DUNIA YA BUSHOKE KUWASHIKA MWANZA!!

Wakazi wa kanda ya ziwa kaeni mkao wa kula Bushoke atawashika hivi karibuni.

JAQUILINE MOSHA ASHINDA TUZO YA PMTCT MEDIA COMPETITION!!

Mwandishi wa habari kutoka Gazei la Guardian Jaquiline Mosha akipokea tuzo ya Cheti na Shilingi laki tatu kutoka kwa naibu mwakilishi wa UNICEF hapa nchini Ms. Hasmik Egien Were alizoshinda katika shindano la makala za Media Campain on PMTCT Media Competition makala zilizoeleza kupiga vita na kuelimisha maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waandishi wengine 17 kutoka vyombo mbalimbali vya habari pia walikabidhiwa zawadi zao katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo.

KATIBU MKUU WAZARA YA HABARI ATEMBELEA (TSN)!!

Mhariri wa Makala wa Gazeti la Habarileo Oscar Mbuza akitoa Maelezo jinsi wanavyoandaa makala mbalimbali kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka (aliyevaa suti) wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) zilizopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam (Picha na Anna Nkinda wa Habari Maelezo)


Meneja wa Uchapishaji wa magazeti ya Serikali (TSN) John Mcharo akimuelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka (aliyevaa suti) jinsi magazeti hayo yanavyoandaliwa kwa ajili ya kuchapishwa wakati alipotembelea kiwanda chao cha Uchapishaji kilichopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Uchapishaji wa magazeti ya Serikali (TSN) John Mcharo akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka (aliyevaa suti) jinsi magazeti hayo yanavyoandaliwa kwa ajili ya kuchapishwa wakati alipotembelea kiwanda chao cha magazeti kilichopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Habibu Nyundo.


UNYANYASAJI HUU WA ASKARI MGAMBO WA JIJI MPAKA LINI!!

Hapa mmoja wa mgambo hao akibeba Plastiki lililokuwa na mandazi ya kijana huyo aliyokuwa akiuza ili kujipatia mlo na mahitaji mengine ya kibinadamu hata hivyo kijana huyo aliwashinda nguvu na kukimbia kusikojulikana kaazi kwelikweli!.
Hapa anaonekana akipambana nao vilivyo ili wasimchukue na kumpeleka lupango.

Kijana huyu kama anavyoonekana akibebwa juujuu na mgambo wa jiji kwa kilichodaiwa kufanya biashara kiholela katika mtaa wa Garden jijini leo.

MWANAMITINDO MWINYI AHMED APATA MWALIKO AFRIKA KUSINI!!


Mwanamuziki chipukizi wa Bendi ya Machozi inayomilikiwa na Lady Jay Dee na mwanamitindo pia Mwinyi Ahmed anatarajia kuondoka hapa nchini 15/2/2009 kuelekea nchini Afrika kusini kwa mawaliko wa kampuni ya African Disgner ya nchini humo kwa maonyesho kadhaa ya mavazi.
Akizungumza na FULLSHANGWE Mwinyi amesema anatarajia kuongozana na wanamitindo wenzie wa kiume watatu aliowataja kwa jina mojamoja ambao ni Yusuph, Ally na Hemed wote kutoka Dar es alaam.

Mwinyi amesema kuwa wakiwa huko wataonyesha mavazi yatakayobuniwa na kampuni ya African Disgner ya nchini humo na wabunifu wengine chipukizi kutoka nchi mbalimbali, za Afika ameongeza kuwa katika maonyesho hayo ambayo pia atakuwepo mwanamitindo maarufu duniani Naomi Campbell yaatshirikisha pia wabunifu kutoka ufaransa na Italia.
Ametaja miji ambayo watafanya maonyesho hayo kuwa ni Johanesburg, Port Elizaberth. Durban na Victoria, Mwinyi ameongeza kuwa kualikwa kwake katika maonyesho hayo kunamfungulia milango yeye na wanamitindo wengine kutoka hapa nyumbani watakaoshirika katika maonyesho hayo kutambulika kimataifa kwa kuwa maonyesho hayo ya mitindo yanashirikisha watu Maarufu wengi hapa duniani.
Mwanamuziki huyo pia hivi sasa tayari amesharekodi Single yake ya kwanza tangu aanze kuimba kama mwanamuziki wa Machozi Band inayokwenda kwa jina la Ndani ya Mapenzi iliyorekodiwa Mj Records na anatarajia kusambaza kwenye vituo vya redio mwezi ujao mara baada ya kurejea kutoka Afrka ya kusini, FULLSHANGWE tunakutakia kila mafanikio katika kazi zako.

ZIZZOU FASHION STORE VICTORIA NI VIWALO TU KAZI KWENU WADAU!!

Haya jamani ukitaka kutoka mtoko wa kushangweka Wikiendi kwa Viwalo babukubwa nenda ZIZZOU FASHION STORE VICTORIA utapata kila aina ya kiwalo unachokitaka ili upendeze na kuwa mtanashati haya wadau kazi kwenu mi nimeshawamwagia umbea huo maana hiyo ndiyo kazi yangu pata picha zaidi chini.



WALIOKUWA MAOFISA WA BENKI KUU WAFIKISHWA MAHAKAMANI!!

Aliyekuwa mkuu wa utumishi wa Benki kuu ya Tanzania Joachim Liyumba kulia na aliyekuwa Meneja wa Mradi wa Benki hiyo Dawson Kweka wakiwa kizimbani leo mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili Picha kwa hisani www.Michuzi.bogspot.com

WAJASIRIAMALI 400 WA PRIDE TANZANIA WATUNUKIWA VYETI!!

Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu akitoa hotuba yake kwa wahitimu 400 wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na chuo kikuu cha Dar es alaam wakati walipokabidhiwa vyeti vyao na waziri huyo leo mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo kulia ni Mkurugenzi wa Pride Tanzania Bw. Rashid Malima, maafali yamefanyika kwenye tawi la Pride Magomeni

Meneja mkuu wa Pride Tanzania Shimimana Ntuyabaliwe kushoto akimwelekeza waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu kuelekea katika viwanja yalipofanyika maafali ya wajasiriamali 400 wa shirika hilo katika tawai la Pride Magomeni leo mara baada ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na chuo kikuu cha Dar es alaam kulia ni Mkurugenzi wa Pride Tanzania Bw. Rashid Malima.
Hawa ni baadhi ya wahitimu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Dr. Mary Nagu ambaye ni waziri wa viwanda Biashara na Masoko wakati wa maafali hayo.


Kikundi cha ngoma kutoka kijiji cha makumbusho jijini Dar. kikitumbuiza wakati wa maafali ya wajasiriamali 400 wa Pride Tanzania ambao walitunukiwa vyeti vyao leo na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu mara baada ya kuhitimu mafunzo yao yaliyotolewa na chuo kikuu ca Dar es alaam.

TANDALE KWA MTOGOLE NI TAABU TU MVUA IKINYESHA!!


Hii ndiyo hali halisi ya Tandale kwa mtogole jijini Dar es alaam mara mvua inaponyesha mitaa haipitiki kutokana na tope kujaa barabarani hali ambayo inapelekea hata waendesha baiskeli na maguta kupata shida sana wakati wa kupita maeneo hayo kama huyu kijana ambaye alikutwa na Camera ya FULLSHANGWE akihangaika na Guta lake.

THIS WEEK ON M-NET'S STUDIO 53... NIGERIA, GHANA, SOUTH AFRICA, MOZAMBIQUE AND UGANDA






January 2009

DStv audiences are invited to Nigeria, Ghana, South Africa, Mozambique and Uganda this week as M-Net's STUDIO 53 makes stopovers at these destinations during the latest episode of the lifestyle program!

First stop is Lagos, Nigeria where AfricaMagic recently celebrated their fifth birthday. The gala evening kicked off with live entertainment and a 5 star meal. But everyone was here for the same reason, to celebrate the channel that celebrates the continent! The evening focused on celebrating all that AfricaMagic had achieved in five short years, and using that past success to ensure future growth. The evening also honored the people whose vision and contribution have made AfricaMagic a reality.

Then STUDIO53’s Anita is off to Ghana to chat to Tei Huagie about the booming textile business. Huagie graduated from the Ghanatta College of Arts and Design 15 years ago and since then he has been piecing together his own interpretation of textile art. When he’s not sewing metal, Tei turns his attention to making these ‘more wearable’ works of art. Also using fabric as her canvas and taking her inspiration from her daily life in Ghana is Batik artist Edwina Assan. Tune in as STUDIO 53’s Anita tell DStv viewers more about Textile art, that is quickly gaining popularity in Ghana, its art that can be hung, wore or used to decorate.

Also in the show, STUDIO 53’s Mapumba travels to Durban in South Africa to Boyzie Cekwana, co-founder of the Soweto Dance Theatre. When he founded the theatre at the tender age of 18, he knew this was what he wanted to do with his life.
Today he is one of the most sought after dancers and choreographers in South Africa and regularly travels around the world conducting dance workshops.

Next Rosie takes DStv audiences on a trip to Mozambique’s Pemba resort, where only the tides tell time… Touch down on the coast of Pemba and it won’t take long to realize you’ve landed somewhere very special. Untouched beaches and the warm waves of the Indian Ocean invite you to relax and unwind while you soak up the sun. But it won’t be long before the sounds of the sea draws you back to the beach. Here days start and end with the movement of the sun and months are clocked by the changing of the seasons.

Lastly STUDIO 53’s Gaetano attends the Jazz festival in Uganda. The sizzling Jazz Safari is an effort to promote jazz in Uganda, determined not to miss a thing, Gaetano made sure he got some one-on-one time before the show with a couple of the evening’s star performers. Open air jazz concerts like this are held once a month here, at Ange Noir. Uganda’s jazz artists got the audience warmed up and showed off their talent. But the evening’s headliner, Saxophonist Eric Marienthal, stole the show.

DStv audiences in East and West Africa can watch STUDIO 53 on M-NET on Thursday January 29 at 19:30 CAT and on M-Net Series on Saturday January 31 at 18:00 CAT.

PATA MATUKIO MBALIMBALI YA JANA JIJINI!!

Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Utamaduni Tanzania Rose Sayore (kulia) pamoja na wakazi wengine wa Regent Estate (ambao majina yao hayakupatikana) wakijisomea vitabu katika maktaba ya Taasisi ya SOMA wakati wa uzinduzi wa Jarida la SOMA uliofanyika hivi karibuni katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Kijana ambaye jina lake halikuweza kufahamika akiwa amejipumzisha kwenye mtaro ulioko barabara ya Morogoro karibu na kituo cha daladala Ubungo jana jioni jijini Dar es salaam kitendo ambacho ni hatari kwa afya na usalama wa maisha yake. Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

CANAL TOP WA AKUDO IMPACT AWAPIGISHA KWATA ZA SANGWE MASHABIKI!!

Rapa wa Akudo Impact Canal Top kushoto akiwapigisha kwata za shangwe wanenguaji wa bendi yao wakati ilipofanya onyesho lao pale Equator Grill Mtoni ilikuwa shangwe kwa kwenda mbele.
Wanenguaji wa Akudo Impact wakifanya mambo makubwa jukwaani wakati bendi yao ilipofanya onyesho kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni jana.

Mh Temba wa TMK wa pili kutoka kulia alikuwepo pia na washikaji zake.

Mashabiki wa Akudo Impact wakishangweka kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni jana.

KALUNDE YAIMARIKA ZAIDI WAKATI DEO MWANAMBILIMBI ANATARAJIA KUPATA MWENZA!!

Bwana harusi Mtarajiwa Deo Mwanambilimbi na Aminata Nikama wanaimba hivi "Kumagereza kumagereza kumagereza aiyeex2" kwa picha na habari zaidi shuka chini.

Irene Uwoya na rafiki yake Shamy nao wakajiachia kwenye raha za wana Kalunde Band

hilo ndiyo pozi la Debora kulia na Aminata unalionaje mdau wa kushangweka?

kutoka kushoto Debora Nyange, Aminata na Dalola si mchezo jamani yaani raha wanapokua jukwaani

Deo Mwanambilimbi kulia akiwaongoza wanamuziki wenzie kufanya vitu vyao jukwaani wanaofuatia ni Dalola, Aminata na Debora Nyange.

Mwanamuziki mwaalikwa Kasaloo Kyanga kushoto akiimba pamoja na Banana Zorro katika onyesho la bendi ya Kalunde lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Rainbow Mbezi Beach.

Kundi la muziki la Kalunde Band limeendelea kujiimarisha baada ya kununua vyombo vipya hivyo kuongeza uwezo kwa bendi hiyo kuimba muziki mzuri na wenye kiwango cha juu miongoni mwa bendi zilizopo hapa nchini.
Akizungumza na FULLSHANGWE kiongozi wa Bendi hiyo Bwana harusi mtarajiwa Deo Mwanambilimbi amesema wameongeza nguvu katika mfumo mzima wa Bass System kwa maana spika kubwa za besi, kinanda cha kisasa kabisa AMF PSRS 900 Yamaha ambacho ni muundo mpya, Drum mpya za umeme na gitaa la Sollo aina ya Finder la kisasa ambavyo vimeimarisha sana kazi yao kwa ujumla.
Amesema kimsingi maendeleo ya bendi ni mazuri na wanamuziki wanajituma sana kufanya kazi yao kitu ambacho kinaleta mwangaza mpya wa kazi yao kwa sasa na wakati ujao katika bendi yao.
Deo ameongeza kuwa katika kuukaribisha na kuanza mwaka huu wa 2009 tayari wameshaipua kibao kikali kinachokwenda kwa jina la Fikiri kabla ya kuamua ambacho kimetungwa na mwanamuziki Shehe Mwakichui na kurekodiwa studio za Big Time Records ambacho pia waimbaji wakuu ni yeye Deo Mwanambilimbi mwenyewe na Shehe Mwakichui na hiki kibao ndicho kinachokamilisha nyimbo za Albam nzima ya Nataka Nizae na wewe ambayo nyimbo zake zingine zitatambulishwa katika usiku wa wapendanao yaani (Valentine Day) mwezi ujao.
Amesema kuwa tayari wanenguaji wao wawili waliokuwa nchi za Falme za kiarabu kwa kazi za kimuziki Queen Vero na Aminata wamerejea na kujiunga moja kwa moja na Kalunde Band na kuanza kazi, bendi ya Kalunde ambayo kwa sasa imejizolea umaarufu mkubwa hapa jijini kwa kazi yao nzuri inayoonyeshwa na vibao vyao vikali kama vile Nataka nizae na wewe na Itumba ngwewe, kwa wiki wanafanya maonyesho katika kumbi tatu tofauti ambapo siku ya jumatano wanapiga pale Peacock Hotel katika usiku wa mwafrika, ijumaa wanapiga Cine Club na jumamosi wanakuwa pale Rainbow Club pande za Mbezi Beach ambapo ameongza kuwa usalama ni wa hali ya juu katika kumbi hizo pia kuna huduma bora kabisa kwa wateja.
Wakati huohuo habari zaidi zinasema mwanamuziki Deo Mwanambilimbi anatarajia kupata mwenza hivi karibuni anayejulikana kwa jina la Teresia mwenyeji wa mkoa wa Iringa , habari hizo zimeeleza kuwa mambo yote ya taratibu za mambo ya mila na utoaji wa mahari yameshakamilika huko mkoani Arusha ambako anaishi na kinachoendelea ni mipango ya kufunga ndoa ambayo huenda ikafanyika mapema mwezi wa nne.

Muziki wa Utamaduni unaweza kubadili maisha ya msanii kimaendeleo!!

kazi ni kazi na kupiga ngoma za utamaduni ni moja ya kazi ambazo ukifanya kwa misingi na taratibu zake na ukaweza kujiendeleza ipasavyo unaweza kabadilisha maisha yako yakawa ya kiwango cha hali ya juu yaani ukamudu kuendesha maisha na familia yako lakini pia ukaweza kujiletea maendeleo kwani tumeshudia wasanii wengi katika nchi mbalimbali wakifanya kazi zao za sanaa na muziki wa kiutamaduni kwa mafanikio makubwa, hivyo watanzania wenzangu hasa mnaofanya kazi za muziki huu wa kiutamaduni anzeni kubadilika na kuona kuwa muziki wa utamaduni kwanza ni utalii lakini pia unakutambulisha utaifa wako hivyo zingatieni taratibu na mambo muhimu ambayo yanaweza kuwaweka katika kiwango cha kimataifa katika muziki wenu lakini pia nyinyi kama wasanii mjiheshimu ili washabiki wa muziki huu wakiwemo wageni hasa watalii na wengine wawaheshimu na kuzikubali kazi zenu, huyu ni mmoja wa wapiga ngoma katika kikundi cha ngoma za utamaduni kinachaofanya maonyesho yake kwenye kijiji cha makumbusho jijini.

Blog mpya yazaliwa ni ya Evance Mhando wa TBC!!

Ndugu wadau mwana blog mwenzetu mpya ameingia hewani na tuko naye pamoja twamkaribisha kwa shangwe kama ilivyo kauli mbiu yetu wana FULLSHANGWE na huyo si mwingine ni Muandishi na mtangazaji wa TBC Evance Muhando Blog yake inakuja kwa jina la www.tupowote.blogspot.com

Unauonaje Mchuma wa Jamaa mdau!!

Huu ndiyo mchuma wa Rais Barack Obama wa Marekani hebu ucheki.

NYOSHI EL. SADAAT AZUNGUMZIA NA KULAANI WANAMUZIKI WANAOHAMAHAMA BENDI!!

Rais wa Bendi ya FM Academia Nyoshi Al Sadaat akiongea na waandishi wa Habari jana katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam kuhusu athari za wanamuziki kuhamahama katika Bendi mbalimbalimali hapa Nchini. Kushoto ni Meneja wa Bendi hiyo Mujibu Khamisi.


Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia Kalidjo Mwana Kitokolo akiimba wimbo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano baina yao na waandishi hao uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni rais wa Bendi hiyo Nyoshi Al Sadaat akimpigia makofi ili kumpa hamasa zaidi.

SPIKA WA BUNGE AFUNGUA MKUTANO JUU YA UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI WA MASHIRIKA YA UMMA!!

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akifungua mkutano wa siku mbili wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma unaojadili utendaji na uwajibikaji wa mashirika ya Umma katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es salaam , kushoto kwa spika ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Bw. Ludovick Uttoch. (Picha na Aron Msigwa wa Maelezo)


Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya hesabu za mashirika ya Umma Mh: Zitto Kabwe akitoa taarifa kuhusu mashirika sita ya Umma mara baada ya kamati hiyo kuyatembelea ili kutathmini utendaji wa mashirika hayo katika Ukumbi wa mikutano wa Karimjee leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akifuatiwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Karimjee mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Kamati ya Bunge ya hesabu za mashirika ya Umma unaojadili utendaji na uwajibikaji wa mashirika hayo.

BUNGE LA AFRIKA (PAP) LAFUNGUA OFISI ZAKE NCHINI!!

Huu ni ujumbe muhimu kwa waafrika wote jamani.
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri la Afrika (AU) na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mh. Bernad Membe akiwahutubia wageni waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa Ofisi za Bunge la Afrika (PAP)uliofanyika jana katika Hoteli ya Movenpick, bunge hilo sasa litakuwa na ofisi zake nchini zitakazokuwa katika jengo la ofisi ndongo ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es alaam kulia ni afisa wa PAP Salah Majoali kutoka nchini Libya aliyekuwa anatafsiri kwa kifaransa pata matukio mbalimbali katika picha zaidi chini.

Rais wa Bunge la Afrika (PAP) mama Getrude Mongela akitoa hotuba yake mbele ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha jioni baada ya bunge hilo kuzindua ofisi zake jijini Dar es alaam jana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa bungela Afrka (PAP) wa nne kutoka kushoto mara baada ya hafla hiyo iliyofanyika jana Movenpick Hotel baada ya uzinduzi wa ofisi za Bunge hilo jijini Dar es alaam jana.

Rais wa Bunge la Afrika(PAP) mama Getrude Mongela kulia akizungumza na mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Bw. Reginard Mengi wakati wa hafla hiyo.

Model wetu wa leo dada Belinda akipozi katikati ya ramani ya Afrika huku mavazi yake yakiwa na Ramani hiyo ilipendeza kwa kweli.
Dada Belinda aliwakilisha vyema Tanzania yetu kwa mavazi yake yaliyopambwa na maua ya ramani ya Afrika na picha za baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika.

THT kama kawaida yao wakawasha motsi wa kawaida watoto hawa jamani eh! si mchezo.

Msanii Eva Nyambe wa Parapanda Thietre akisoma shairi lilioelekeza makombora kwa Rais wa Bunge la Afrika mama Getrude Mongela kuhakikisha bunge hilo linatatua matatizo mbalimbali yaliyopo katika nchi za Afrika ili kujenga heshima na uaminifu kwa Bunge hilo akitoa mifano ya marais kama Robert Mugabe wa zimbabwe ambao wamesanbabisha matatizo makubwa katika nchi zao.

Parapanda Thietre wakifanya vitu vyao jukwaani.

Waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini wakati kundi la muziki wa asili la Parapanda Thietre likitumbuiza katika hafla hiyo.

Meneja Masoko wa Multchoice Furaha Samalu kulia na wageni walaalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa karibu kila klichoendelea wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Bunge la Afrika jana kwenye Hoteli ya Movenpick.

Meneja masoko wa Tanzania Tourist Board Bw. Geofrey Meena kulia akiwa na Betty Msokia Mkurugenzi wa Haki Elimu na kushoto ni John Ulanga mkurugenzi wa the Foundation For Civil Society Tanzania katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliawa na Bunge la Afrika mara baada ya kuzindua rasmi ofisi zake jijini Dar es alaam iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jana.