VIDEO ZA BABY MADAHA NA FEISAL ISMAIL ZAFUNIKA, ZAANZA KUUZWA MADUKANI!!

Nilesh Bhatt mkurugenzi wa uzalishaji wa kampuni ya Pilipili Entertainment akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa kampuni hiyo na Video mbili za wanamuziki Feisal Ismail na Baby Madaha uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana.
Bw. Nilesh Bhatt Amesema kuwa Albam hizi zimerekodiwa katika kiwango cha hali ya juu kwa kushirikisha wasani wengine kamaPancho Latino Chid Benzi, Nura, Mr. Blue na Feri Kano, ambapo albam ya Baby Madaha inalenga katika Mapenzi na Albam ya Feisal inalenga katika mambo ya kutumaini mafanikio, ameongeza kuwa wimbo wa Baby Madaha unafundisha kwa kiwango kikubwa, kwani zaidi ya miaka 50 iliyopita Utamaduni wa India ulikuwa umejifunga sana lakini kwa sasa unaanza kufunguka na kuingiliana na tamaduni nyingine nyingi, hivyo mabadiliko yataanza kutokea kadiri siku zinavyoenda na nyimbo hii ya Baby hakika itakuwa ni Fundisho zuri kwa jamii za watu wa nchi zote mbili yaani India na Tanzania.
Waziri wa Viwanda na Biashara mama Marry Nagu akionyesha video ya Feisal Ismail mara baada ya kuizindua rasmi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana ambapo pia aliizindua kampuni ya Pilipili Entertainment iliyotengeneza Video za wanamuziki hao nchini India kushoto ni Nilesh Bhatt mkurugenzi wa uzalishaji kampuni ya Pilipili.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika akionyesha Video ya Baby Madaha mara baada ya kuizindua rasmi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kushoto ni mkurugenzi wa uzalishaji kampuni ya Pilipili Entertainment Nilesh Bhatt.

Mkurugenzi na Mbunifu wa mavazi kutoka kampuni ya Carpuany and Design Mamaa Grace Sinamwita kulia akipozi katika picha na Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Ritah Paulsen wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Pilipili Entertainment uliofanyika jana sambamba na uzinduzi wa Video mbili za wanamuziki Baby Madaha na Faisal Ismail kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

Meneja mkuu wa Vituo vya Radio na Televisheni vya East Fm, Nairobi Star, Classic 105 na Kiss Fm kutoka Nairobi nchini kenya Martin Khafafa akizungumza katika uzinduzi wa Video za wanamuziki wawili Feisal na Baby Madaha uliofanyika jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kulia ni mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Fm na miliki wa kikundi cha muziki cha THT Ruge Mutahaba.

Wakurugenzi, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Pilipili Entertainment wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Kampuni hiyo na video mbili za Baby Madaha na Feisal kufanyika jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

Kutoka kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, Mwanamuziki Feisal Ismail maadam Ritah Paulsen Mkurugenzi wa Benchimark Production kampuni, ambayo pia inaandaa Bongo Star Search na Waziri wa Viwanda na Biashara mama Marry Nagu wakiwa katika picha ya pamoja, Feisal aliibuliwa na Bongo Star Search mpaka hapo alipofikia katika mafanikio yake.
Feisal Ismail naye akifanya vitu vyake jukwaani.

Baby Madaha akithibitisha ubora wake jukwaani wakati wa Uzinduzi wa Video yake .

Burudani kwa kwenda mbele

Dada Agricola Kossey kutoka shirika la Save Albino Tanzania hakutaka kukosa kile kilichofanywa na wanamuziki Feisal Ismail na Baby Madaha kama unavyomuona katika picha akiwa makini ili kuona ubora wa Video Hizo.

Hawa ndiyo waliowezesha shughuli hii nzima kushoto ni Sophia Mdecha Meneja Matukio wa Pilipili Entertainment na Simbiso Machine Meneja uhusiano wa Kampuni hiyo wakipozi kwa picha, mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa Video hizo sambamba na Kampuni ya Pilipili kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana.

Wataalamu hawa wa kuchanganya picha nao walikuwa bize kwelikweli ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa hebu wacheki mdau.

Mh. Marry Nagu Waziri wa Viwanda na Biashara kulia Mh. George Mkuchika Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo katikati na mwanamuziki Feisal Ismail wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi huo, hii ni dalili kuwa viongozi hao wa kitaifa wamevutiwa sana na kijana Feisal kutokana na kazi yake nzuri itakayomtangaza vyema yeye binafsi na Tanzania kwa ujumla katika Anga za muziki.
Miss Tanzania 2007 Richa Adhia na mama yake Maria Adia kulia wakipozi katika picha wakati wa uzinduzi wa Video mbili za wanamuziki Baby Madaha na Feisal Ismail kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jana usiku

Hili ni Jopo la waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifutilia uzinduzi huo ili kujua kila kilichojiri wakiwa tayari kuupasha umma juu ya uzinduzi huo.

Baadi ya washabiki na wapenzi mbalimbali wa muziki wakifuatilia matukio ya uzinduzi huo.

Kaka Rwaga na Maiwaifu wake Dina nao hawakutaka kukosa uzinduzi huo uliokuwa wa kukata na shoka kama unavyoona matukio katika picha mdau.

Mamaa Frolence akiwa na rafiki yake Annet kati na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania wakifuatilia Yason Mashaka kwa karibu kila kilichoendelea katika uzinduzi wa Video mbili za wasanii Baby Madaha na Feisal Ismail jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment