Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu vidole machoni na "Kizabi zabina"!

Kaka braza kakimbilia studio kufyatua wimbo mpya uliobeba jina la "Kizabi Zabina" si mtu Mwema! Kizabi zabina huyo alitajwa kwa jina la Mzee pazi, analalamikiwa na kiongozi wa bendi ya ngoma africa ras makunja kwa kuigombanisha jamii nakuwa sumu ndani jamii.
Wadaku walioshuhudia madongo makali yalikuwa yakirushwa na mwanamziki huyo katika studio huko ughaibuni.wamebaki midomo wazi kutokana na uzito wa madongo na hoja zilizojaa ukweli ukweli kuhusu "Kizabi Zabina" huyo aka Mzee Pazi.
Kiongozi wa Ngoma Africa Ras Makunja kamshitaki kwa jamii "Kizabi Zabina" kwa kosa la kuichonganisha jamii, tena kampa Shua kwa kumwambia "atafute la kufanya" na "kuwekeza muda mwingi katika maendeleo".
Watafiti wa mambo wanadai kuwa Ras makunja na kitu kipya hiko "Kizabi Zabina" kinaifanya bendi ya The Ngoma Africa yenye maskani ughaibuni kuonekana kuwa karibu sana na jamii ya Uswahilini kwa tungo zake ambazo mara nyingi zina elimisha,au kuishauri jamii ,wakati mwingine ni mwaliko wa malumbano ya hoja.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment