WAJASIRIAMALI 400 WA PRIDE TANZANIA WATUNUKIWA VYETI!!

Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu akitoa hotuba yake kwa wahitimu 400 wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na chuo kikuu cha Dar es alaam wakati walipokabidhiwa vyeti vyao na waziri huyo leo mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo kulia ni Mkurugenzi wa Pride Tanzania Bw. Rashid Malima, maafali yamefanyika kwenye tawi la Pride Magomeni

Meneja mkuu wa Pride Tanzania Shimimana Ntuyabaliwe kushoto akimwelekeza waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu kuelekea katika viwanja yalipofanyika maafali ya wajasiriamali 400 wa shirika hilo katika tawai la Pride Magomeni leo mara baada ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na chuo kikuu cha Dar es alaam kulia ni Mkurugenzi wa Pride Tanzania Bw. Rashid Malima.
Hawa ni baadhi ya wahitimu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Dr. Mary Nagu ambaye ni waziri wa viwanda Biashara na Masoko wakati wa maafali hayo.


Kikundi cha ngoma kutoka kijiji cha makumbusho jijini Dar. kikitumbuiza wakati wa maafali ya wajasiriamali 400 wa Pride Tanzania ambao walitunukiwa vyeti vyao leo na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu mara baada ya kuhitimu mafunzo yao yaliyotolewa na chuo kikuu ca Dar es alaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment