SPIKA WA BUNGE AFUNGUA MKUTANO JUU YA UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI WA MASHIRIKA YA UMMA!!

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akifungua mkutano wa siku mbili wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma unaojadili utendaji na uwajibikaji wa mashirika ya Umma katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es salaam , kushoto kwa spika ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Bw. Ludovick Uttoch. (Picha na Aron Msigwa wa Maelezo)


Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya hesabu za mashirika ya Umma Mh: Zitto Kabwe akitoa taarifa kuhusu mashirika sita ya Umma mara baada ya kamati hiyo kuyatembelea ili kutathmini utendaji wa mashirika hayo katika Ukumbi wa mikutano wa Karimjee leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akifuatiwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samwel Sitta akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Karimjee mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Kamati ya Bunge ya hesabu za mashirika ya Umma unaojadili utendaji na uwajibikaji wa mashirika hayo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment