BARRICK YADHAMINI TAIFA GOLD CUP KWA MILIONI 63.5!!

Afisa uhusiano wa kampuni ya Barrick Teweli Teweli kushoto akikabidhi mfano wa hundi ya Fedha shilingi milioni 63.5000.000 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa shirikisho la mpira wa kikapu TBF kama udhamini wa mashindano ya TAIFA GOLD CUP yanayotarajiwa kuanza oktoba 26 mwaka huu jijini katika uwanja wa Taifa wa ndani




Hapa akikabidhi baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi katika mashindano hayo.



Afisa uhusiano wa kampuni ya Barrick Teweli Teweli akikabidhi jezi za kuchezea kwa katibu mkuu wa TBF Lawrence Gedion Cheyo.


Ofisa kutoka kampuni ya Silver Bullet Kim Matinyi kushoto akisalimiana na afisa uhusiano wa kampuni ya Barrick Tewel Teweli mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo masaki jijini leo 24/10/2008


Kampuni ya uchimbaji wa madini Barrick leo imetangaza udhamini kwa mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama TAIFA GOLD CUP yanayotarajiwa kuanza 26 Oktoba jumapili hadi 1 Novemba 2008 katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar.

Akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari Afisa habari wa kampuni hiyo Tewel Teweli amesema jumla ya udhamini huo ni kiasi cha fedha shilingi milioni 63.5000.000/= ambazo zimegawanywa katika makundi sita ikiwa ni kulipia malazi na chakula kwa timu zote 24.000.000/=, vifaa vya michezo 15.000.000/=, Fulana na Kofia 6.5000.000/=, medali 1.5000.000/=, matangazo 10.000.000n na utawala na shughuli zingine za kiofisi ni shilingi 6.000.000/=.
Teweli amesema kampuni hiyo imeongeza udhamini kwa asilimia kumi na mbili ukilinganisha na mwaka jana ambapo TBF ilidhaminiwa kwa milioni 50.000.000 ili kuandaa mashindano hayo, ameongeza kuwa mwaka huu timu zimeongezeka na kuwa 22 tofauti na mwaka jana ambapo zilikuwa chini ya hapo.

Ameongeza kuwa michezo hiyo itazinduliwa kesho kwa moja ya timu za Dar es alaam kucheza na timu itakayochaguliwa kutoka miongoni mwa timu zilizotoka mikoani na mgeni wa heshima atakuwa Mh. Jaji Mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhani.

Naye katibu mkuu wa TBF Taifa Bw. Lawrence Gedion Cheyo ameishukuru kampuni ya Barrick kwa udhamini huo na kwamba utayafanya mashindano hayo ya TAIFA GOLD CUP kuwa na hadhi ya kimataifa zaidi na tunaweza kupata wachezaji wenye viwango vitakavyotusaidia kupata wachezaji wazuri zaidi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment