Muziki wa Utamaduni unaweza kubadili maisha ya msanii kimaendeleo!!

kazi ni kazi na kupiga ngoma za utamaduni ni moja ya kazi ambazo ukifanya kwa misingi na taratibu zake na ukaweza kujiendeleza ipasavyo unaweza kabadilisha maisha yako yakawa ya kiwango cha hali ya juu yaani ukamudu kuendesha maisha na familia yako lakini pia ukaweza kujiletea maendeleo kwani tumeshudia wasanii wengi katika nchi mbalimbali wakifanya kazi zao za sanaa na muziki wa kiutamaduni kwa mafanikio makubwa, hivyo watanzania wenzangu hasa mnaofanya kazi za muziki huu wa kiutamaduni anzeni kubadilika na kuona kuwa muziki wa utamaduni kwanza ni utalii lakini pia unakutambulisha utaifa wako hivyo zingatieni taratibu na mambo muhimu ambayo yanaweza kuwaweka katika kiwango cha kimataifa katika muziki wenu lakini pia nyinyi kama wasanii mjiheshimu ili washabiki wa muziki huu wakiwemo wageni hasa watalii na wengine wawaheshimu na kuzikubali kazi zenu, huyu ni mmoja wa wapiga ngoma katika kikundi cha ngoma za utamaduni kinachaofanya maonyesho yake kwenye kijiji cha makumbusho jijini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment