MEA FOUNDATION NA STANDARD CHATERED BANK WAADHIMISHA SIKU YA MARELIA BAGAMOYO!!

Kikundi Cha Sanaa Arts kikifanya igizo katika kuelimisha jinsi ya kujikinga na mbu wanaoweza kusababisha ugonjwa wa Marelia na lakini pia kuwahi matibabu mara mgonjwa anapohisi kuumwa ugonjwa huo ili apate matibabu mapema kabla hali ahijakuwa mbaya hii ilikuwa katika maadhimisho ya siku ya marelia Duniani ambayo huazimishwa 25 mwezi wa Aprili kila mwaka MEA Foundation iliyopo chini ya kanisa Anglican na Standard Chatered Bank waliadhimisha sherehe hizo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Hoteli ya Kiromo iliyoko nje kidogo ya mji wa Bagamoyo taasisi hizo zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika mapambano dhidi ya Marelia na ukimwi, pata matukio mbalimbali yaliyojiri katika maadhimisho hayo katika picha kwa kushuka chini.
Hapa Kama Unavyoona Chandarua kimefungwa katika kitanda tayari kwa binadamu kukitumia ili kujikinga na ugonjwa wa Marelia.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Jinsia wanawake na Watoto mama Magreti Sitta akipanda mti ikiwa ni ishara ya kuweka mazingira safi hii ilikuwa katika maadhimisho ya mapambano ya marelia Duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Kiromo nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Standard Chatered Jeremy Awori akipanda mti kama ishara ya utunzaji wa mazingira wakati wa maadhimisho ya siku ya Marelia iliyofanyika wilyani Bagamoyo.
Mkurugenzi wa MEA Foundation Bw. Gao John Gao akikaribisha wageni mbalimbali waliofika katika Maadhimisho ya Marelia yaliyofanyika siku ya jumamosi iliyopita katika Hoteli ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya mji wa Bagamoyo

Askofu mkuu kanisa la Anglican Nchini Dr. Valentine Mokiwa kushoto akiwa na Ofisa Mtendaji mkuu wa Benki ya Standard Chatered Jeremy Awori katika maadhimisho hayo, kanisa la Anglican lenye kuendesha Taasisi ya MEA Foundation inayojishughulisha na mapambano ya Marelia na Ukimwi inashirikiana kwa karibu na benki hiyo katika mapambano ya marelia nchini kwa kutoa elimu na ushauri nasaha na kusambaza vyandarua na madawa ya Marelia.

Katibu Muhtasi wa MEA Foundation Cecilia Mwalingo kushoto na Victoria Ketegwe mratibu wa ukimwi katika Taasisi hiyo wakiwa wamekaa wakifuatilia kwa makini kilchokuwa kikiendelea katika maadhimisho hayo ya siku ya Marelia Duniani iliyofanyika Kiromo Hotel nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment