Kamanda mpya wa Vijana CCM Tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele Nyerere, akiongea na wana CCM. mara baada ya kutawazwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa kata hiyo leo kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za tawi hilo na kuhudhuriwa na wanachama wa chama hicho, pamoja na marafiki wa msanii huo anayeigiza sauti za viongozi.
"Steve Nyerere" amewashukuru marafiki zake, wazee wake mtaani, mama zake pamoja na mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Ritah. ambaye amemtania kwamba anaongea sana hivyo anaweza kuanzisha chama cha kuwasuta watu na kikawa kizuri sana, lakini pia hakusita kumshukuru mke wake na kumtania kwamba leo walipoamka asubuhi alimsalimia kwa kumtania na kusema "Mambo Kamanda naye Steve Nyerere akajibu Poa mke wangu"
Mjumbea wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Mkoani Mara na mgeni rasmi Bw. Domi Athman Juma akimvisha joho Kamanda mpya wa vijana wa tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele maarufu kama Steven Nyerere leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika tawini hapo na kuhudhuriwa na wanaccm mbalimbali wa kutoka tawi hilo.





1 comments:
Wewe pamoja na blog yako ni vibaraka wa CCM, hakuna asiyeelewa hivyo. Ndiyo maana huwa hauposti comments za watu kuoga kupewa challenge. Unafiki tu huu.
Post a Comment