JENGO LA PPF TOWER LANUSURIKA KULIPUKA MOTO ASUBUHI HII!!

Hii ni Sehemu ambayo ilipata hitilafu ya umeme katika jengo la PPF Tower mtaa wa Garden na Ohio ghorofa ya 15 kwenye ofisi za kampuni ya simu za mkononi Vodacom kitengo cha Fedha, sakata hilo limetokea asubuhi hii yapata kama saa tatu kasorobo hivi ambapo zilisikika kelele za mmoja wa wafanayakazi wa kampuni hiyo kuashiria moto, huku moshi mkubwa ukitanda katika ofisi hiyo, kitu kilichawafanya wafanyakazi wengine kuanza kutimua mbio wakishuka chini ya jengo na kutoka nje, hata hivyo walifanya mawasiliano na kikosi cha zimamoto kutoka kampuni ya knight Surport ambao waliwahi katika eneo la tukio na kudhibiti hali hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa kikosi cha zimamoto kutoka kampuni hiyo Bw. Glad Billy Moyo amesema "ulikuwa mlipuko mdogo uliotokea kwenye Tubelight (Taa)ya moja ya vyumba vya jengo hilo ghorofa ya 15, na kusababisha moshi mkubwa uliwashtua wafanayakazi wengi waliokuwemo katika jengo hilo, hata hivyo Glad amesema hakuna madhara yoyote yaliyotokea na moto umedhibitiwa hivyo watu wanaweza kuendelea na shughuli zao kama kawaida
Wafanyakazi wa kikosi cha kuzima cha kampuni ya Knight Surport wakiwa katika picha ya pamoja katika ghorofa ya 15 ya jengo hilo mara baada ya kukamilisha zoezi la kudhibiti moto huo.

Magari ya kampuni ya kikosi cha kuzima moto cha Knight Surport yakiwa yameegeshwa chini ya jengo hilo tayari kwa kukabiliana na moto huo leo asubuhi huku watu mbalimbali wanaofanya kazi katika makampuni yaliyopanga kwenye jengo hilo wakiwa nje ya jengo kusubiri hatma ya moto huo.

Jengo la PPF Tower kamalinavyoonekana leo asubuhi lilinusurika kulipuka moto baada ya hitilafu kutokea katika ghorofa ya 15 leo asubuhi.

MELI NYINGINE YA ABIRIA YAKWAMA KARIBU NA BANDARI YA MALINDI!!

Inasemekana kuwa Boti zilizokuwa zikifanya kazi ya uokoaji zimesitisha kwa muda kazi hiyo ili kwenda kuivuta meli nyingine ya abiria, habari zinasema meli hiyo imepata hitirafu karibu kabisa na Gati ya bandari ya Malindi, Meli hiyo ni ya abiria lakini haikufahamika mara moja inaitwaje inadawiwa ilikuwa ikitokea Dar as alaam kwenda Zanzibar haikufahamika mara moja ni tatizo gani limeitokea na lina ukubwa wa kiasi gani, tukio kama hili litakuwa linawatia hofu abiria waliomo katika meli hiyo ukizingatia kwamba bado hawajasahau tukio la kuzama kwa meli ya Fatih siku mbili zilizopita ambayo mpaka sasa bado waokoaji wanaendelea kutafuta kama kuna ya watu miili watu zaidi na kujaribu kuiibua tena meli hiyo ambapo mpaka sasa ni maiti sita zilizopatikana na watu 27 wameokolewa wakiwa hai.

VODACOM MISS KIGAMBONI 2009 APATIKANA!!

Vodacom Miss Kigamboni 2009 Karne Lukule

Mshindi wa Vodacom Miss Kigamboni 2009 Karne Lukule (kati) akiwa na washindi wenzake Irene Chentopher (kushoto) ambaye alishika nafasi ya pili na Samirah Kafunda aliyeshika namba Tatu shindano hilo liliandaliwa na Kampuni ya Bongo5 Entertiment. na lilifanyika jana kwenye ukumbi wa Meese Resort Kigamboni
Majaji wakiwajibika kumtafuta mshindi wakiongozwa na Ben Kisaka jaji mkuu (kulia) ,Miss kigamboni 2008 Lona Swai (kushoto) na Joketi Mwegelo ambaye alikuwa Miss Temeke 2007, na alishika nafasi za juu Miss Tanzania mwaka 2007.

Warembo walioshiriki shindano la kumsaka Vodacom Miss kigamboni lililofanyika jana wakionyesha shoo ya ufunguzi wakati wa shindano hilo katika ukumbi wa Meese Resort Kigamboni .

VIDEO ZA BABY MADAHA NA FEISAL ISMAIL ZAFUNIKA, ZAANZA KUUZWA MADUKANI!!

Nilesh Bhatt mkurugenzi wa uzalishaji wa kampuni ya Pilipili Entertainment akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa kampuni hiyo na Video mbili za wanamuziki Feisal Ismail na Baby Madaha uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana.
Bw. Nilesh Bhatt Amesema kuwa Albam hizi zimerekodiwa katika kiwango cha hali ya juu kwa kushirikisha wasani wengine kamaPancho Latino Chid Benzi, Nura, Mr. Blue na Feri Kano, ambapo albam ya Baby Madaha inalenga katika Mapenzi na Albam ya Feisal inalenga katika mambo ya kutumaini mafanikio, ameongeza kuwa wimbo wa Baby Madaha unafundisha kwa kiwango kikubwa, kwani zaidi ya miaka 50 iliyopita Utamaduni wa India ulikuwa umejifunga sana lakini kwa sasa unaanza kufunguka na kuingiliana na tamaduni nyingine nyingi, hivyo mabadiliko yataanza kutokea kadiri siku zinavyoenda na nyimbo hii ya Baby hakika itakuwa ni Fundisho zuri kwa jamii za watu wa nchi zote mbili yaani India na Tanzania.
Waziri wa Viwanda na Biashara mama Marry Nagu akionyesha video ya Feisal Ismail mara baada ya kuizindua rasmi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana ambapo pia aliizindua kampuni ya Pilipili Entertainment iliyotengeneza Video za wanamuziki hao nchini India kushoto ni Nilesh Bhatt mkurugenzi wa uzalishaji kampuni ya Pilipili.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika akionyesha Video ya Baby Madaha mara baada ya kuizindua rasmi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kushoto ni mkurugenzi wa uzalishaji kampuni ya Pilipili Entertainment Nilesh Bhatt.

Mkurugenzi na Mbunifu wa mavazi kutoka kampuni ya Carpuany and Design Mamaa Grace Sinamwita kulia akipozi katika picha na Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Ritah Paulsen wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Pilipili Entertainment uliofanyika jana sambamba na uzinduzi wa Video mbili za wanamuziki Baby Madaha na Faisal Ismail kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

Meneja mkuu wa Vituo vya Radio na Televisheni vya East Fm, Nairobi Star, Classic 105 na Kiss Fm kutoka Nairobi nchini kenya Martin Khafafa akizungumza katika uzinduzi wa Video za wanamuziki wawili Feisal na Baby Madaha uliofanyika jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kulia ni mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Fm na miliki wa kikundi cha muziki cha THT Ruge Mutahaba.

Wakurugenzi, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Pilipili Entertainment wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Kampuni hiyo na video mbili za Baby Madaha na Feisal kufanyika jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

Kutoka kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, Mwanamuziki Feisal Ismail maadam Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchimark Production kampuni, ambayo pia inaandaa Bongo Star Search na Waziri wa Viwanda na Biashara mama Marry Nagu wakiwa katika picha ya pamoja, Feisal aliibuliwa na Bongo Star Search mpaka hapo alipofikia katika mafanikio yake.
Feisal Ismail naye akifanya vitu vyake jukwaani.

Baby Madaha akithibitisha ubora wake jukwaani wakati wa Uzinduzi wa Video yake .

Burudani kwa kwenda mbele

Dada Agricola Kossey kutoka shirika la Save Albino Tanzania hakutaka kukosa kile kilichofanywa na wanamuziki Feisal Ismail na Baby Madaha kama unavyomuona katika picha akiwa makini ili kuona ubora wa Video Hizo.

Hawa ndiyo waliowezesha shughuli hii nzima kushoto ni Sophia Mdecha Meneja Matukio wa Pilipili Entertainment na Simbiso Machine Meneja uhusiano wa Kampuni hiyo wakipozi kwa picha, mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa Video hizo sambamba na Kampuni ya Pilipili kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana.

Wataalamu hawa wa kuchanganya picha nao walikuwa bize kwelikweli ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa hebu wacheki mdau.

Mh. Marry Nagu Waziri wa Viwanda na Biashara kulia Mh. George Mkuchika Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo katikati na mwanamuziki Feisal Ismail wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi huo, hii ni dalili kuwa viongozi hao wa kitaifa wamevutiwa sana na kijana Feisal kutokana na kazi yake nzuri itakayomtangaza vyema yeye binafsi na Tanzania kwa ujumla katika Anga za muziki.
Miss Tanzania 2007 Richa Adhia na mama yake Maria Adia kulia wakipozi katika picha wakati wa uzinduzi wa Video mbili za wanamuziki Baby Madaha na Feisal Ismail kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana usiku

Hili ni Jopo la waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifutilia uzinduzi huo ili kujua kila kilichojiri wakiwa tayari kuupasha umma juu ya uzinduzi huo.

Baadi ya washabiki na wapenzi mbalimbali wa muziki wakifuatilia matukio ya uzinduzi huo.

Kaka Rwaga na Maiwaifu wake Dina nao hawakutaka kukosa uzinduzi huo uliokuwa wa kukata na shoka kama unavyoona matukio katika picha mdau.

Mamaa Frolence akiwa na rafiki yake Annet kati na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania wakifuatilia Yason Mashaka kwa karibu kila kilichoendelea katika uzinduzi wa Video mbili za wasanii Baby Madaha na Feisal Ismail jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

HIVI NDIVYO MELI YA MV FATIH ILIVYOZAMA KATIKA BANDALI YA MALINDI ZANZIBAR!!


MELI YA ABIRIA NA MIZIGO YA MV FATIH ZANZIBAR BAADA YA KUPINDUKA NA KUZAMA KATIKA BANDARI YA MALINDI ZANZIBAR JANA USIKU KAMA INAVYOONEKANA KATIKA PICHA AMBAPO INADAIWA KUWA NA ABIRIA KADHAA LAKINI HADI LEO MCHANA ABIRIA 27 TAYARI WALIKUWA WAMEOKOLEWA PAMOJA NA KUPATIKANA MAITI TATU AKIWEMO MTOTO WA KIUME NA MWANAMKE MMOJA, HATA HIVYO KUNA HABARI ZIMETUFIKIA HIVI PUNDE ZINANSEMA TAYARI KUNA MELI YA JESHI LA WANANCHI IMESHAFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO NA WAMESHAANZA KAZI YA KUJARIBU KUOKOA WATU WALIONASA KATIKA MELI HIYO, HABARI ZINASEMA KUNA WATU WANAWEZA KUWA BADO HAI KUTOKANA NA MENEO WATAKAYOKUWA WAMEJIHIFAZI NDANI YA MELI HIYO KAMA HAYATAKUWA YAMEFIKIWA NA MAJI
(Picha na mpiga picha wetu)

WANAMICHEZO BORA WILAYA YA TEMEKE KUPEWA TUZO MAALUM!!

Mratibu wa Tuzo Richard Yalomba (Bob Rich) akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya utoaji wa tuzo kwa wanamichezo wa Temeke uliofanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni hivi karibuni.


Wanamichezo, Wasanii na wanamuziki mbalimbali waliowahi na wanaofanya vizuri mpaka sasa katika Wilaya ya Temeke wanatarajiwa kupewa Tuzo maalum hivi karibuni baada ya maandalizi ya sherehe za kutoa tuzo hizo kukamilika.


Akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya Tuzo hizo uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally Mratibu wa tamasha hilo Bw. Richard Yalomba (Bob Rich) amesema kila kitu kinakwenda vyema na mwitikio ni mkubwa sana kwa wakazi wa Temeke kuhusiana na utoazji wa tuzo hizo.


Amesema Mbunge wa Temeke Mh. Abbas Mtemvu naye yuko bega kwa bega na waandaaji ili kuhakikisha tuzo hizo zinatolewa kwa wanamichezo wake ambao anaamini wameiletea sifa kubwa Wilaya ya Temeke hivyo, wanafaa kukumbukwa na ni kitu muhimu kuwakumbuka kutokana na mchango wao kwa Jimbo la Temeke


Bob Rich amesema Hafla ya kutoa tuzo hizo imepangwa ifanyike Julai 30 2009 katika ukumbi utakaotangazwa baadae kutokana na maandalizi yanavyokwenda, mkutano huo, ulihudhuriwa na baadhi ya wanamichezo na wanamuziki kutoka wilayani humo waliohudhuria kikao hicho nia bondia Rashid Matumla, Mwakilishi wa mwanamuziki Bushoke, KR Mulla kutoka kundi la TMK Wanaume Family, Dansa wa siku nyingi Salum Makuka (Sammy Cool) Richard Yalomba (Bob Rich) Mwenyewe wambaye ndiyo mratibu na wengine wengi hata hivyo vikao vya maandalizi vinaendelea na blogu yako hii itaendelea kukuletea kila kinachatakiwa kujulikana kwa wadau wa michezo sanaa na muziki.

JAMANI WATANZANIA TUCHUKUENI TAHADHARI KABLA YA KUTOKEA KWA AJALI, ZITATUMALIZA!!

Moja ya Meli kubwa ya Mizigo KMM ikiingia katika Bandari ya Dar es alaam hivi karibuni, ni jambo la muhimu kuwa na usalama wa kutosha katika Bandari zetu kitu muhimu kwa vyombo vinavyohusika kuchukua tahadhari kabla ya ajali ili kuweza kukabiliana na matukio ya ajali, kama hii ambayo imetokea Zanzibar hivi sasa.

Habari kutoka katika eneo la ajali Baharini inayoihusisha Meli ya MV Fathi huko visiwani Zanzibar, zinasema mpaka sasa ni maiti tatu zimeopolewa na majina yao bado hayajatambuliwa huku kazi ya kuokoa miili ambayo bado imekwama katika meli hiyo ya mizigo ikiendelea.

Meli hiyo ilikuwa ikijiandaa kwenda Dar es alaam kutoka Zanzibar ikiwa na shehena ya mizigo mbalimbali na watu kadhaa, haijajulikana mpaka sasa ni watu wangapi wako ndani ya meli hiyo wakiwa hai, na ni wangapi wamekufa, bado tunaendelea kusubiri taarifa za vyombo vya usalama ili kujua sababu za kutokea kwa ajali hiyo na idadi ya watu waliokufa au kuokolewa pamoja na hasara ya mali, mara tutakapopata taarifa zaidi tutawaleteeni mara moja.

WADAU WA TWANGA PEPETA WAMSIKILIZA "MWANA DAR ES ALAAM" KABLA YA KUTOLEWA!!

Mtangazaji wa East Africa Television Mamaa Maimartha wa Jesse ndiye alikuwa msema chochote, hapa anaonekana akiongea maneno fulani kumkaribisha mkurugenzi wa Bendi ya African Staras Asha Baraka, ili kukaribisha wageni na kuwaambia chochote kutokana na maandalizi ya Albam hiyo ya yalivyokuwa na mafanikio yaliyofikiwa mpaka kuikia hatua hiyo ya kukamilisha albam ya (Mwana Dar es alaam) na matayarisho kwa ujumla kuhusiana na uzinduzi wake, unaotarajiwa kufanyika juni 5 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kimsingi nyimbo zilizomo kwenye albam hiyo zinaonekana kukubalika kwa watu wengi kutokana na umakini na utulivu sauti za wanamuziki na wa vyombo uliopo katika nyimbo hizo ikizisililiza tofauti na albam kadhaa zilizoopita mara hii inaonekana wazi kuwa kumefanyika kazi makini, heko wana Twanga wote FULLSHANGWE inawatakia maandalizi mema kwa ajili ya uzinduzi huo tutaendelea kupeana habari kadiri tutakavyozipata kuhusiana na uzinduzi huo.
Wanahabari walijimwaga vyakutosha katika Hafla hiyo hebu wacheki dada Khadija Khalili wa Gazeti la Tanzania Daima na dada Cecilia wa Radio Huhuru wakila pozi kwa mbali.

Waimbaji wa Bendi ya African Staras wakiimba wakati wa Hafla hiyo wakiongozwa na Rogati Hega (katapila) kulia akifuatiwa na mamaa Luiza Mbutu.

Kundi zima la wanenguaji wa African Staras Bend wana wa Kutwanga na kupepeta wakiwajibika jukwaani jana katika Hafla ya kusikiliza nyimbo zao mpya zilizopo kwenye albam yao mpya inayokwenda kwa jina la Mwana Dar es alaam iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick.

Yeye Aisha Madinda akawakamata vyema Mwimbaji wa muziki wa Taarab Mzee Yusuf wa Jahazi Molden Taarab na Mdoe wa Screen Master hapa hawachomoki hata kidogo.

Mnenguaji huyu wa Twanga akiwapepetea mashabiki kama unavyowaona wakimtazama kwa makini na kumpigia makofi.

Waigizaji wa Filamu wakavamia kwa nguvu zote kumbe kweli wanapenda muziki kuoka kulia ni Tino, Dr. Cheni, Kanumba, Ray, mwanamuziki Tid na rafiki yao ambaye hakufahamika mara moja wakijumuika na wana Twanga Pepeta katika hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Nanihii kushoto naye alikuwepo katika hafla hiyo iliyovuta watu maarufu wengi kulia ni Mpiganaji Deus Mhagale kutoka New Habari Cooparation akiwa ameshikilia Camera yake.
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Juma Pinto akiwa na rafiki yake.
Wafanyakazi wa Grobal Publishers wakiongozwa na Meneja wao Abdalla Mrisho aliyekaa katikati wakisikiliza kwa makini nyimbo za Albam Mpya ya bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) katika hafla ya kusikiliza nyimbo hizo kabla ya uzinduzi utakaofanyika Juni 5 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hafla hiyo imefanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick.

RSM Ashvir Launch at Kilimanjaro Kempinski!!

RSM Network in Africa and Chairman, RSM International Brian Eaton.

Group Photo of RSM Ashvir Directors and Staff

RSM Ashvir as we formally launch the admission of the firm as full member of RSM International, the 7th largest network of independent accounting and consulting firms. RSM Ashvir becomes only the third full member firm from Africa to be admitted to this growth network of independent professional services firms, often ranking within the top ten in their own locality, who are united by a common desire to provide the highest quality for services to clients.
RSM Ashvir was founded in Kenya in February 2004. Within a space of 5 years the firm has offices in Nairobi, Mombasa and Dar es Salaam with a apartner/director strength of 5 and a staff complement of over 65. At RSM Ashvir we work exceptionally hard to understand our clients’ needs, and in adherence with the firm’s motto “We Deliver”, provide perfect-fit solutions that will achieve their short and long-term ambitions.
In line with our vision which is to be a leading Pan-African professional services firm, with international affiliation, recognized for its ethics, values and professionalism with a strong culture of personalized and partner-led quality service, supported by investment in its human capital and technology, we have chosen RSM International as our network. RSM member firms share the same vision and value. This coupled with the strict quality control framework within which RSM member firm operate, will enable RSM Ashvir to serve its clients more effectively as they grow in within region and internationally.
RSM International has also developed various initiatives like the RSM Academy and the Centres of Excellence structure in each of the four main operating areas of audit, tax, risk assurance and transaction support. This will enable RSM Ashvir to work with regional team of experts who have the specialist knowledge to serve our clients specific needs. With its strong international language capability, effective global communication and resource sharing, RSM member firms maintain a strong position to service clients in diverse business sectors with a common brand the world-over.
We pay tribute to all our staff for the true dedication and unstinting commitment to upholding professional values and standards and to our clients and business associates for their trust and support without which this milestone would not have been possible.

Serengeti Breweries Launches ‘Wape Shavu Taifa Stars na Serengeti Premium Lager!!

Teddy mapunda left pr, media and communications manager with Nandi Mwiyombella Brand Manager addressing Press conference today during the launch a campaign ‘wape shavu Taifa stars kunywa Serengeti lager
May 27, 2008

Serengeti Breweries Launches ‘Wape Shavu Taifa Stars na Serengeti Premium Lager Campaign in Dar Es Salaam
Serengeti Breweries today, launched a campaign in Dar Es Salaam aimed at popularizing and supporting the National Team ‘Taifa Stars’ to Tanzanians ahead of the International friendly match with New Zealand National Team.
Speaking at the press conference today, SBL Public Relations, Media and Communications Manager Mrs Teddy Mapunda Said, that they will introduce road shows to encourage people to turn up in their numbers to support Taifa Stars. Akudo Impact Band will also be incorporated in the shows and culminate their performance during the match day.
Serengeti breweries, who are the main sponsors of the ‘Taifa Stars’ until 2011, will be using their branded truck for the campaign and will activate 6 big promotions which will go round the 3 districts, and all Dar Es Salaam Residents are invited to participate for the questions and answer session when the truck is around their area.
There will be a raffle draw for the people who will visit the truck and winners will get free entry tickets to this highly anticipated match. This campaign will run from tomorrow 29th May, 2009 till 2nd June, 2009.
On the day of the match, there will also be a Road show around the city of Dar es Salaam and the final destination will be outside the New National Stadium hyping up the match.
This campaign is launched for the first time in Dar Es Salaam and is the first of its kind in Tanzania in support of Taifa Stars. Serengeti Breweries wishes the team good luck and urge all the Tanzanians to support the team.
The match which will be played on the 03rd June, 2009 at the New National Stadium in Dar Es Salaam.


WATAKAOSHIRIKI MBIO ZA VODACOM DAR ES ALAAM MARATHON KUPIMWA AFYA JUNI 20!!

Meneja wa promosheni na matukio wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (katikati)akiongea na wanahabari juu ya upimaji wa afya katika maandalizi ya kushiriki mbio za Vodacom zitakazofanyika,Tarehe 20 mwezi ujao wanamichezo watapimwa Afya zao na Tarehe 21 wananchi wa kawaida wanaopenda kushiriki mbio hizo watapimwa Afya zao.(kushoto)katibu wa Afya Club Dr Deogratus Pissa,(kulia)Mwenyekiti wa chama cha riadha Dares Salaam Christin Malundi.

MORE GLAMOUR, INTRIGUE AND DRAMA ON M-NET AS TINSEL SEASON TWO LAUNCHES!

June 2009
With its refreshed Afro-centric lifestyle series STUDIO 53 returning to DStv screens recently, and following on its ever-growing investment in the African film and TV industry, M-NET is gearing up for the launch of season two of its glamourous soap opera TINSEL.

With season one running 65 episodes and screening twice a week on M-Net, season two will offer even more to DStv viewers. Now running an impressive 156 episodes, TINSEL will be screened three times a week, every Wednesday to Friday at 20.00 CAT from June 10.

M-Net’s Africa Director Biola Adekanbi says TINSEL remains a key part of M-Net’s plans in Africa and that season two is going to open a new chapter for the series.
“Traditionally soap opera as a TV genre takes longer to entrench because producers have to include a wide cast and multiple angles up front and then play these out over a course of time. This is why the first season of a soap opera is so important, to set up the storyline and the characters. With TINSEL this groundwork has been successfully built, so M-Net felt confident producing a second season. We always intended to invest significantly in TINSEL and the new season is set to provide great new plotlines and all the unexpected drama that make soap operas so attractive to audiences.”
Once again, the action returns to Reel Studios where veteran movie mogul Fred Ade-Williams is battling illness and the control of his empire, which remains under threat from ambitious business rival, Brenda Nana Mensah.
But with the secret now revealed that Brenda is in fact Fred’s daughter from a previous relationship, how will Fred cope with the pressure of the new situation. Will the blood that binds them together help them to find common ground?
Or will Brenda, in her role as boss of Odyssey Pictures, continue to push for her company’s success at the expense of her father’s legacy?
Meanwhile Fred’s charming playboy son turned film executive Philip Ade-Williams must be feeling the heat…
Always desperate to flee the boardroom will his new sister’s sudden appearance and her natural ease in business, a role that Fred always wanted for Philip, result in more family drama? Restless, ambitious and with penchant for the finer things in life, Philip’s unpredictability and unhappiness makes him a dangerous enemy.
And while the boardroom battles rage, even love is in the firing line…
Reginald Okoh, hot-shot executive at Reel Studios, now finds his marriage on the line as his deceptions catch up with him. His attorney wife Amaka, furious to discover her husband’s relationship with his secretary Angela, stormed out on him, but as season one ended with Reginald’s shooting, can trouble bridge the gap between them?

Or will his attraction to Angela prove too strong to ignore?
Adding to the tension, another ‘mole’ at Reel Studios is betraying the company, infiltrating the business and selling its secrets…but will they be discovered?
And who would be willing to risk everything to take on such a devious plan?
Plus, with the bullet destined for him hitting Reginald instead, will Ziggy’s troubles turn deadly? It’s all happening on TINSEL this season
Meanwhile, with season two of TINSEL well into production, Adekanbi has gone on to reveal that a great deal of time and resource has been invested into preparing for it.
Returning to TINSEL in season two are the talented cast – Victor Olaotan (Fred), Gideon Okeke (Philip), Omar Shariff Captan (Reginald), Uzo Egeeonu (Amaka), Matilda Obaseki (Angela), Chris Attoh (Kwame), Kunle Coker (Ziggy), Gbenro Ajibade (Soji), Iyke Okechukwu (Chuks) and Damilola Adegbite (Telema) and introducing Funlola Aofiyebi-Raimi as Brenda.
So get ready for TINSEL season two on M-Net every Wednesday, Thursday and Friday at 20:00 CAT. And for more information on the series or a sneak peek at what’s coming up in the next episode, log on to http://www.mnetafrica.com/

Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu vidole machoni na "Kizabi zabina"!

Kaka braza kakimbilia studio kufyatua wimbo mpya uliobeba jina la "Kizabi Zabina" si mtu Mwema! Kizabi zabina huyo alitajwa kwa jina la Mzee pazi, analalamikiwa na kiongozi wa bendi ya ngoma africa ras makunja kwa kuigombanisha jamii nakuwa sumu ndani jamii.
Wadaku walioshuhudia madongo makali yalikuwa yakirushwa na mwanamziki huyo katika studio huko ughaibuni.wamebaki midomo wazi kutokana na uzito wa madongo na hoja zilizojaa ukweli ukweli kuhusu "Kizabi Zabina" huyo aka Mzee Pazi.
Kiongozi wa Ngoma Africa Ras Makunja kamshitaki kwa jamii "Kizabi Zabina" kwa kosa la kuichonganisha jamii, tena kampa Shua kwa kumwambia "atafute la kufanya" na "kuwekeza muda mwingi katika maendeleo".
Watafiti wa mambo wanadai kuwa Ras makunja na kitu kipya hiko "Kizabi Zabina" kinaifanya bendi ya The Ngoma Africa yenye maskani ughaibuni kuonekana kuwa karibu sana na jamii ya Uswahilini kwa tungo zake ambazo mara nyingi zina elimisha,au kuishauri jamii ,wakati mwingine ni mwaliko wa malumbano ya hoja.

WASHIRIKI WA MISS VODACOM KIGAMBONI KATIKA PICHA YA PAMOJA!!

Hawa ndiyo warembo wanaotarajiwa kupanda jukwaani katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Miss Vodacom Kigamboni 2009 mwishoni mwa wiki hii hapa wakiwa katika mazoezi yao ya mwisho pale Sanaa Pub mtaa wa Ohio.

MABALOZI WAMTEMBELEA WAZIRI MARGARET SITTA!!

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe. Margaret Sitta akiwapokea baadhi ya Mabalozi waliomtembelea ofisini kwake leo.
Kikao kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe. Margaret Sitta na Mabalozi wa nchi za Ireland,Uingereza,Sweden,Denmark, Canada , Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na wawakilishi kutoka Mashirika ya Kimataifa ya UNFPA na UNIFEM . Katika kikao hicho Mhe. Waziri amewaeleza namna Wizara yake inavyotekeleza masuala mbalimbali yanayohusu Jinsia na Mikakati ya Wizara ya baadae.