NANI KUONDOKA NA MILIONI 10 LEO MAISHA PLUS?

Shindano la Maisha Plus linafikia tamati Jumapili leo, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 papo hapo baada kudumu kwa siku 56. Shindano hilo lililoanza Machi 1,2009 linafikia tamati ikiwa ni sehemu ya kwanza na ya pekee katika historia ya mashindano ya uhalisia( Reality Shows) nchini Tanzania. Mratibu wa shindano hilo, David Sevuri anasema shindano hilo linamalizika huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa. “Tulilenga kuwawezesha vijana kujitambua,Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali, Kuendeleza vipaji vyao,kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki,kubadilishana utamaduni na kuburudisha watazamaji, tunajivunia kusema kuwa tumeweza kufanikisha yote haya” amesema.
Wtazamaji mbalimbali wa luninga wataweza kuona moja kwa moja kutoka kijijini hapo mshindi akipatikana kati ya washiriki kumi waliobaki kijijini hapo leo usiku kupitia Television ya Serikali TBC1 ambapo saa mbili leo asubuhi walitakiwa kutolewe baadhi ya washiriki na saa nane mchana pia wametolewa washiriki wengine na kubaki watatu ambapo leo kuanzia saa mbili usiku watatolewa washiriki wengine wawili na kubaki mmoja ambaye ndiyo atakuwa mshindi wa shindano hilo FULLSHANGWE inawatakia fainali njema washiriki wote wa MaishaPlus na pia tunampongeza atakayeshinda na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment