambayo yalitokea mwishoni mwa Desemba mwaka jana na kuathiri watu 26,000. “Tunahitaji sh. bilioni 38 ili kuweza kurudisha hali ya makazi kwa wahanga wa mafuliko kama ilikuwa awali.
Fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na mahitaji muhimu ya jamii mfano shule na huduma za maji,” alisema mkuu huyo.Alisema ili kuweza kupata fedha hizo wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaomba kuchangia.Aliongeza kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuwatafutia makazi ya kudumu wahanga hao hadi juzi(jana) tayari viwanja 500 vimeshapimwa kwenye maeneo ambayo hayana athari za mafuriko na kazi hiyo bado inaendelea.
Akizungumzia kuhusu hali ya chakula Mratibu wa Maafa, Jenerali Natason Mdeo kutoka Kitengo cha Maafa Osifi ya Waziri Mkuu alisema hakuna tatizo la chakula kwa wahanga hao, hivyo zaidi ya tani 236 za mahindi zimetolewa ambacho kitatosheleza kwa kipindi cha miezi minne na wataongeza nyingine kwa ajili ya cha kukidhi miezi mitatu ijayo.Jenerali Mdoe alisema kwamba wametoa kiasi cha fedha cha zaidi sh.milioni 282 kwa ajili ya kununua mafuta, maharagwe na mbegu huku akiongeza tani 19 za mbegu za aina ya mtama, mahindi na maharagwe zimetolewa pia.
Aliongeza kuwa kitengo hicho kimetoa magodoro 3,000 na vyandarua 6,000Alisema misaada iliyotolewa na jumuiya ya watu Libya imeshawafikia wananchi. Hivi karibuni jumiya hiyo iltoa msaada wa magaro 1,100, blanketi, 400, mahema 1300 na mito 1,200 na maboksi ya madawa vikiwemo vifaa vya huduma ya kwanza na nyumba 15 (mabweni) kati ya 200 zimeshajengwa.
0 comments:
Post a Comment