‘EL CLASICO’ LIVE THIS WEEKEND!!


April 2009

The Spanish La Liga title race, which had looked over in February when the imperious Barcelona held a 12-point lead, is still very much on ahead of what was once described by former England coach Sir Bobby Robson as the biggest club match in the world.

The rivalry between Barcelona and Real Madrid is legendary, dating back to the Spanish Civil War when the two clubs supported different sides, but is heightened by the fact that the duo, more often than not, are competing head-to-head for the treasured La Liga title.

The latest installment of ‘El Clásico’ is on Saturday, May 2 at the Santiago Bernabéu, when Real will attempt to close the four-point gap between the two sides at the top of the table, while a win for Barca would almost certainly sew up the title.

Real hold the edge in matches between the two, with 68 wins to Barca’s 59, but last time out in December late goals from Lionel Messi and Samuel Eto’o, a former Real player, handed Barca a precious 2-0 win.

So look out for the likes of Messi, Thierry Henry, Xavi Hernandez, Eto’o, Raul, Iker Casillas, Wesley Sneijder and Fabio Cannavaro, all live on SuperSport 7 on Saturday May 2 at 19:30 CAT on DStv.

WATU WAFURIKA HOSPITALI YA TEMEKE KUANGALIA MAJERUHI NA NDUGU ZAO!!

Muuguzi wa Hospitali ya Temeke Anna Mbarouk akimhudumia mmoja wa majeruhi ambaye inasemekana amevunjika mguu habari zinasema majeruhi zaidi ya mia moja wamefikishwa katika Hospitali ya Temeke kwa Matibabu ambapo wengine walitibiwa na kurejea nyumbani na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Muhimbili kwa Matibabu na mmoja wa wafanyakazi katika Hospitali hiyo amesema "idadi kubwa ya Majeruhi hao ilikuwa ni ya wanafunzi zaidi", hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es alaam Mh. Wiliam Lukuvi amesema watu wasiwe na wasiwasi hali imeshadhibitiwa na Vikosi vyetu vya Jeshi la wananchi JWTZ, Polisi na Kikosi cha Zimamoto na wakazi wa huko mbagala wanaweza kurejea makwao, kazi kubwa leo ilikuwa ni kuwatafuta watoto waliopotea kutokana na kukimbia milipuko hiyo ambapo wazai na walezi walikuwa wakihaha huku na kule wakiwatafuta watoto wao ambao maeneo mbalimbali ya jiji.

Hapa baadhi ya majeruhi wakiwa wamepumzishwa na kuwekewa Dripu za maji.


Baadhi ya majeruhi wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke leo jioni waliojeruhiwa kutokana na milipuko hiyo iliyotokea katika kambi ya jeshi mbagala Zakhem.


Askari mgambo ni miongoni mwa vikosi vilivyosaidia kuokoa majeruhi na kuwapeleka Hospitali hapa wakiwa wamejipumzisha nje ya Hospitali ya Temeke baada ya kasi ya kuwaleta majeruhi kupungua.



Umati wa watu mbalimbali waliokwenda Hospitali ya Temeke kutambua ndugu zao waliojeruhiwa katika patashika hilo, hapa wakiwa nje ya uzio wa lango kuu Hospitali hiyo kwani hawakuruhusiwa kuingia kutokana na idadi kubwa ya watu waliofika hospitalini hapo.

MABOMU YALETA KIZAAZAA JIJINI!!

Kamishna wa jeshi la polisi Paul Chagonja akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kutokana na milipuko iliyotokea katika Ghala la Jeshi katika kambi iliyoko mbagala Zhakhem, Kamishna Chagonja akiwa katika eneo la tukio amesema wananchi wawe watulivu wakati jeshi hilo pamoja na Jeshi la wananchi JWTZ wakishirikiana kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzima moto unaowaka, Chagonja amesema watu wasisogee eneo la tukio kwani bado si salama kutokana na milipuko kuendelea kusikika mpaka hali itakapokuwa imetulia ameongeza kuwa ni mapema kueleza chanzo cha milipuko hiyo na hasara yake au madhara yaliyotokea kwa bidadamu, lakini wananchi wawe watulivu watapewa taarifa.
Askari wa jeshi la ulinzi wakifukuza raia wasisogee karibu na eneo la tukio kwa usalama wao, hata hivyo watu wengi waliofika kutaka kushuhudia tukio hilo walikuwa wabishi kuondoka, kana kwamba hawajui madhara wanayoweza kuyapata kutokana na milipuko hiyo.

Na hivi ni vipande vya mabomu vilivyotua mbagala kizuiani baada ya mlipuko kama unavyoona wakazi wa maeneo hayo wakivishangaa.

Hiki ni moja ya kipande cha bomu kilichoruka kutoka eneo la tukio na kutua katika Barabara ya Kirwa baada ya bomu kulipuka.

Katika kila tukio hata kama ni hatari kwa kiasi gani lakini vibaka hawakosekani kama unavyowaona hawa wakiwa wamekamatwa na askasi wa polisi.

Askari wa Usalama Barabarani na Polisi wakiwa wametanda katika maeneo hayo ili kuangalia usalama wa watu na kuzuia watu kuenda eneo la Tukio.

Kamishna wa Oparesheni ya Polisi Paul Chagonja akiongea na vyombo mbalimbali vya kimataifa ikiwemo BBC na Dauch Welle.

Waandishi mbalimbali wakiwa kandokando ya njiapanda ya kwenda kambini huko hakuna anayeruhusiwa kuingia huko kwani hali bado si salama mpaka sasa na mabomu bado yanalipuka.

Eneo la Mbagala Zhakem mahala ambapo kuna barabara inayoingia katika kambi ya jeshi ambako Ghala la kuhifadhia Silaha lielipuka likiwa limezungushiwa uzio milipuko hiyo imeleta Kizaazaa kwa wakazi wa jiji la Dar es alaam na , hakuna mtu wala Mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kuingia katika eneo la tukio Vikosi vya jeshi la ulinzi, zimamoto na Polisi wote kwa pamoja wanajaribu kuzuia watu wasiende katika eneo la tukio.



MARAIS WA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA UJENZI WA BARABARA YA ARUSHA NAMANGA!!



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na marais Mwai Kibaki wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda jana jioni walizindua ujenzi wa barabara ya Arusha Namanga inayoitwa Anthi River Road huko Lengijabe Pembezoni mwa Jiji la Arusha, mara itakapokamilika barabara hiyo itakuwa ni ukombozi kwa wananchi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kupunkwa kiwango kikubwa tatizo la mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

ESPN AIRS EXCLUSIVE INTERVIEW ON THE ANNIVERSARY OF AYRTON SENNA’S DEATH!!

Ayrton Senna Brazil Win1 .

Ayrton Senna 1994.

Ayrton Senna crash.


April 2009

Ayrton Senna da Silva will arguably be remembered as one of the greatest drivers in Formula-One history. A triple Formula One world champion Senna was a legend in his own lifetime. Tune in this May as ESPN pays tribute to Senna on DStv.

Airing on May 1 - the 15 year anniversary of Senna’s death - ESPN will air excerpts from an exclusive interview conducted recently with Dr Sid Watkins, the doctor who first saw Senna after he crashed and died at the San Marino Grand Prix at Imola in 1994, the last time that a driver died during a Formula 1 race.

Senna was charismatic, strong-willed, forceful and seldom vulnerable. Behind the wheel of a racing car he exhibited a 'magic' rarely, if ever before seen. Senna's tragic accident still casts a long shadow into many person related to F1 even today.

In the first part the interview Sid Watkins talks DStv viewers through these tragic events.
Watkins was later appointed President of the FIA Motorsport Safety Council. He spends the latter part of the interview making comparisons with F1 safety today.

Excerpts from the interview with Dr Sid Watkins:

For the full interview tune in on Friday May 1 on ESPN (channel 230) on DStv. Don’t miss all the live coverage of 2009 Formula One season on SuperSport.

KIBONDE AISHANGAA CHAMPAIGN ALIYOIFUNGUA MWEYEWE, PATAMU HAPO MDAU!!

Mtangazaji wa Radio Clouds Fm Efraim Kibonde mwenye vituko vya kuigiza sauti na vichekesho anayetangaza katika kipindi cha (Jahazi) akiishangaa Champaign aliyokuwa ameifungua mwenyewe katika moja ya sherehe ya harusi aliyokuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi , huku wenzie wakimuangalia, kama unavyomuona mdau hapa akiitazama jinsi ilivyokuwa ikifoka kwa kurusha povu juu, Champaign ni kinywaji kinachotumiwa sana katika sherehe mbalimbali Duniani kote na kilivumbuliwa huko Ufaransa miaka ya 1700 na ushee hivi.

VODACOM YAMPELEKA MMOJA WA WASHINDI WA VGSS UBELIGIJI!!

Mkuu wa Udhamini kampuni ya simu za mkononi Vodacom George Rwehumbiza katikati akizungumza na wanahabari katika makao mkuu ya kampuni hiyo jengo la PPF Tower leo Rwehembiza amesema Nyota wa kwanza wa GVSS anaondoka leo kwenda Ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka lakulipwa huko.
Kijana huyu si mwingine ni Francis Casto kutoka Mbeya amabaye ni miongoni mwa washindi watatu waliopatikana katika shindano la Vodacom Global Soccer Star, wenzake ni Salum Saad kutoka Zanzibar na Cosmas Mwazembe kutoka Mbeya.
Rwehumbiza amesema Fracis Casto anaenda nchini Ubeligiji katika shule maalum ya soka inayoitwa Cecle Brugge na atakuwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili akifanya majaribio hayo, Casto ataondoka leo usiku na ndege ya shirika la ndege la KLM wakati washindi wengine wawili Saad na Mwazembe wakisubiri mipango yao ya kwenda kufanya majaribio ikikamilishwa, katika picha wengine ni Francis Casto kulia na Emillian Rwejuna meneja udhamini Vodacom.

AMREF KUZINDUA PROGRAMU YA "ANGAZA ZAIDI"

Dr. Grace Magembe kutoka Manispaa ya Ilala akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakatika Shirika la AMREF linalojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi lilipotangaza kuzindua Programu yake mpya iatakayojulikana kama "ANGAZA ZAIDI" katika picha anayefuta ni Dr. Karen Shelley Mkuu kitengo USAID na AMREF, Ms Blache Pitt Mkurugenzi mkazi AMREF na mwisho ni Meneja Mipango wa ANGAZA ZAIDI.

Virusi vya ukimwi (VVU) na Ukimwi bado vimeendelea kuleta changamoto kubwa katika afya za Watanzania wengi wakati uvumbuzi wa mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hii inaendelea uzoefu umeonyesha kuwa ushauri nasaha na Upimaji wa VVU ni njia muhimu katika kuzuia maambukizi ya ukimwi pamoja na kutoa tiba ya magonjwa nyemelezi.

Katika jitihada zake za kupambana natatizo hili Shirika la Afya na Utafiti Afrika AMREF nchini Tanzania linatarajia kuzindua programu maalum ya miaka mitanoinayojulikana kama ANGAZA ZAIDI.
Programu hii imefadhiliwa na watu wa Marekani kupitia mpango wa Dharura wa Rais wa nchi hiyounaoshughulikia Ukimwi (PEPFAR) mpango huu mpya utatumia mbinu mpya ya kuweza kizifikia jamii zote za Watanzania waishio mijini na vijijini ili waweze kupata huduma za ushauri nasaha, upimaji pamoja na kupatiwa huduma muafaka baada ya upimaji wa VVU ikiwa ni pamoja na utoaji wa rufaa kwa ajili ya tiba.
Hafla ya uzinduzi wa Programu hii utafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es alaam tarehe 28 mwezi Aprili 2009 mgeni rasmi katika hafla hii akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

MEA FOUNDATION NA STANDARD CHATERED BANK WAADHIMISHA SIKU YA MARELIA BAGAMOYO!!

Kikundi Cha Sanaa Arts kikifanya igizo katika kuelimisha jinsi ya kujikinga na mbu wanaoweza kusababisha ugonjwa wa Marelia na lakini pia kuwahi matibabu mara mgonjwa anapohisi kuumwa ugonjwa huo ili apate matibabu mapema kabla hali ahijakuwa mbaya hii ilikuwa katika maadhimisho ya siku ya marelia Duniani ambayo huazimishwa 25 mwezi wa Aprili kila mwaka MEA Foundation iliyopo chini ya kanisa Anglican na Standard Chatered Bank waliadhimisha sherehe hizo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Hoteli ya Kiromo iliyoko nje kidogo ya mji wa Bagamoyo taasisi hizo zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika mapambano dhidi ya Marelia na ukimwi, pata matukio mbalimbali yaliyojiri katika maadhimisho hayo katika picha kwa kushuka chini.
Hapa Kama Unavyoona Chandarua kimefungwa katika kitanda tayari kwa binadamu kukitumia ili kujikinga na ugonjwa wa Marelia.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Jinsia wanawake na Watoto mama Magreti Sitta akipanda mti ikiwa ni ishara ya kuweka mazingira safi hii ilikuwa katika maadhimisho ya mapambano ya marelia Duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Kiromo nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Standard Chatered Jeremy Awori akipanda mti kama ishara ya utunzaji wa mazingira wakati wa maadhimisho ya siku ya Marelia iliyofanyika wilyani Bagamoyo.
Mkurugenzi wa MEA Foundation Bw. Gao John Gao akikaribisha wageni mbalimbali waliofika katika Maadhimisho ya Marelia yaliyofanyika siku ya jumamosi iliyopita katika Hoteli ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya mji wa Bagamoyo

Askofu mkuu kanisa la Anglican Nchini Dr. Valentine Mokiwa kushoto akiwa na Ofisa Mtendaji mkuu wa Benki ya Standard Chatered Jeremy Awori katika maadhimisho hayo, kanisa la Anglican lenye kuendesha Taasisi ya MEA Foundation inayojishughulisha na mapambano ya Marelia na Ukimwi inashirikiana kwa karibu na benki hiyo katika mapambano ya marelia nchini kwa kutoa elimu na ushauri nasaha na kusambaza vyandarua na madawa ya Marelia.

Katibu Muhtasi wa MEA Foundation Cecilia Mwalingo kushoto na Victoria Ketegwe mratibu wa ukimwi katika Taasisi hiyo wakiwa wamekaa wakifuatilia kwa makini kilchokuwa kikiendelea katika maadhimisho hayo ya siku ya Marelia Duniani iliyofanyika Kiromo Hotel nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

ABDULL KUTOKA ZANZIBAR ALAMBA MILIONI 10 ZA MAISHAPLUS!!

Abdull kushoto akiwa na Maulid
Mshiriki wa kijiji cha MaishaPlus Abdull kutoka Zanzibar jana aliibuka kidedea baada ya
kushinda na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10 zilizokuwa zimetangazwa kama zawadi kwa mtu atakayeshinda katika mchezo huo uliokuwa ukisisimua
Katika fainali hiyo iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC1 kutoka kijijini hapo ambapo masanii Malony alikuwa moja wa watu maarufu walioshuhudia fainali hizo na kuwatumbuiza washiriki hao.
Adull aliwashinda wenzake Maulid Wadi, Upendo Peneza, Charles na wengine na kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo kwa mwaka huu wa 2009 Hivyo abdull kutoka Zanzibar ndiyo anaandika historia ya kuanzishwa kwa shindano hili la MaishaPlus kwani kwa ni mara ya kwanza kufanyika na yeye ndiyo mshindi wa kwanza kapatikana
MaishaPlus n i shindano la uhalisia ( Reality Show) ambayo halijawahi kufanyika barani Afrika, ni shindalo linalo 'reflect' maisha halisi ya Mtanzania hasa vijana. Shindano hili lilianza kuonyeshwa kupitia kituo cha TBC1 Machi 1,2009, Mchakato wa kuwatafuta washiriki 18 ulianza Novemba mwaka 2008 katika kanda nane za Tanzania bara na Visiwani.
Lengo la Maisha Plus ni nini? 1. Kuwawezesha vijana kujitambua 2.Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali kupitia semina na mafunzo mbalimbali wanayopewa. 3. Kuendeleza vipaji vyao 4.Kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki. 5. Kubadilishana utamaduni 6. Kuburudisha watazamaji. Malengo ya badae ya Maisha Plus Mwezi wa saba season II ya shindano hili itaanza na safari hii usaili utafanyika katika mikoa yote ya Tanzania. Season III ya shindano hili itajumuisha nchi zote za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi n.k. Waandaaji wa shindano hili ni kampuni ya DMB Inc inayomilikiwa na Masoud Kipanya, Fransis Bonda na David Sevuri. Kipindi hutengenezwa na kampuni ya True Vision Production.

IRENE UWOYA MREMBO ANAYEWAKAMATA MASHABIKI WAKE KATIKA FILAMU!!

Hebu licheki poozi la Irene Uwoya mchezaji wa Filamu anayechipukia sana hivi sasa katika filamu za kibongo nchini huyu amekuwa mcheza Filamu mwenye uwezo mkubwa katika kuuvaa uhalisia wa kile anachokiigiza mara anapopewa nafasi ya kuigiza amekuwa akionyesha mambo makubwa hasa anapopewa nafasi ya kuigiza kama mpenzi wa mwanaume fulani katika Filamu amekuwa akiwavutia mashabiki wengi wa filamu za kibongo Hongera Irene Uwoya kwa kazi nzuri ambayo unafanya katika kuigiza filamu kama umewahi kuona Filamu inayoitwa Oprah ambalo ni jina lake la uigizaji katika Filamu hiyo Uwoya aliigiza kama mpenzi wa Raymondi Kigosi maarufu kama Ray na ameonyesha uwezo mkubwa Filamu nyingine ni Shakila ameigiza kama Shakila akiwa mpenzi wa Ray tena.

ALLY KIBA ATUA NAPOLI TAYARI KWA MAONYESHO YAKE!!

Mwanamuziki Ally Kiba akipokelewa kwa shangwe mara baada ya kuwasili jijini Napoli nchini Italia jana , Kiba yuko huko kwa maonyesho kadhaa kama unavyomuona akipozi kwa picha na Mashabiki waliojitokeza kumpokea mwamuziki huyo mara baada ya kumkabidhi ua kama ishara ya upendo kutoka kwa mashabiki wake nchini humo.

NANI KUONDOKA NA MILIONI 10 LEO MAISHA PLUS?

Shindano la Maisha Plus linafikia tamati Jumapili leo, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 papo hapo baada kudumu kwa siku 56. Shindano hilo lililoanza Machi 1,2009 linafikia tamati ikiwa ni sehemu ya kwanza na ya pekee katika historia ya mashindano ya uhalisia( Reality Shows) nchini Tanzania. Mratibu wa shindano hilo, David Sevuri anasema shindano hilo linamalizika huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa. “Tulilenga kuwawezesha vijana kujitambua,Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali, Kuendeleza vipaji vyao,kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki,kubadilishana utamaduni na kuburudisha watazamaji, tunajivunia kusema kuwa tumeweza kufanikisha yote haya” amesema.
Wtazamaji mbalimbali wa luninga wataweza kuona moja kwa moja kutoka kijijini hapo mshindi akipatikana kati ya washiriki kumi waliobaki kijijini hapo leo usiku kupitia Television ya Serikali TBC1 ambapo saa mbili leo asubuhi walitakiwa kutolewe baadhi ya washiriki na saa nane mchana pia wametolewa washiriki wengine na kubaki watatu ambapo leo kuanzia saa mbili usiku watatolewa washiriki wengine wawili na kubaki mmoja ambaye ndiyo atakuwa mshindi wa shindano hilo FULLSHANGWE inawatakia fainali njema washiriki wote wa MaishaPlus na pia tunampongeza atakayeshinda na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10

PROFESOR J. ATUWAKILISHA VYEMA WANAFULLSHANGWE!!

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya bongofleva Profesor J ambaye pia ni mtunzi bora tuzo za Kili Music Award 2009 tuzo aliyojinyakulia hivi karibuni
alituwakilisha vyema wana FULLSHANGWE wakati alipogawa shangwe zake vyakutosha kwa mashabiki waliofurika kwenye ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga katika mfululizo wa maonyesha hayo yenye lengo la kuzindua Albam yenye nyimbo mchanganiko kutoka kwa wasanii tofauti nchini iliyopewa jina la Shangwe maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni kongwe ya Prime Time Promotion ikishirikiana na Radio ya watu Clouds Fm, onyesho la Shinyanga lilikuwa ndiyo hitimisho la ziara ya maonyesho uzinduzi wa Albam hiyo kote nchini.
Profesor J. akiutikisa mji wa shinyanga kwa kwa kufanya mambo makubwa jukwaani kama unavyoona mdau umti huu wote uko fullshangwe.

Mashabiki mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Albam ya shangwe uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF mkoani shinyanga wakijipa shangwe vyakutosha hapa hata kama mwanamuziki Pr. J angewaambia mguu pande wangeweza kufanya hivyo kutokana na mzuka ulivyowapanda mashabiki hawa kama unavyowaona mdau.


RODRICK NA SALAMA WAMEREMETA, KUFANYA SHEREHE YA KUKATA NA SHOKA KARIMJEE USIKU HUU!!

Rodrick akiwa na maiwaifu wake mara maada ya kufunga ndoa yao leo jioni hii harusi hiyo inafuatiwa na bonge la sherehe itakayofanyika kwenye ukumbi wa karimjee jijini usiku huu FULLSHANGWE inawatakia maisha mema ya ndoa yao takatifu mungu awabariki sana.
Salama akiwa na matroni wake katika pozi

Rodrick na Salama wakiwa na wazazi harusi hiyo inafuatiwa na bonge la sherehe katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar.

Rodrick na Salama wakiwa na wazazi na ndugu na jamaa zao mara baada ya kufunga ndoa .





MWANARIADHA CHIPUKIZI MARY NAALI MWANAMICHEZO BORA 2008!!

Kati ni Mchezabora wa Mwaka Mary Naali akinyanyua juu kikombe chake alichozawadiwa na TASWA baada ya kuwa bwaga Mussa Hassan Mgosi mchezaji wa simba na Athuman Idd Chuji Mary Naali amechaguliwa mchezajibora kutokana na kushinda Medali ya Shaba katika mashindano ya Riadha yaliyofanyika nchini India yakijulikan kama Mumbai Marathon na wakati mwanaradha huyo anashiriki alikuwa hajatimiza miaka 17 hivyo alishiriki akiwa bado na umri mdogo sana lakini pia kwa mwaka jana katika riadha hiyo medali ya shaba kutoka kwa Mary Naali ndiyo medali pekee ambayo Tanzania ilijipatia katika mchezo wa riadha hivyo kuchaguliwa kwake kuwa mwanamichezo bora wa mwaka 2008 kulistahili kabisa ukilinganisha na wanamichezo wengine ambao nao walifanya vizuri pia lakini Mary Naali alikuwa kwenye kiwango cha juu sasa FULLSHANGWE tunamtakia kila mafanikio Mary Naali aili aweze kusonga mbele na kupata mafanikio zaidi katika picha kulia ni Juma Kaseja wa golikipa Yanga amabaye alimwakilisha rafiki yake mshambuliaji wa Simba Mussa Hassan Mgossi na kushoto ni kiungo wa Athuman Idd Chuji wa Yanga, kwa matukio zaidi shuka chini mdau upate yaliyojiri katika hafla hiyo ya kuwatangaza wanamichezo Bora wa Mwaka 2008 iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana usiku.

Kubadilishana mawazo na kupeana maalifa zaidi ni kitu muhimu sana, hawa inawezekana wanapanga mkakati mzito sasa ili kufanikisha mambo yao ukizingatia kuwa pamoja na kuwa waandishi wa habari lakini pia ni wandaaji wa Miss Tanzania katika vitongoji vyaMiss Sinza ambako Saleh Ally anaandaa na Miss Mzizima Mahmoud Zuber ambako anaandaa pia.
Mgeni Rasmi Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mh. Mohamed Seif Khatib akitoa hotuba katika Hafla hiyo kulia ni mwenyekiti wa TASWA Boniface Wambura.
Siku mkulima Amir Mhando alipopigwa picha zaidi ya miambili huku jopo la wapiga picha likiongozwa na kaka Michuzi anayening'iniza Camera katikati, amiri ni Mhariri wa michezo Gazeti la Habari Leo na ni Naibu Katibu mkuu wa TASWA.
Meneja uhusiano wa kampuni ya bia nchini TBL Maneno Mbegu kushoto akimkabidhi kikombe chake na cheti mchezaji wa Yanga Athuman Idd (Chuji) jana

Mtoto wa mchezaji wa Netboli marehemu Grace Daudi Angela Paul akiwa ameshikilia kikombe na cheti alivyozawadiwa marehemu mama yake angela alivipokea kwa niaba mama yake.

Meneja uhusiano Benki ya Standard Chatered Hoyce Temu akimkabidhi zawadi na kikombe Bondia Francis Miyeyusho.

THT walikonga nyoyo za wanamichezo walipokuwa wakitoa burudani katika hafla hiyo jana usiku.
Mwenyekiti wa TASWA Boniface Wambura akitoa hotuba yake fupi katika hafla hiyo.

Mwani kushoto mwandishi wa habari kutoka magazeti ya New Habari akiteta jambo na mwanahabari mwenzie FULLSHANGWE haikunasa jina lake mara moja wakati hafla ya kuwazawadia wanamichezo bora wa mwaka 2008 katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana, wanahabari kwa kuteta jamani si mchezo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya wanamichezo bora wa mwaka 2008 Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mh.Muhamed Seif Khatib kulia akiwa na mwenmyekiti wa Chama cha waandishi wa habari TASWA Boniface Wambura na mmoja wa maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Matadi Yasoda kushoto wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo.

Hapa ni kama vile mwandishi wa habari Eddo Kumwembe akituliza munkari wa Mwenyekiti wa Yanga Imani Mahugila Madega walipokuwa wanapiga stori aliyesimama ni mwandishi Abraham Ojuku na mwisho kulia ni Said Mwishehe wa Majira yote ni burudani tu wadau.

Miamba wawili wakakutana jana hao si wengine ni katibu mkuu wa zamani FAT sasa TFF Richard Wambura kulia na Fredrick Mwakalebela katibu mkuu wa sasa wa TFF shirikisho la mpira wa miguu nchini kama unayoona kila mtu na muda wake lakini baadae walipiga sana stori mdau.

Kutoka kushoto ni waandishi Saleh Ally wa Mwanaspoti, Mhariri wa michezo majira Selemani Mbuguni, Egberti Mkoko wa Star Television na mtoto wa mujini Dj wa siku nyingi KIM hapa naona kama anashangaa jamaa aliyekaa naye karibu hayuko pichani anavyopombeka na glasi yake ya kinywaji.

Katibu mkuu wa TBF Rawlence Cheyo kushoto na mwenyekiti wa DARBA Saimon Msofe wakipanga mikakati yao, hawa ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini kwani wao ndiyo wanaoratibu mambo yote juu ya maendeleo ya mchezo huo.

Wapambanaji Father Kidevu (Mroki. Mroki) kutoka Gazeti la Habari Leo na Suleiman Mpochi wa gazeti la Guardian wakinoanoa vifaa vyao tayari kwa kazi ya kudungua picha.

TIPO kulia Mahmoud Zuberi kati na Golikipa mahiri wa Yanga Juma Kaseja wakibadilishana mawazo ilikuwa imetulia sana wadau.

Mwandishi wa habari mkongwe Rashid Kejo kulia akiongea na mshambuliaji wa Yanga Boniface Ambani

Viongozi waandamizi wa TASWA Abdala Majura wa BBC na Nasongelya kilyinga kutoka Dairy News.

Meneja uhusiano wa benki ya Standard Chatered Hoyce temu na afisa mwanadamizi wa uhsiano wa benki ya NMB Shayrose Banji wakiteta jambo na Irene Kiwia katika sherehe za kumtangaza mchezaji bora wa mwaka 2008 zilizofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana sherehe hizo zilizndaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA.