Mzee wa "aladji aladji" kuwasha moto Bilicanas Club leo.



Baada ya kuzikonga nyoyo za wapenzi wa lile songi lililobamba sana hapa bongo la Alaji Alaji,ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 ndani ya viwanja vya Lidaz Club,kutoka kwa mwanamuziki wa Ivory Coast Jeff Bogolabang, leo usiku atalitikisa tena goma la alaji alaji ndani ya Bilicanas Club (Much More) kwenye uzinduzi wa Clouds Tv kujumuisha vipindi na muziki kutoka kituo cha MTV BASE.


Katika uzinduzi huo utakaokuwa na msisimko mkubwa kwa wadau wa mambo ya muziki na burudani ,utapambwa na wasanii wengine wa hapa nyumbani na pia kutoka kwa wale watani zetu wa jadi kutakuwepo na wale wakali wa kusugua sugua sahani CODERED DJ'S,ambao pia walifamya makamuzi ya kiaina ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse.


Aidha katika taarifa iliyotolewa na Clouds TV/MTV BASE,imeeleza kuwa kuanzia agasti 10 2010,watazamaji wa Clouds TV watapata nafasi ya kuburudishwa kwa masaa mawili ya vipindi vya muziki na mitindo ya maisha kutoka katika kituo cha televisheni cha Kimataifa,kinachorusha matangazo yake Afrika pekee cha MTV BASE.Burudani hiyo itarushwa hewani jumatatu hadi jumapili kati ya saa 12 jioni na saa 1 usiku,na vile vile kukiwa na mwendelezo wa burudani kati ya saa 4 na saa 5 usiku kwa siku za wiki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment