WATU WAFURIKA HOSPITALI YA TEMEKE KUANGALIA MAJERUHI NA NDUGU ZAO!!

Muuguzi wa Hospitali ya Temeke Anna Mbarouk akimhudumia mmoja wa majeruhi ambaye inasemekana amevunjika mguu habari zinasema majeruhi zaidi ya mia moja wamefikishwa katika Hospitali ya Temeke kwa Matibabu ambapo wengine walitibiwa na kurejea nyumbani na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Muhimbili kwa Matibabu na mmoja wa wafanyakazi katika Hospitali hiyo amesema "idadi kubwa ya Majeruhi hao ilikuwa ni ya wanafunzi zaidi", hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es alaam Mh. Wiliam Lukuvi amesema watu wasiwe na wasiwasi hali imeshadhibitiwa na Vikosi vyetu vya Jeshi la wananchi JWTZ, Polisi na Kikosi cha Zimamoto na wakazi wa huko mbagala wanaweza kurejea makwao, kazi kubwa leo ilikuwa ni kuwatafuta watoto waliopotea kutokana na kukimbia milipuko hiyo ambapo wazai na walezi walikuwa wakihaha huku na kule wakiwatafuta watoto wao ambao maeneo mbalimbali ya jiji.

Hapa baadhi ya majeruhi wakiwa wamepumzishwa na kuwekewa Dripu za maji.


Baadhi ya majeruhi wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke leo jioni waliojeruhiwa kutokana na milipuko hiyo iliyotokea katika kambi ya jeshi mbagala Zakhem.


Askari mgambo ni miongoni mwa vikosi vilivyosaidia kuokoa majeruhi na kuwapeleka Hospitali hapa wakiwa wamejipumzisha nje ya Hospitali ya Temeke baada ya kasi ya kuwaleta majeruhi kupungua.



Umati wa watu mbalimbali waliokwenda Hospitali ya Temeke kutambua ndugu zao waliojeruhiwa katika patashika hilo, hapa wakiwa nje ya uzio wa lango kuu Hospitali hiyo kwani hawakuruhusiwa kuingia kutokana na idadi kubwa ya watu waliofika hospitalini hapo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. Shangwe uko juu. just tufanye jitiada za kujitangaza.Ninauhakika mtu akitutembelea mara moja basi tumemteka. ILA JARIBU KUTOA MAMBO YA VERIFICATION WORD

  2. nashukuru kwa maoni yako mazuri nitajitahidi sana ndugu una moyo wa kizalendo

Post a Comment