AMREF KUZINDUA PROGRAMU YA "ANGAZA ZAIDI"

Dr. Grace Magembe kutoka Manispaa ya Ilala akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakatika Shirika la AMREF linalojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi lilipotangaza kuzindua Programu yake mpya iatakayojulikana kama "ANGAZA ZAIDI" katika picha anayefuta ni Dr. Karen Shelley Mkuu kitengo USAID na AMREF, Ms Blache Pitt Mkurugenzi mkazi AMREF na mwisho ni Meneja Mipango wa ANGAZA ZAIDI.

Virusi vya ukimwi (VVU) na Ukimwi bado vimeendelea kuleta changamoto kubwa katika afya za Watanzania wengi wakati uvumbuzi wa mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hii inaendelea uzoefu umeonyesha kuwa ushauri nasaha na Upimaji wa VVU ni njia muhimu katika kuzuia maambukizi ya ukimwi pamoja na kutoa tiba ya magonjwa nyemelezi.

Katika jitihada zake za kupambana natatizo hili Shirika la Afya na Utafiti Afrika AMREF nchini Tanzania linatarajia kuzindua programu maalum ya miaka mitanoinayojulikana kama ANGAZA ZAIDI.
Programu hii imefadhiliwa na watu wa Marekani kupitia mpango wa Dharura wa Rais wa nchi hiyounaoshughulikia Ukimwi (PEPFAR) mpango huu mpya utatumia mbinu mpya ya kuweza kizifikia jamii zote za Watanzania waishio mijini na vijijini ili waweze kupata huduma za ushauri nasaha, upimaji pamoja na kupatiwa huduma muafaka baada ya upimaji wa VVU ikiwa ni pamoja na utoaji wa rufaa kwa ajili ya tiba.
Hafla ya uzinduzi wa Programu hii utafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es alaam tarehe 28 mwezi Aprili 2009 mgeni rasmi katika hafla hii akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment