WADAU WA TWANGA PEPETA WAMSIKILIZA "MWANA DAR ES ALAAM" KABLA YA KUTOLEWA!!

Mtangazaji wa East Africa Television Mamaa Maimartha wa Jesse ndiye alikuwa msema chochote, hapa anaonekana akiongea maneno fulani kumkaribisha mkurugenzi wa Bendi ya African Staras Asha Baraka, ili kukaribisha wageni na kuwaambia chochote kutokana na maandalizi ya Albam hiyo ya yalivyokuwa na mafanikio yaliyofikiwa mpaka kuikia hatua hiyo ya kukamilisha albam ya (Mwana Dar es alaam) na matayarisho kwa ujumla kuhusiana na uzinduzi wake, unaotarajiwa kufanyika juni 5 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kimsingi nyimbo zilizomo kwenye albam hiyo zinaonekana kukubalika kwa watu wengi kutokana na umakini na utulivu sauti za wanamuziki na wa vyombo uliopo katika nyimbo hizo ikizisililiza tofauti na albam kadhaa zilizoopita mara hii inaonekana wazi kuwa kumefanyika kazi makini, heko wana Twanga wote FULLSHANGWE inawatakia maandalizi mema kwa ajili ya uzinduzi huo tutaendelea kupeana habari kadiri tutakavyozipata kuhusiana na uzinduzi huo.
Wanahabari walijimwaga vyakutosha katika Hafla hiyo hebu wacheki dada Khadija Khalili wa Gazeti la Tanzania Daima na dada Cecilia wa Radio Huhuru wakila pozi kwa mbali.

Waimbaji wa Bendi ya African Staras wakiimba wakati wa Hafla hiyo wakiongozwa na Rogati Hega (katapila) kulia akifuatiwa na mamaa Luiza Mbutu.

Kundi zima la wanenguaji wa African Staras Bend wana wa Kutwanga na kupepeta wakiwajibika jukwaani jana katika Hafla ya kusikiliza nyimbo zao mpya zilizopo kwenye albam yao mpya inayokwenda kwa jina la Mwana Dar es alaam iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick.

Yeye Aisha Madinda akawakamata vyema Mwimbaji wa muziki wa Taarab Mzee Yusuf wa Jahazi Molden Taarab na Mdoe wa Screen Master hapa hawachomoki hata kidogo.

Mnenguaji huyu wa Twanga akiwapepetea mashabiki kama unavyowaona wakimtazama kwa makini na kumpigia makofi.

Waigizaji wa Filamu wakavamia kwa nguvu zote kumbe kweli wanapenda muziki kuoka kulia ni Tino, Dr. Cheni, Kanumba, Ray, mwanamuziki Tid na rafiki yao ambaye hakufahamika mara moja wakijumuika na wana Twanga Pepeta katika hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Nanihii kushoto naye alikuwepo katika hafla hiyo iliyovuta watu maarufu wengi kulia ni Mpiganaji Deus Mhagale kutoka New Habari Cooparation akiwa ameshikilia Camera yake.
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Juma Pinto akiwa na rafiki yake.
Wafanyakazi wa Grobal Publishers wakiongozwa na Meneja wao Abdalla Mrisho aliyekaa katikati wakisikiliza kwa makini nyimbo za Albam Mpya ya bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) katika hafla ya kusikiliza nyimbo hizo kabla ya uzinduzi utakaofanyika Juni 5 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hafla hiyo imefanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment