MWANARIADHA CHIPUKIZI MARY NAALI MWANAMICHEZO BORA 2008!!

Kati ni Mchezabora wa Mwaka Mary Naali akinyanyua juu kikombe chake alichozawadiwa na TASWA baada ya kuwa bwaga Mussa Hassan Mgosi mchezaji wa simba na Athuman Idd Chuji Mary Naali amechaguliwa mchezajibora kutokana na kushinda Medali ya Shaba katika mashindano ya Riadha yaliyofanyika nchini India yakijulikan kama Mumbai Marathon na wakati mwanaradha huyo anashiriki alikuwa hajatimiza miaka 17 hivyo alishiriki akiwa bado na umri mdogo sana lakini pia kwa mwaka jana katika riadha hiyo medali ya shaba kutoka kwa Mary Naali ndiyo medali pekee ambayo Tanzania ilijipatia katika mchezo wa riadha hivyo kuchaguliwa kwake kuwa mwanamichezo bora wa mwaka 2008 kulistahili kabisa ukilinganisha na wanamichezo wengine ambao nao walifanya vizuri pia lakini Mary Naali alikuwa kwenye kiwango cha juu sasa FULLSHANGWE tunamtakia kila mafanikio Mary Naali aili aweze kusonga mbele na kupata mafanikio zaidi katika picha kulia ni Juma Kaseja wa golikipa Yanga amabaye alimwakilisha rafiki yake mshambuliaji wa Simba Mussa Hassan Mgossi na kushoto ni kiungo wa Athuman Idd Chuji wa Yanga, kwa matukio zaidi shuka chini mdau upate yaliyojiri katika hafla hiyo ya kuwatangaza wanamichezo Bora wa Mwaka 2008 iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana usiku.

Kubadilishana mawazo na kupeana maalifa zaidi ni kitu muhimu sana, hawa inawezekana wanapanga mkakati mzito sasa ili kufanikisha mambo yao ukizingatia kuwa pamoja na kuwa waandishi wa habari lakini pia ni wandaaji wa Miss Tanzania katika vitongoji vyaMiss Sinza ambako Saleh Ally anaandaa na Miss Mzizima Mahmoud Zuber ambako anaandaa pia.
Mgeni Rasmi Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mh. Mohamed Seif Khatib akitoa hotuba katika Hafla hiyo kulia ni mwenyekiti wa TASWA Boniface Wambura.
Siku mkulima Amir Mhando alipopigwa picha zaidi ya miambili huku jopo la wapiga picha likiongozwa na kaka Michuzi anayening'iniza Camera katikati, amiri ni Mhariri wa michezo Gazeti la Habari Leo na ni Naibu Katibu mkuu wa TASWA.
Meneja uhusiano wa kampuni ya bia nchini TBL Maneno Mbegu kushoto akimkabidhi kikombe chake na cheti mchezaji wa Yanga Athuman Idd (Chuji) jana

Mtoto wa mchezaji wa Netboli marehemu Grace Daudi Angela Paul akiwa ameshikilia kikombe na cheti alivyozawadiwa marehemu mama yake angela alivipokea kwa niaba mama yake.

Meneja uhusiano Benki ya Standard Chatered Hoyce Temu akimkabidhi zawadi na kikombe Bondia Francis Miyeyusho.

THT walikonga nyoyo za wanamichezo walipokuwa wakitoa burudani katika hafla hiyo jana usiku.
Mwenyekiti wa TASWA Boniface Wambura akitoa hotuba yake fupi katika hafla hiyo.

Mwani kushoto mwandishi wa habari kutoka magazeti ya New Habari akiteta jambo na mwanahabari mwenzie FULLSHANGWE haikunasa jina lake mara moja wakati hafla ya kuwazawadia wanamichezo bora wa mwaka 2008 katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana, wanahabari kwa kuteta jamani si mchezo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya wanamichezo bora wa mwaka 2008 Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mh.Muhamed Seif Khatib kulia akiwa na mwenmyekiti wa Chama cha waandishi wa habari TASWA Boniface Wambura na mmoja wa maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Matadi Yasoda kushoto wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo.

Hapa ni kama vile mwandishi wa habari Eddo Kumwembe akituliza munkari wa Mwenyekiti wa Yanga Imani Mahugila Madega walipokuwa wanapiga stori aliyesimama ni mwandishi Abraham Ojuku na mwisho kulia ni Said Mwishehe wa Majira yote ni burudani tu wadau.

Miamba wawili wakakutana jana hao si wengine ni katibu mkuu wa zamani FAT sasa TFF Richard Wambura kulia na Fredrick Mwakalebela katibu mkuu wa sasa wa TFF shirikisho la mpira wa miguu nchini kama unayoona kila mtu na muda wake lakini baadae walipiga sana stori mdau.

Kutoka kushoto ni waandishi Saleh Ally wa Mwanaspoti, Mhariri wa michezo majira Selemani Mbuguni, Egberti Mkoko wa Star Television na mtoto wa mujini Dj wa siku nyingi KIM hapa naona kama anashangaa jamaa aliyekaa naye karibu hayuko pichani anavyopombeka na glasi yake ya kinywaji.

Katibu mkuu wa TBF Rawlence Cheyo kushoto na mwenyekiti wa DARBA Saimon Msofe wakipanga mikakati yao, hawa ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini kwani wao ndiyo wanaoratibu mambo yote juu ya maendeleo ya mchezo huo.

Wapambanaji Father Kidevu (Mroki. Mroki) kutoka Gazeti la Habari Leo na Suleiman Mpochi wa gazeti la Guardian wakinoanoa vifaa vyao tayari kwa kazi ya kudungua picha.

TIPO kulia Mahmoud Zuberi kati na Golikipa mahiri wa Yanga Juma Kaseja wakibadilishana mawazo ilikuwa imetulia sana wadau.

Mwandishi wa habari mkongwe Rashid Kejo kulia akiongea na mshambuliaji wa Yanga Boniface Ambani

Viongozi waandamizi wa TASWA Abdala Majura wa BBC na Nasongelya kilyinga kutoka Dairy News.

Meneja uhusiano wa benki ya Standard Chatered Hoyce temu na afisa mwanadamizi wa uhsiano wa benki ya NMB Shayrose Banji wakiteta jambo na Irene Kiwia katika sherehe za kumtangaza mchezaji bora wa mwaka 2008 zilizofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana sherehe hizo zilizndaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment