BUNGE LA AFRIKA (PAP) LAFUNGUA OFISI ZAKE NCHINI!!

Huu ni ujumbe muhimu kwa waafrika wote jamani.
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri la Afrika (AU) na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mh. Bernad Membe akiwahutubia wageni waalikwa katika Hafla ya uzinduzi wa Ofisi za Bunge la Afrika (PAP)uliofanyika jana katika Hoteli ya Movenpick, bunge hilo sasa litakuwa na ofisi zake nchini zitakazokuwa katika jengo la ofisi ndongo ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es alaam kulia ni afisa wa PAP Salah Majoali kutoka nchini Libya aliyekuwa anatafsiri kwa kifaransa pata matukio mbalimbali katika picha zaidi chini.

Rais wa Bunge la Afrika (PAP) mama Getrude Mongela akitoa hotuba yake mbele ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha jioni baada ya bunge hilo kuzindua ofisi zake jijini Dar es alaam jana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa bungela Afrka (PAP) wa nne kutoka kushoto mara baada ya hafla hiyo iliyofanyika jana Movenpick Hotel baada ya uzinduzi wa ofisi za Bunge hilo jijini Dar es alaam jana.

Rais wa Bunge la Afrika(PAP) mama Getrude Mongela kulia akizungumza na mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Bw. Reginard Mengi wakati wa hafla hiyo.

Model wetu wa leo dada Belinda akipozi katikati ya ramani ya Afrika huku mavazi yake yakiwa na Ramani hiyo ilipendeza kwa kweli.
Dada Belinda aliwakilisha vyema Tanzania yetu kwa mavazi yake yaliyopambwa na maua ya ramani ya Afrika na picha za baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika.

THT kama kawaida yao wakawasha motsi wa kawaida watoto hawa jamani eh! si mchezo.

Msanii Eva Nyambe wa Parapanda Thietre akisoma shairi lilioelekeza makombora kwa Rais wa Bunge la Afrika mama Getrude Mongela kuhakikisha bunge hilo linatatua matatizo mbalimbali yaliyopo katika nchi za Afrika ili kujenga heshima na uaminifu kwa Bunge hilo akitoa mifano ya marais kama Robert Mugabe wa zimbabwe ambao wamesanbabisha matatizo makubwa katika nchi zao.

Parapanda Thietre wakifanya vitu vyao jukwaani.

Waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini wakati kundi la muziki wa asili la Parapanda Thietre likitumbuiza katika hafla hiyo.

Meneja Masoko wa Multchoice Furaha Samalu kulia na wageni walaalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa karibu kila klichoendelea wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Bunge la Afrika jana kwenye Hoteli ya Movenpick.

Meneja masoko wa Tanzania Tourist Board Bw. Geofrey Meena kulia akiwa na Betty Msokia Mkurugenzi wa Haki Elimu na kushoto ni John Ulanga mkurugenzi wa the Foundation For Civil Society Tanzania katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliawa na Bunge la Afrika mara baada ya kuzindua rasmi ofisi zake jijini Dar es alaam iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment