WANAMICHEZO BORA WILAYA YA TEMEKE KUPEWA TUZO MAALUM!!

Mratibu wa Tuzo Richard Yalomba (Bob Rich) akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya utoaji wa tuzo kwa wanamichezo wa Temeke uliofanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni hivi karibuni.


Wanamichezo, Wasanii na wanamuziki mbalimbali waliowahi na wanaofanya vizuri mpaka sasa katika Wilaya ya Temeke wanatarajiwa kupewa Tuzo maalum hivi karibuni baada ya maandalizi ya sherehe za kutoa tuzo hizo kukamilika.


Akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya Tuzo hizo uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally Mratibu wa tamasha hilo Bw. Richard Yalomba (Bob Rich) amesema kila kitu kinakwenda vyema na mwitikio ni mkubwa sana kwa wakazi wa Temeke kuhusiana na utoazji wa tuzo hizo.


Amesema Mbunge wa Temeke Mh. Abbas Mtemvu naye yuko bega kwa bega na waandaaji ili kuhakikisha tuzo hizo zinatolewa kwa wanamichezo wake ambao anaamini wameiletea sifa kubwa Wilaya ya Temeke hivyo, wanafaa kukumbukwa na ni kitu muhimu kuwakumbuka kutokana na mchango wao kwa Jimbo la Temeke


Bob Rich amesema Hafla ya kutoa tuzo hizo imepangwa ifanyike Julai 30 2009 katika ukumbi utakaotangazwa baadae kutokana na maandalizi yanavyokwenda, mkutano huo, ulihudhuriwa na baadhi ya wanamichezo na wanamuziki kutoka wilayani humo waliohudhuria kikao hicho nia bondia Rashid Matumla, Mwakilishi wa mwanamuziki Bushoke, KR Mulla kutoka kundi la TMK Wanaume Family, Dansa wa siku nyingi Salum Makuka (Sammy Cool) Richard Yalomba (Bob Rich) Mwenyewe wambaye ndiyo mratibu na wengine wengi hata hivyo vikao vya maandalizi vinaendelea na blogu yako hii itaendelea kukuletea kila kinachatakiwa kujulikana kwa wadau wa michezo sanaa na muziki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment