MWANAMITINDO MWINYI AHMED APATA MWALIKO AFRIKA KUSINI!!


Mwanamuziki chipukizi wa Bendi ya Machozi inayomilikiwa na Lady Jay Dee na mwanamitindo pia Mwinyi Ahmed anatarajia kuondoka hapa nchini 15/2/2009 kuelekea nchini Afrika kusini kwa mawaliko wa kampuni ya African Disgner ya nchini humo kwa maonyesho kadhaa ya mavazi.
Akizungumza na FULLSHANGWE Mwinyi amesema anatarajia kuongozana na wanamitindo wenzie wa kiume watatu aliowataja kwa jina mojamoja ambao ni Yusuph, Ally na Hemed wote kutoka Dar es alaam.

Mwinyi amesema kuwa wakiwa huko wataonyesha mavazi yatakayobuniwa na kampuni ya African Disgner ya nchini humo na wabunifu wengine chipukizi kutoka nchi mbalimbali, za Afika ameongeza kuwa katika maonyesho hayo ambayo pia atakuwepo mwanamitindo maarufu duniani Naomi Campbell yaatshirikisha pia wabunifu kutoka ufaransa na Italia.
Ametaja miji ambayo watafanya maonyesho hayo kuwa ni Johanesburg, Port Elizaberth. Durban na Victoria, Mwinyi ameongeza kuwa kualikwa kwake katika maonyesho hayo kunamfungulia milango yeye na wanamitindo wengine kutoka hapa nyumbani watakaoshirika katika maonyesho hayo kutambulika kimataifa kwa kuwa maonyesho hayo ya mitindo yanashirikisha watu Maarufu wengi hapa duniani.
Mwanamuziki huyo pia hivi sasa tayari amesharekodi Single yake ya kwanza tangu aanze kuimba kama mwanamuziki wa Machozi Band inayokwenda kwa jina la Ndani ya Mapenzi iliyorekodiwa Mj Records na anatarajia kusambaza kwenye vituo vya redio mwezi ujao mara baada ya kurejea kutoka Afrka ya kusini, FULLSHANGWE tunakutakia kila mafanikio katika kazi zako.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment