ABDULL KUTOKA ZANZIBAR ALAMBA MILIONI 10 ZA MAISHAPLUS!!

Abdull kushoto akiwa na Maulid
Mshiriki wa kijiji cha MaishaPlus Abdull kutoka Zanzibar jana aliibuka kidedea baada ya
kushinda na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10 zilizokuwa zimetangazwa kama zawadi kwa mtu atakayeshinda katika mchezo huo uliokuwa ukisisimua
Katika fainali hiyo iliyokuwa ikirushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC1 kutoka kijijini hapo ambapo masanii Malony alikuwa moja wa watu maarufu walioshuhudia fainali hizo na kuwatumbuiza washiriki hao.
Adull aliwashinda wenzake Maulid Wadi, Upendo Peneza, Charles na wengine na kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo kwa mwaka huu wa 2009 Hivyo abdull kutoka Zanzibar ndiyo anaandika historia ya kuanzishwa kwa shindano hili la MaishaPlus kwani kwa ni mara ya kwanza kufanyika na yeye ndiyo mshindi wa kwanza kapatikana
MaishaPlus n i shindano la uhalisia ( Reality Show) ambayo halijawahi kufanyika barani Afrika, ni shindalo linalo 'reflect' maisha halisi ya Mtanzania hasa vijana. Shindano hili lilianza kuonyeshwa kupitia kituo cha TBC1 Machi 1,2009, Mchakato wa kuwatafuta washiriki 18 ulianza Novemba mwaka 2008 katika kanda nane za Tanzania bara na Visiwani.
Lengo la Maisha Plus ni nini? 1. Kuwawezesha vijana kujitambua 2.Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali kupitia semina na mafunzo mbalimbali wanayopewa. 3. Kuendeleza vipaji vyao 4.Kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki. 5. Kubadilishana utamaduni 6. Kuburudisha watazamaji. Malengo ya badae ya Maisha Plus Mwezi wa saba season II ya shindano hili itaanza na safari hii usaili utafanyika katika mikoa yote ya Tanzania. Season III ya shindano hili itajumuisha nchi zote za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi n.k. Waandaaji wa shindano hili ni kampuni ya DMB Inc inayomilikiwa na Masoud Kipanya, Fransis Bonda na David Sevuri. Kipindi hutengenezwa na kampuni ya True Vision Production.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment