KALUNDE YAIMARIKA ZAIDI WAKATI DEO MWANAMBILIMBI ANATARAJIA KUPATA MWENZA!!

Bwana harusi Mtarajiwa Deo Mwanambilimbi na Aminata Nikama wanaimba hivi "Kumagereza kumagereza kumagereza aiyeex2" kwa picha na habari zaidi shuka chini.

Irene Uwoya na rafiki yake Shamy nao wakajiachia kwenye raha za wana Kalunde Band

hilo ndiyo pozi la Debora kulia na Aminata unalionaje mdau wa kushangweka?

kutoka kushoto Debora Nyange, Aminata na Dalola si mchezo jamani yaani raha wanapokua jukwaani

Deo Mwanambilimbi kulia akiwaongoza wanamuziki wenzie kufanya vitu vyao jukwaani wanaofuatia ni Dalola, Aminata na Debora Nyange.

Mwanamuziki mwaalikwa Kasaloo Kyanga kushoto akiimba pamoja na Banana Zorro katika onyesho la bendi ya Kalunde lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Rainbow Mbezi Beach.

Kundi la muziki la Kalunde Band limeendelea kujiimarisha baada ya kununua vyombo vipya hivyo kuongeza uwezo kwa bendi hiyo kuimba muziki mzuri na wenye kiwango cha juu miongoni mwa bendi zilizopo hapa nchini.
Akizungumza na FULLSHANGWE kiongozi wa Bendi hiyo Bwana harusi mtarajiwa Deo Mwanambilimbi amesema wameongeza nguvu katika mfumo mzima wa Bass System kwa maana spika kubwa za besi, kinanda cha kisasa kabisa AMF PSRS 900 Yamaha ambacho ni muundo mpya, Drum mpya za umeme na gitaa la Sollo aina ya Finder la kisasa ambavyo vimeimarisha sana kazi yao kwa ujumla.
Amesema kimsingi maendeleo ya bendi ni mazuri na wanamuziki wanajituma sana kufanya kazi yao kitu ambacho kinaleta mwangaza mpya wa kazi yao kwa sasa na wakati ujao katika bendi yao.
Deo ameongeza kuwa katika kuukaribisha na kuanza mwaka huu wa 2009 tayari wameshaipua kibao kikali kinachokwenda kwa jina la Fikiri kabla ya kuamua ambacho kimetungwa na mwanamuziki Shehe Mwakichui na kurekodiwa studio za Big Time Records ambacho pia waimbaji wakuu ni yeye Deo Mwanambilimbi mwenyewe na Shehe Mwakichui na hiki kibao ndicho kinachokamilisha nyimbo za Albam nzima ya Nataka Nizae na wewe ambayo nyimbo zake zingine zitatambulishwa katika usiku wa wapendanao yaani (Valentine Day) mwezi ujao.
Amesema kuwa tayari wanenguaji wao wawili waliokuwa nchi za Falme za kiarabu kwa kazi za kimuziki Queen Vero na Aminata wamerejea na kujiunga moja kwa moja na Kalunde Band na kuanza kazi, bendi ya Kalunde ambayo kwa sasa imejizolea umaarufu mkubwa hapa jijini kwa kazi yao nzuri inayoonyeshwa na vibao vyao vikali kama vile Nataka nizae na wewe na Itumba ngwewe, kwa wiki wanafanya maonyesho katika kumbi tatu tofauti ambapo siku ya jumatano wanapiga pale Peacock Hotel katika usiku wa mwafrika, ijumaa wanapiga Cine Club na jumamosi wanakuwa pale Rainbow Club pande za Mbezi Beach ambapo ameongza kuwa usalama ni wa hali ya juu katika kumbi hizo pia kuna huduma bora kabisa kwa wateja.
Wakati huohuo habari zaidi zinasema mwanamuziki Deo Mwanambilimbi anatarajia kupata mwenza hivi karibuni anayejulikana kwa jina la Teresia mwenyeji wa mkoa wa Iringa , habari hizo zimeeleza kuwa mambo yote ya taratibu za mambo ya mila na utoaji wa mahari yameshakamilika huko mkoani Arusha ambako anaishi na kinachoendelea ni mipango ya kufunga ndoa ambayo huenda ikafanyika mapema mwezi wa nne.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment