JENGO LA PPF TOWER LANUSURIKA KULIPUKA MOTO ASUBUHI HII!!

Hii ni Sehemu ambayo ilipata hitilafu ya umeme katika jengo la PPF Tower mtaa wa Garden na Ohio ghorofa ya 15 kwenye ofisi za kampuni ya simu za mkononi Vodacom kitengo cha Fedha, sakata hilo limetokea asubuhi hii yapata kama saa tatu kasorobo hivi ambapo zilisikika kelele za mmoja wa wafanayakazi wa kampuni hiyo kuashiria moto, huku moshi mkubwa ukitanda katika ofisi hiyo, kitu kilichawafanya wafanyakazi wengine kuanza kutimua mbio wakishuka chini ya jengo na kutoka nje, hata hivyo walifanya mawasiliano na kikosi cha zimamoto kutoka kampuni ya knight Surport ambao waliwahi katika eneo la tukio na kudhibiti hali hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa kikosi cha zimamoto kutoka kampuni hiyo Bw. Glad Billy Moyo amesema "ulikuwa mlipuko mdogo uliotokea kwenye Tubelight (Taa)ya moja ya vyumba vya jengo hilo ghorofa ya 15, na kusababisha moshi mkubwa uliwashtua wafanayakazi wengi waliokuwemo katika jengo hilo, hata hivyo Glad amesema hakuna madhara yoyote yaliyotokea na moto umedhibitiwa hivyo watu wanaweza kuendelea na shughuli zao kama kawaida
Wafanyakazi wa kikosi cha kuzima cha kampuni ya Knight Surport wakiwa katika picha ya pamoja katika ghorofa ya 15 ya jengo hilo mara baada ya kukamilisha zoezi la kudhibiti moto huo.

Magari ya kampuni ya kikosi cha kuzima moto cha Knight Surport yakiwa yameegeshwa chini ya jengo hilo tayari kwa kukabiliana na moto huo leo asubuhi huku watu mbalimbali wanaofanya kazi katika makampuni yaliyopanga kwenye jengo hilo wakiwa nje ya jengo kusubiri hatma ya moto huo.

Jengo la PPF Tower kamalinavyoonekana leo asubuhi lilinusurika kulipuka moto baada ya hitilafu kutokea katika ghorofa ya 15 leo asubuhi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment