VODACOM YAMPELEKA MMOJA WA WASHINDI WA VGSS UBELIGIJI!!

Mkuu wa Udhamini kampuni ya simu za mkononi Vodacom George Rwehumbiza katikati akizungumza na wanahabari katika makao mkuu ya kampuni hiyo jengo la PPF Tower leo Rwehembiza amesema Nyota wa kwanza wa GVSS anaondoka leo kwenda Ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka lakulipwa huko.
Kijana huyu si mwingine ni Francis Casto kutoka Mbeya amabaye ni miongoni mwa washindi watatu waliopatikana katika shindano la Vodacom Global Soccer Star, wenzake ni Salum Saad kutoka Zanzibar na Cosmas Mwazembe kutoka Mbeya.
Rwehumbiza amesema Fracis Casto anaenda nchini Ubeligiji katika shule maalum ya soka inayoitwa Cecle Brugge na atakuwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili akifanya majaribio hayo, Casto ataondoka leo usiku na ndege ya shirika la ndege la KLM wakati washindi wengine wawili Saad na Mwazembe wakisubiri mipango yao ya kwenda kufanya majaribio ikikamilishwa, katika picha wengine ni Francis Casto kulia na Emillian Rwejuna meneja udhamini Vodacom.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment