Nokia yatoa toleo jipya lenye maudhui ya mfungo wa ramadhani



Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam


Nokia imetangaza kuzindua mfumo mpya kwenye simu wenye maudhui ya kuridhisha kwa wakenya maalumu katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaotarajia kuanza hivi karibuni. Toleo hilo ni jipya la maudhui ya mfungo wa Ramadhan 2010,ambapo simu zimeongezewa mambo muhimu ya mwezi mtukufu na yanapatikana kwenye Ovi, moja ya mfumo maarufu wa Nokia utakaoweza sasa kuupata kutumia simu ya nokia bure Mkuu wa kitengo cha mauzo Afrika Mashariki na kusini Bwana Kenneth Oyolla alisema, sasa watumiaji wa simu za Nokia ni wamoja na itakuwa rahisi kwao kupata maudhui na ujuzi ambao waislamu wengi wangependa kuupata ili uwaweke karibu zaidi na mwezi huu mtukufu.







Tumeshuhudia ongezeko kubwa la mahitaji kwa Wakenya na tunatarajia majibu kutoka kwa watumiaji watakapotumia mfumo huu mpya haswa kwa ndugu zetu waislam wanaoingia kwenye mwezi huu mtukufu.” Mfumo huo wa Ramadhan una wasifu pamoja na Quran tukufu, muda wa kuswali na hadithi za Mtume.








Quran tukufu imejumuisha maandiko ya Quran kutoka kwenye simulizi mbali ambapo watumiaji wataweza kuchagua katika mfumo wa MP3 na pia itatoa muongozo wa Qibla, inayotolewa kwa maeneo 1000 katika nchi 200, pia utaweza kuiingiza kwenye simu yako, kuitoa, kuisahihisha au kuongeza eneo lolote kwa kutumia GPS.







“Mfumo wa mwaka huu utawezesha simu za Nokia zikiwamo za kugusa na kuandika zote zinapatikana kwa lugha mbalimbali. Tunayofuraha kutoa mfumo huu katika kipindi hiki”, alisema Bwana Oyolla. “Hiki ni kipindi maalumu kwetu na tumejidhatiti kuhakikisha kwamba tunatoa suluhisho litakalokidhi mahitaji. Mfumo huu wa Ramadhani 2010 ni bure na unatoa ridhaa mbalimbali kutoka kwa watoaji wakimataifa na kitaifa na itapatikana kwa kupitia simu mbalimbali,” aliongeza Bwana Oyolla.






Bwana Oyolla alisema mfumo huo maalum kwa ajili ya Ramadhani 2010 umeunganishwa na simu za Nokia ambazo ni pamoja na Nokia N97 mini, Nokia E72, Nokia E52, Nokia X6, Nokia 5230,Nokia 5530,Nokia C5,Nokia 5235, Nokia 5800, Nokia E5, Nokia 6700 slide, Nokia 5233, Nokia X3, Nokia 6303i, Nokia 2710, na Nokia C3. Pia unapatikana kwa lugha ya Kiingereza, Kiarabu, Farsi, Kifaransa na Urdu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment