KATIBU MKUU WAZARA YA HABARI ATEMBELEA (TSN)!!

Mhariri wa Makala wa Gazeti la Habarileo Oscar Mbuza akitoa Maelezo jinsi wanavyoandaa makala mbalimbali kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka (aliyevaa suti) wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) zilizopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam (Picha na Anna Nkinda wa Habari Maelezo)


Meneja wa Uchapishaji wa magazeti ya Serikali (TSN) John Mcharo akimuelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka (aliyevaa suti) jinsi magazeti hayo yanavyoandaliwa kwa ajili ya kuchapishwa wakati alipotembelea kiwanda chao cha Uchapishaji kilichopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Uchapishaji wa magazeti ya Serikali (TSN) John Mcharo akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka (aliyevaa suti) jinsi magazeti hayo yanavyoandaliwa kwa ajili ya kuchapishwa wakati alipotembelea kiwanda chao cha magazeti kilichopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Habibu Nyundo.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment