PROFESOR J. ATUWAKILISHA VYEMA WANAFULLSHANGWE!!

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya bongofleva Profesor J ambaye pia ni mtunzi bora tuzo za Kili Music Award 2009 tuzo aliyojinyakulia hivi karibuni
alituwakilisha vyema wana FULLSHANGWE wakati alipogawa shangwe zake vyakutosha kwa mashabiki waliofurika kwenye ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga katika mfululizo wa maonyesha hayo yenye lengo la kuzindua Albam yenye nyimbo mchanganiko kutoka kwa wasanii tofauti nchini iliyopewa jina la Shangwe maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni kongwe ya Prime Time Promotion ikishirikiana na Radio ya watu Clouds Fm, onyesho la Shinyanga lilikuwa ndiyo hitimisho la ziara ya maonyesho uzinduzi wa Albam hiyo kote nchini.
Profesor J. akiutikisa mji wa shinyanga kwa kwa kufanya mambo makubwa jukwaani kama unavyoona mdau umti huu wote uko fullshangwe.

Mashabiki mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Albam ya shangwe uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF mkoani shinyanga wakijipa shangwe vyakutosha hapa hata kama mwanamuziki Pr. J angewaambia mguu pande wangeweza kufanya hivyo kutokana na mzuka ulivyowapanda mashabiki hawa kama unavyowaona mdau.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment