Afisa biashara mkuu wa Benki ya NMB Bw.Bans Nierop akipiga mpira huku katibu mkuu wa TFF akiangali kama ishara ya uzinduzi wa awamu ya tatu katika programu ya kuendeleza watoto kwa mpira wa miguu benki hiyo pia ilikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa shirikisho la mpira wa miguu TFF uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Gymkana jijini jana
\\ Meneja masoko wa benki ya NMB Bw. Imani Kajula akiwa ameshika mpira pamoja na watoto mara baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa kwa Shirikisho la mpira TFF kwa ajili ya programu ya awamu ya tatu ya kuendeleza mpira kwa watoto wadogo katika Viwanja vya Gymkana Jana


AKUDO IMPACT YAPAGAISHA UZINDUZI WA WIKI YA USALAMA BARABARANI

Waimbaji wa bendi ya Akudo Impack wakicheza wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani mjini Morogoro Jumapili. Zain ilichangia zaidi ya sh. milioni 30 Wiki ya Usalama Barabarani na kupewa tuzo na kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani.



Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impack wakiwajibika wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani mjini Morogoro Jumapili. Zain ilichangia zaidi ya sh. milioni 30 Wiki ya Usalama Barabarani na kupewa tuzo na kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani.

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAANDAMANA!!

Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakiandamana leo asubuhi kutoka mtaa wa Rugoda hadi ofisi za Wizara ya Habari na Utamaduni inayoongozwa na waziri George Mkuchika, huku wakiwa wamefunga midomo yao na plasta kupinga kitendo cha serikali kulifungia kwa muda wa miezi mitatu Gazeti la Mwanahalisi na kushinikiza serikali irekebishe sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 1976 ili kuleta uhuru kamili kwa vyombo vya habari.

YANGA YASHINDA BAO MOJA LAKINI YAPELEKWA MZOBEMZOBE!!!

Kivutio kikubwa kwa mashabiki katika mechi hiyo ya watani wa jadi Simba na Yanga ilikuwa Mechi ya utangulizi iliyochezwa kati ya timu ya Wabunge na timu ya Maalbino ambapo waheshimiwa wabunge waliisambaratisha timu ya maalbino magoli mawili kwa Nunge kama anavyoonekana mbunge wa Mkuranga na naibu waziri wa Nishati na Madini Mh. Adam Malima wa timu ya wabunge akimtoka mchezaji wa timu ya Maalbino Sefu Urati kwenda kumuona kipa.
Mashabiki wa Simba wakiipa tafu timu yao katika mpambano huo.

Mashabiki wa Yanga wakishangilia kwa nguvu katika mpambano huo ambao Yanga ilishinda kwa Goli moja lililofungwa na mashambuliaji Ben Mwalala akipokea pasi ya Mchezaji mahiri wa Yanga Boniface Ambani hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kuifunga Simba baada ya kunyanyaswa kwa miaka nane

Kikosi cha Yanga.

Kikosi cha timu ya simba kilichopambana na Yanga Jana kwenye uwanja mkuu wa Taifa.

ILIKUWA NI FULL KUJIRAMBA TU MJI KASORO BAHARI!!

Mzee wa vina Profesa J akiwapagaisha mashabiki katika moja ya maonyesho ya fiesta na wiki hii limefanyika onyesho kabambe mkoani morogoro ambalo lilishirikisha wasnii kibao yaani ilikuwa full kujiramba tu

Ray C. na kiuno chake laini akipagawisha mashabiki.

Q. Chilla kama kawaida yake akiimba na mmoja wa waimbaji mahri wa kundi la THT
THT wakifvitu vyao jukwaani




SHINDANO LA RAFDA LAFANA KILIMANJARO KEMPISKI!!

Hatimaye mshindi Saidi Tambwe alipatikana jana 24/10/2008 ambaye ni mbunifu kutoka mkoani Mwanza ilikuwa nguo ya ajabu kwangu nimeshuhudia wabunifu wengi wakibuni mavazi lakini hili la Saidi Tambwe kweli amejitahidi na nafikiri anaweza kuwa mwakilishi mzuri kwa nchi yetu katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Botswana hapo baadae

mwaka huu
Burudani za ngoma za asili pia zilikonga nyoyo za watazamaji.




Mamodo walipita jukwaani na nguo za wabunifu mbalimbali na kila mbunifu alijitahidi kuonyesha nguo nzuri ili nguo yake iweze kushinda.

Hiki kilikuwa kivazi matata na cha kuvutia kilitia fora

Warembo wengi walijitokeza kwakweli lilikuwa ni shindano matata sana na Redds wanastahili kupongezwa kwa maandalizi mazuri katika shindano hilo

Banana Zoro kushoto na baba yake mzee Zahir Ally Zoro katikati na Siz Q kutoka B. Band walikuwepo katika kuburudisha wageni mbalimbali na wapenzi mambo ya mitindo

Meneja wa kinywaji Cha Redds ambao ndiyo wandaaji wakuu wa RAFDA Bw. George Kavishe akizungumza na Irene Kiwia katika kuweka mambo sawa kabla ya kuanza kwa shindano hilo.

Hatuwezi kuikosa Rafda!!

Agrey Mareale mkurugenzi wa Executive Solution Prashant Patel, Ramesh Shah Richa Adhia na Mrs Agrey Mareale

Abby akihojiana na Max kushoto na Willy

Kamati ya Miss Tanzania ilikuwepo pia kutoka kulia ni Afisa uhusiano wa kamati hiyo Rico, Ramesh Shah jaji mkuu, mkuu wa itifaki Arbert Makoye, Miss Tanzania 2007Richa Adhia Mwenyekiti wa kamati hiyo Prashant Patel na jackson Kalikumtima Mkurugenzi Hashim Lundenga anachungulia kwa mbali nyuma.

Wabunifu wa mavazi kutoka kulia niFatma Amour,Asia Idalus na Farha wa Fnaaz Designer.

Meneja masoko wa Zain Kelvin Twisa kutoka kushoto Khadija Mwanamboka Irene Kiwia na mbunifu wa mavazi kutoka Zanzibar Farouque Abdela wakizungumza.

Mwanamuziki Jaquiline Ntuyabaliwe kushoto Abby wa Chanel 5 na Sophia Byanaku

Hawa nao hawakutaka kukosa fainali hizo.

















ODEMBA ATABIRIWA KUFANYA VYEMA MISS EARTH 2008!!

Tovuti kubwa na maarufu inayoshughulika na masuala ya urembo ya Global ya Beauties imeonyesha utabiri kuwa katika mashindano hayo ya Miss Earth 2008 yanayofanyika jijini Mannila ncini Philipines ambayo jumla ya warembo 90 watashiriki inaonyesha katika utabiri huo kuwa mrembo wa Tanzania Miriam Odemba anaweza kufanya vyema kutokana na nafasi aliyowekwa lakini pia Afrika inaweza kufanya vyema kutokana na warembo wengine kutoka Botswana na Sudan ya kusini kwa habari zaidi tembelea http://www.globalbeauties.com

/earth/2008/e08_tree.htm).

TIMU YA MAALBINO YAPANIA KUWASAMBARATISHA WABUNGE KABLA YA MPAMBANO WA WATANI WA JADI!!

Mpambano utakaofanyika kabla ya mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga katika uwanja mkuu wa Taifa kati ya timu ya Maalbino na Wabunge wa Jmhuri ya muungano wa Tanzania nao umezidi kuwa mkali baada ya kampuni ya (Sumsung) chini ya Freedom Electronics kumwaga vifaa mbalimbali kwa ajili ya mchezo huo wapenzi na mshabiki wa mpira wa miguu kaeni mkao wa kufurahi kutokana na jinsi timu ya Maalbino ilivyopania kuisambaratisha timu ya waheshimiwa Wabunge, kutoka kushoto ni Sefu Urati mwenyekiti wa chama cha maalbino Ilala, Mhamed Chenzi mwenyekiti mkoa, Oscar na David Joseph kutoka kampuni ya Freedom Electronics


Homa ya watani wa jadi yazidi kupanda lakini nayo maandalizi ya mpambano wa timu ya Maalbino na wabunge wazidi kuwa mkali.


BARRICK YADHAMINI TAIFA GOLD CUP KWA MILIONI 63.5!!

Afisa uhusiano wa kampuni ya Barrick Teweli Teweli kushoto akikabidhi mfano wa hundi ya Fedha shilingi milioni 63.5000.000 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa shirikisho la mpira wa kikapu TBF kama udhamini wa mashindano ya TAIFA GOLD CUP yanayotarajiwa kuanza oktoba 26 mwaka huu jijini katika uwanja wa Taifa wa ndani




Hapa akikabidhi baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi katika mashindano hayo.



Afisa uhusiano wa kampuni ya Barrick Teweli Teweli akikabidhi jezi za kuchezea kwa katibu mkuu wa TBF Lawrence Gedion Cheyo.


Ofisa kutoka kampuni ya Silver Bullet Kim Matinyi kushoto akisalimiana na afisa uhusiano wa kampuni ya Barrick Tewel Teweli mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo masaki jijini leo 24/10/2008


Kampuni ya uchimbaji wa madini Barrick leo imetangaza udhamini kwa mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama TAIFA GOLD CUP yanayotarajiwa kuanza 26 Oktoba jumapili hadi 1 Novemba 2008 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar.

Akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari Afisa habari wa kampuni hiyo Tewel Teweli amesema jumla ya udhamini huo ni kiasi cha fedha shilingi milioni 63.5000.000/= ambazo zimegawanywa katika makundi sita ikiwa ni kulipia malazi na chakula kwa timu zote 24.000.000/=, vifaa vya michezo 15.000.000/=, Fulana na Kofia 6.5000.000/=, medali 1.5000.000/=, matangazo 10.000.000n na utawala na shughuli zingine za kiofisi ni shilingi 6.000.000/=.
Teweli amesema kampuni hiyo imeongeza udhamini kwa asilimia kumi na mbili ukilinganisha na mwaka jana ambapo TBF ilidhaminiwa kwa milioni 50.000.000 ili kuandaa mashindano hayo, ameongeza kuwa mwaka huu timu zimeongezeka na kuwa 22 tofauti na mwaka jana ambapo zilikuwa chini ya hapo.

Ameongeza kuwa michezo hiyo itazinduliwa kesho kwa moja ya timu za Dar es alaam kucheza na timu itakayochaguliwa kutoka miongoni mwa timu zilizotoka mikoani na mgeni wa heshima atakuwa Mh. Jaji Mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhani.

Naye katibu mkuu wa TBF Taifa Bw. Lawrence Gedion Cheyo ameishukuru kampuni ya Barrick kwa udhamini huo na kwamba utayafanya mashindano hayo ya TAIFA GOLD CUP kuwa na hadhi ya kimataifa zaidi na tunaweza kupata wachezaji wenye viwango vitakavyotusaidia kupata wachezaji wazuri zaidi.

ZAIN YACHEZESHA DROO YA MUDA WA MAONGEZI!

Balozi wa Zain Muhidin Issa Michuzi akibofya kitufe cha kompyuta katika droo ya muda wa maongezi iliyochezeshwa leo 23/10/2008 makao makuu ya kampuni hiyo kijitonyama anayefuata ni Abadalla Ahmed kutoka bodi ya kusimamia michezo ya bahati nasibu ya taifa katikati ni meneja masoko wa kampuni hiyo Kelvin Twisa na mwisho ni afisa uhusiano Celina Njuju picha kwa hisani ya Michuzi.blogspot.com.

TUENDELEZE LIBENEKE LA BURUDANI SIYO KUTUNISHIANA MISULI JAMANI!!



Wapenzi wadau wa michezo na burudani jumapili iliyopita Pale Leaders Club kulitokea msuguano kidogo kati ya timu ya Namanga na Mango wakati wa mechi yao rapsha zilizomfanya refa wa mchezo huo kupiga filimbi ili kukatisha mchezo huo.
Jamani mimi mzee wa FLLSHANGWE ningependa kuwashauri hawa ndugu zangu kuwa Bonanza ni mahali pa kukutana watu tofauti marafiki wapenzi wa burudani na kufanya mazoezi pamoja na kushauriana mambo mbalimbali ya maendeleo lakini pia kusaidiana katika matatizo kwa hiyo pasiwe mahali pa kutunishiana misuli ndugu zangu sisi wote ni wamoja ndiyo maana tunaongea lugha moja yaani kiswahili FULLSHANGWE tunasema tunawapenda wote na tunawatakia maisha mema ili tuendeleze libeneke la burudani.

JAMANI ETI BONGO HAKUNA WEEKEND MANAKE WATU NI FULL KUJIRAMBA TU IWE JUMATATU JUMANNE YAANI KILA SIKU!!

Aah! na huyu blaza vipi mbona anajishebedua hivi eeh!, tuyaache wadau manake kila mtu anajipa raha na kujiramba kwa raha zake ndiyo mambo ya burudani hayo




" Pinda mugongo pinda mugongo pinda mugongo"



" Nikicheza hivi lazima wapandishe mzuka wa Shangwe tu"


" Hapa unaonaje hii staili kali sasa nimeitoa Ughaibuni"

HIYO NDIYO NGWASUMA YA NZOMBOLO NA MATEMBELE

Queen Aliya wa FM ACADEMIA BAND akifanya makeke

"mwanamke cheni kiunoni si unaona mwenyewe"


Jamani mnaonaje hapa nawapa raha eeh!!


M-NET BIG BROTHER AFRICA 3 – Day 57 (October 20, 2008).






A surprise visitor for M-Net’s Big Brother Africa housemates as Johan from Big Brother Finland enters the Big Brother Africa. Meanwhile Zimbabwean Big Brother Africa housemate Munya has headed off to Finland in an exciting swap between the two houses. Audiences can tune in to Big Brother Africa 24/7 live, on DStv channel 198 or catch the daily shows on M-Net. For more information, to vote or to post your comments on the show, log on to
www.mnetafrica.com/bigbrother
.